ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
Wana bodi salam
Nyumbani kwetu kigoma. Nimezaliwa na kukulia hapo kabla ya kuanza kusafiri kwenda nje ya mkoa wa Kigoma.
Kigoma ni mkoa ulio jirani na nchi za Rwanda na Burundi. Kwa nilivyo tembea, sijawahi kuona mkoa wowote ulio jirani na nchi nyingine wakazi wake wananyanyaswa na kubaguliwa kama wakazi wa Kigoma.
Arusha na Kilimanjaro wana mpaka na Kenya, lkn wananchi wa huko hawanyanyaswi.
Mara wana mpaka na Kenya lkn wananchi wake hawanyanyaswi
Mbeya na Songwe zina ujirani na Malawi na Zambia lkn wananchi wake hawajui kunyanyaswa na mamlaka za Tanzania.
Mtwara wako mpakani lkn hautasikia wananyanyaswa na kubaguliwa kama ilivyo kwa wakazi wa mkoa wa kigoma.
Huwa najiuliza shida ni nini? Je, Tanzania inaogopa mataifa ya Rwanda na Burundi na hivyo kuwachukulia wakaazi wa nchi hizo kuwa hatari?
Fikiria ubaguzi ufuatao:-
1. NIDA-Katika mikoa ambayo wameandikisha watu wachache, Kigoma huenda inaongoza. Kigoma kusajili line wachache wanasajili kwa majina yao, wengi hutumia usajili wa waliofanikiwa kupata Nida. Hii ni kinyume na sheria. Sababu? Eti wanaepuka kuandikisha wakimbizi.
2. Uhamiaji. Kigoma ni mkoa pekee ambao idara ya uhamiaji wana vizuizi vya kukagua vitambulisho. Natambua pale Bunda wapo, lkn hukagua wanaotoka sirari zaidi.
Kigoma, ukitoka pande yoyote ya nchi, kuingia mkoa wa kigoma, utadaiwa kitambulisho au passport. Ni kama unaingia nchi nyingine kabisa.
Vivyo hivyo ukitoka kigoma kwenda mikoa mingine, huvuki mkoa bila kuonesha kitambulisho. Ni kama vile kigoma ni nchi na hivyo taratibu za kuvuka na kuingia kigoma, zinatumika sawasawa kama kuvuka na kuingia nchini nyingine za kigeni.
Kama ndivyo, kwa nini kigoma isiwe nchi ili tupambane na maisha yetu wenyewe?
Haiingii akilini tume ya uchaguzi kwa kuwa mnataka wapiga kura, wakazi wa kigoma huandikishwa bila ubaguzi sana lakini kwenye NIDA achilia mbali kupata passport waanze kubaguliwa. Mnatukera sisi wa kigoma.
Mnaboa sana