Tumeona baadhi ya wanachama wa vyama wakikimbilia mahakamani kutafuta haki kwa nafasi zinazohusu uongozi ndani ya vyombo vya dola kama bunge na serikali kama ilivyotokea kwa wabunge 19 wa CHADEMA.
Hapa tunaona wabunge wanaweza kukimbilia mahakamani kutafuta haki ambayo pengine wasingeweza kupata kupitia kamati/vikao vya vyama vyao. Je, kwa nini usiwepo utaratibu wa kupya atikana kwa haki nje ya haki kutendwa na kamati za maadili kwa wanachama ambao nafasi zao hazitokani na vyombo vya dola?
Sitaki kukumbusha ya nyuma lakini tunaweza kuanzia kwenye suala la Membe, mzee Kinana ili tupate kwenye ufumbuzi. Binafsi ninaamini kwa masuala ya kimaadili ya mwanacham si vyema yakajadiliwa na kuamuliwa na kamati zinazohusiana na chama moja kwa moja na badala yake kiundwe chombo huru kama mahakama kwa ajili ya maamuzi na hii itaondoa uminywaji wa haki.
Kwa kinachotokea sasa kwenye kesi ya wabunge 19 was CHADEMA ni matokeo ya kutokuwa na utendaji wa haki wa kamati za maadili ya chama na ni vizuri wao wana upande mwingine wa kupata haki. Hivi inakuja akilini kweli wajumbe wa kikao kilichoniadhibu wajumbe haohao wanavaa uhusika mwingine wa kunisikiliza ?
Natambua eneo hili ndio linafanya wanachama kuumia bila kuwa na pa kusemea kama nafasi zao hazitokani na vyombo vya dola.
Tunaweza hata kuanzisha tawi mahakama kuu kwa ajili ya kusikiliza mashauri ya namna ama kukawa na chombo huru cha kusikiliza mashauri ya namna hii na sio kutegemea kamati za maadili za vyama na kwa kufanya hivi ni kama kesi ya ngendere kula mahindi amepelekewa nyani ahukumu