Ndugu Mwigulu L Nchemba,
Nimelazimika kukuandikia hii thread kukuuliza swali kwamba UNAJISIKIAJE KWA HAYA YANAYOTOKEA na unahusishwa nayo?
1. Katika uchaguzi wa Igunga kuna mwananchi alimwagiwa tindikali na taarifa zilionyesha kwamba ni kati ya watu uliowakodi kwenda kufanya fujo na katika kugombani malipo uliyowapa kwa niaba ya chama, ndipo alimwagiwa tindikali na wenzake.
2. katika uchaguzi wa Igunga kuna mauaji ya mfuasi wa CHADEMA yalipotokea pia ulihusishwa kwamba uliratibu kazi hiyo.
3. Katika uchaguzi wa Igunga pia ilisemekana kwamba wewe ulikamatwa na mke wa mtu ukizini naye.
NB1: Katika yote hapo juu, haujawahi kutokea hadharani na kukanusha kwamba hauhusiki na hayo matukio ya kutisha hapo juu, hivyo sisi kama wananchi na vijana wenzako TUNASHAWISHIKA kuamini kwamba ni kweli ulihusika na matukio hayo hapo juu.
4. Uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki pia ulihusishwa na uratibu wa mauaji ya mwenyekiti wa CHADEMA aliyechinjwa, kwasababu wewe ndiyo ulikuwa mratibu wa shughuli za uchaguzi kwa CCM. Hili nalo unasemaje?
5. Maafa yametokea tena Singida na kwa taarifa za awli zinaonyesha kwamba kuna timu uliunda na kuwalipa na mbaya zaidi umewaambia wanywe pombe ili conscious zao zisiwe sahihi ili wafanye fujo kwenye mkutano wa CHADEMA, na matokeo yake mmoja kati ya vijana wako amepoteza maisha. Nazidi kujiuliza kwamba wewe kama kijana mwenzetu, kama haya matukio ni ya kweli kwamba unahusika, je unajisikiaje nafsini mwako unapokuwa unajihusisha na URATIBU wa shughuli hizi ambazo zinagharimu maisha ya Watanzania wenzako?
Mwigulu,
Napata shida sana jinsi ninavyokufahamu toka ukiwa UDSM na ulipogombea urais wa DARUSO na kushindwa na hata ulivyokuwa unafanya kampeni zako, je ni kweli hii ndiyo tabia yako ilivyo na ulitaka kupeleka jumuiya ya UDSM kwenye maafa kama haya yanayotokea na wewe umeendelea kuwa part and parcel ya haya matukio ya kutisha yanayohusisha kupoteza maisha ya watanzania wenzetu.
Mwigulu, mara ya mwisho mimi na wewe kukaa meza moja ilikuwa ,mwaka 2009 kwenye kikao cha maandalizi ya harusi ya kijana mwenzetu pale baa ya Sinza lkn mpaka muda huo ukiwa bado mtumishi wa BOT, ulikuwa na uwezo wa kuongea mantiki na si kama unavyofanya sasa ambapo katika maneno 100 unayoongea, basi 90 yote ni UONGO NA UNAFIKI na 10 pekee katika 100 ndiyo ina ukweli ndani yake.
Mwigulu,
Naomba nirejee swali langu la msingi, kwamba unajisikiaje nafsini mwako kwa haya matukio ya kutisha yanayohusisha kupoteza maisha ya watu ili mradi tu uonekana shujaa mbele za watu?
Je, nafsini mwako una AMANI kabisa hata kama CCM na serikali inakulipa pesa ambazo unakula na kusaza? Je, familia yako nayo ina amani kwa haya mambo unayohusishwa nayo? Je, haya matukio unayoshiriki sasa hayajakufanya uanze kunywa pombe kali kali ili japo ujiliwaze na siyo kuyakumbuka akilini mwako kila wakati? Na kama sivyo, je unatuhaminisha kwamba wewe kwako siyo tatizo unapohusishwa kwenye matukio yanayopoteza maisha ya watanzania wenzako?
Swali langu la mwisho kwako; Je, kama ni kweli unashiriki (KWANI NAFSI YAKO INAJUA UKWELI) katika kuratibu matukio haya kwasababu ya siasa au pesa, je utaendelea nayo mpaka lini?
NB2: Mwigulu, naomba ujitokoze ukiwa na ID yako kamili au ile nyingine ambayo ulikuwa unatumia kujibizana na dada yetu J. kwenye thread za leo na unipe ni kwa namna gani unavyojisikia nafsini mwako.
Kwa wale vijana wanaolipwa na Nape kulingana na idadi ya pumba wanazotuma humu JF, tafadhali msiurukie hii thread kwa kebehi kama ilivyo TOR mlizopewa na NAPE, na badala yake Mwigulu anijibu yeye kwasababu tunafahamiana naye siku nyingi hata kabla hajaingia kwenye ubunge.