Rais Kikwete na Lowassa hawakukaa chini kuzungumza baada ya tuhuma nzito zilizotolewa Bungeni na hasa maneno makali ya Wabunge mbalimbali. Kwa yeyote aliyesikiliza hoja za Wabunge ni wazi kuwa Waziri Mkuu alikuwa implied na kuna waliothubutu kutaja na majina kabisa.
Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu si jambo dogo hata kidogo hata kama mtu humpendi. Moja ni kwa sababu za kikatiba na jingine ni suala la gharama.
Kikatiba, Waziri Mkuu anapojiuzulu Baraza la Mawaziri linavunjika na hivyo Rais anatakiwa kuanza mchakato mpya wa kupata Waziri Mkuu mpya na Baraza jipya la Mawaziri. Sasa kama Taifa hatuwezi kuruhusu iwe rahisi kwa Waziri Mkuu kujiuzulu na kuanza moja kila inapotolewa tuhuma dhidi yake. NI lazima Rais (anayemteua Waziri huyo) kuwa na msimamo unaoeleweka ili wananchi waridhike kuwa kweli kosa fulani la Waziri Mkuu linamstahilisha kujiuzulu.
Sasa Waziri Mkuu anapotolewa tuhuma nzito ni wajibu wa Rais kumuita na kumsikiliza kabla Waziri huyo hajafanya uamuzi wowote wa papara (kama wa Lowassa). Kwa wanaokumbuka Rais alikuwa mikoa ya Kusini na Makamu alikuwa sehemu nyinyine na wao kama Taifa zima walisikia kujiuzulu kwa Lowassa "radioni". Kwanini Kikwete hakumuita Waziri wake Mkuu na kuhoji tuhuma dhidi yake na kusikia utetezi wake?
Mkuu naamini huna uhakika wa hili. INASEMEKANA kwamba, Rais alikutana na PM wake na kuongelea mambo haya.
Kwa taratibu, katika hoja za nguvu kama zilivyotolewa na wabunge, Kamati Kuu ya NEC hukutana na kujadili nini cha kufanya. Inasemekana kuwa, CC-NEC ilimtaka PM ajiuzuru ili kulinda heshima ya Rais na Serikali. Hapo ndipo PM alipomuuliza Rais nae akasema sina pingamizi. Hivyo uamuzi wa PM ukawa ni kujiuzuru.
Wakati kikao cha Bunge kikizungumzia masuala ya Richmond, Makamu wa Rais alikuwa Arusha na Rais alikuwa Dar. Wote walikutana Dodoma kabla hata PM hajatangaza kujiuzuru. Rais alikutana na Kamati Kuu ya CCM Taifa kabla hata PM wake hajajiuzuru. Na kuna tetesi pia kuwa, Rais alishaamua kuwa atamteua MPP hata kabla EL hajajiuzuru.
Kigharama, kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kunasababisha gharama zisizo za lazima za kuunda Wizara mpya au kuingiza mawaziri wapya. Kikwete alilazimika kuunda wizara mpya na kuleta mawaziri wapya na yote hayo yana gharama. Hivyo, hatuwezi kuchukuliwa kwa urahisi tu kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kana kwamba ni kitu kidogo.
Kweli kabisa
Pia watu wanasahau kikao alichofanya Rais Kikwete na wazee wa Dar kuelezea mshtuko wake wa kujiuzulu kwa Lowassa. Tukumbuke kuwa Kikwete hakusema Lowassa amefanya makosa yoyote na alisema kuwa kujiuzulu kwa Lowassa kulikuwa ni kwa "ajali ya kisiasa". Sasa kama Rais alijua Lowassa hakufanya makosa kwanini hakusimama naye na kuepusha maamuzi ya kisiasa?
Je, tunaweza kukubali hizi "ajali za kisiasa" kwa kushindwa kuzizuia?
Rais hakushtushwa na kujiuzuru kwa EL hata kidogo. Ila naweza kusema alisikitishwa kwa uhakika.
Ni lazima tuzoee kuwa kujiuzuru katika dhamana ya umma ni jambo la lazima kama umevunja sheria za nchi au sheria za utumishi wa umma. Haiwezekani watu wakamezeana kwa kila jambo baya linalotendwa kwa kuogopa gharama ambazo zingeweza kukwepwa kwa kufanya uteuzi makini na kuwa na control kwa watu wanaoteuliwa.
Kama hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa Lowassa kunufaika na mkataba wa Richmond, kama hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kuonesha kuwa Lowassa ndiye Richmonduli, kama Kamati haikuweza kuonesha kuwa mtoto wa Lowassa ndiye alihusika na Richmond na kwa mujibu wa sheria ya Maadili huo ni mgongano wa Maslahi kwa Lowassa, ninajiuliza Lowassa alijiuzulu kwa sababu gani hasa?
Inavyoonekana ni kuwa EL alijiuzuru kwasababu asingefanya hivyo Bunge lingeweza kumtaka ajiuzuru kwa kupiga kura za kutokuwa na imani nae. Uwezekano huo ulikuwepo. Hivyo, aliona ni busara zaidi kujiuzuru kuliko kulazimishwa kwa njia ya kura za maoni za Wabunge.
Nakubaliana na wewe sana kuwa, kama Rais angeamua kuliomba Bunge kuelewa kilichotokea, kwa yeye kuwa na imani kwamba hakukuwa na makosa yaliyofanywa moja kwa moja na waziri wake Mkuu, Bunge lingeweza kutoa onyo kali kwa PM na mambo yangekwisha na EL angeweza kuwa PM hadi leo.
Jibu ni kuwa Lowassa alijiuzulu ili kumkomoa Kikwete! Alijiuzulu kama spite ya Kikwete na urafiki wao; hakujiuzulu kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kwa sababu rafiki yake, mtu aliyehangaika kumuweka madarakani na mtu ambaye kwa kiasi kikubwa ni mshirika wake wa kisiasa alimtosa wakati alipotakiwa kusimama naye.
Hili pia linawezekana. Japokuwa kwa kufanya hivyo hakumuongezei/hakukumuongezea sifa yoyote ya maana kisiasa.
Je, ina maana kwa Kikwete kusimama na Lowassa kunamfanya Lowassa asiwe na makosa? Na kama alikuwa na makosa ni kweli yalimstahilisha ajiuzulu kwa namna ile ya utekaji nyara nchi?
Hapana, naamini kuwa kama Rais angesimama na EL katika yaliyomkuta, kusingefuta makosa yoyote ya EL, hata kidogo. Kwa kutegemea jinsi gani Rais angesimamia hoja, kungeweza kumuingiza Rais katika kashfa ile (angekuwa amenunua kesi) na angeweza kupoteza imani ya wananchi kwake, ama kungeweza kuisafisha serikali yake vizuri sana. Yote yanawezekana. Ila uangalifu mkubwa ulihitajika katika kuamua Rais awe upande gani. Nadhani pia alishauriwa aachie uhuru wa Bunge kufanya kazi yake.