Kwanini Kenya wanapenda sifa sana?

Kwanini Kenya wanapenda sifa sana?

100_1962.JPG
nairobi-metro-pic1.jpg




mvua_dar.jpg

biz+index+pix.jpg
02_11_vrpc2j.jpg
 
NasDaz Nyerere ndio aliyejenga Reli ya TAZARA, reli hii kwakweli ilikua ya kisasa kweli enzi zile, mara ya mwisho nilipanda mwaka 1994 nilipokua nasoma kule Iringa, enzi ya Nyerere huyo huyo ndie aliyeongeza kipande kilicho achwa na mkoloni cha reli ya kati kuja Ubungo maziwa, mahali ambapo Mwakyembe amezindua huo unaoitwa mradi kuondoa kero za Barabarani jijini Dar, Kenye wame copy mfumo wa elimu bure toka kwa Nyerere ambaye wakati huo (enzi za Moi) walikua wanatudharau sana kwakusema, kama unapenda vitu vya bure, hamieni Tanzania, leo hii hata ccm nao wanataka kurudi kule, kama tumewahi kupewa chakula cha bure, kama nitakosea, watu wazima naomba mnisahihishe, ilikua ni mwaka 1982 nafikiri, hii ni mara baada ya ukame mkubwa kuikumba nchi yetu, enzi za Nyerere kulikua na akiba ya chakula cha kutosha kabisa, kuna vihenge vilijengwa pale Iringa, Dar, Mbeya na hata mashirika kama NAFCO yalifanya vizuri sana, enzi za Nyerere, (naomba mwongozo wako hapa) pembejeo gani za kilimo tulikua tunanunua toka nje? Nakumbuka tulikua na viwanda kama UFI Dar pale, ZZK Mbeya, kiwanda cha madawa ya mifugo na mazao Moshi /Arusha, Pareto Mafinga, Karatasi Mgororo-Iringa, Mbolea Tanga n.k Kama sikosei, wakulima wa Pamba wa Kanda ya Ziwa hasa Maswa, Bariadi n.k, walikua wanauwezo wa kufanya vitu vingi tu kwa kutegemea Kilimo sababu, soko lilikuwepo, viwanda vya nguo vilikuwepo karibu kila mkoa unaozalisha Pamba, Wahaya waliweza kusomesha vijana wao kwa kilimo cha Kahawa.

Nataka niseme hivi, enzi za Nyerere, vitega uchumi vilikua vichache sana na vipaumbele vilizingatiwa, nikiwa mdogo, niliona huo ujenzi wa Barabara unaousema ulifanyika pia enzi hizo, Barabara ya tokea Makambako to Songea, ulifanyika enzi za mzee huyu, Bwawa la Mtera, Kidatu n.k. Yote haya Nyerere alikua akifanya ilihali akipata upinzani mkubwa sana toka nchi za Magharibi na Africa ya Kusini, inawezekana siasa ya Ujamaa ndio tatizo, lakini tujiulize, hivi mara baada ya kuingia Ubepari huu leo, nchi inasonga au inarudi nyuma? Thamani ya Tsh dhidi ya Dola ilikua 1:40, karibu kila kinacho sababisha pesa leo, kilianzishwa na Nyerere, aliweka msingi, tena Imara but mchwa wamekuja, wanatafuna kweli, hiki kinacho onekana kama wamefanya ni tone tu la kile tulichotakiwa kukiona!

I am also an Independent thinker and not pro anybody!
 
Last edited by a moderator:
Mazindu Msambule According to Nyerere "Ili tuendelee twahitaji 5 things"
1. Watu
2. Siasa safi
3. Uongozi bora
4. Maji
5. Ardhi
 
Last edited by a moderator:
hakika hii topic na mtiririko wa picha unadhihilisha jina la great thinkes, nahisi tumo humu tunaojua kuwaza vzuri na hata kutenda ili kuleta maendeleo but unfortunately hatutambuliki mungu wangu,.....tulio wapa madaraka watusukume sidhani hta kama theluthi yao ina upeo wowote ule zaidi ya kukosa confidence na kutenda kwa mazoea, haingii akilini waziri mzima hajui nchi ya tanzania ni muungano wa nini na nini.......nashauri post kama hizi angezisoma kikwete laivu ajifunze na kuamua kutenda....mimi nimeumbwa na aibu mfano nikimtembelea rafiki yangu nikamkuta anayo nyumba nzuri, gari, biashara, fenicha n.k huwa napata aibu sana.... nikirudi nyumbani nakaa chini naanzisha plan za kumfukuzia kimaendeleo nimfikie, ajabu maraisi na mawaziri wanasafiri kila siku, je hawaonagi maendeleo ya wenzao na kuingiwa na aibu ili wajipange kufukuzana nao.....jamani nipeni hata ubunge wa msoma vijijni niokoe nchi hiii inatia aibu, aibu, aibu.
 
NasDaz Tangu 1885 hadi leo hawakupata kubadilisha mkoloni!
 
Last edited by a moderator:
sisi ndo tunapenda sifa ya amani ya uongo lakini matatizo hatuyaangalii......amani ipi tulionayo tanzania? kama kuna amani kwa nini majumba mengi yamezungushiwa electric wire fence, kwa nini nyumba nyingi pameandikwa kuna mbwa mkali, kwa nini nyumba nyingi zina mageti makubwa makubwa tena ya chuma? nachukia kuon a zinajengwa kilometa mia za barara nchi nzima ndani ya mwaka mzima basi tunajisifia kwambwa tunathubutu kutenda, hii aibu hapo ni sawa na kuwapa watoto wako zambarau moja moja kama mlo wa siku nzima then unasimama mbele za majiran zako kwamba unalisha vizuri sana familia yako..........upuuuzi mtupu kujenga kijisehemu cha barabara na kuwaambia mawazii waseme kwa wananchi kwamba nini walichokifanya, nao bila aibu wanasimama na lundo ya makaratasi mikononi eti wanasoma report, mi ni mdogo sana kwenu but i think further more zaidi ya ya hayo kiduuuuuchu myatendayo na kujisifu, wenzenu wana tabia wakimgundua mtu fulani ana uwezo wa kitu fulani basi watamtunza na kumwendeleza kwa maendeleo ya taifa, lakini tanzania ukitenda zaidi ya mazoea utafungwa, utafuatwa fuatwa, utaambiwa unachezea amani....pssxxxxxxxxyy
 
kama katika mikataba ya kimataifa kungekuwa na utaratibu wa kubadilishana viongozi walau kwa miaka mitano tu, basi tungezungumza na majirani zetu wakenya ili watupatie viongozi wao kwa miaka kama mitano angalau watukomboe na udumavu wa kimaendeleo tulionao. Sisi tungewapa hawa vilaza wetu ili angalau wawafundishe jinsi ya kuongoza kimaendeleo na wala si kwa maslahi ya matumbo yao. Hivi sisi watz ni nani aliyetuloga mpaka tukahukumiwa kuwa na viongozi vilaza kama tulionao?
 
Ninaona (kwenye nyekundu) unahangaika kuelewesha mambo ya std 2!! Hutaki kuelewa kuwa uongozi unaofuatilia unaweza kubomoa kazi za uongozi uliopita! Kwa taarifa yako Kenya wanaamini kuwa MOI alipangua na kuharibu kazi zote za Kenyata!! Utashi wa kisiasa ni jambo linaloweza kuleta faida au hasara!! hebu ona tawala zote!! baada ya Nyerere! Umeshaelewa akiba na pato la taifa lilikuwaje Ruksa alipokabidhiwa Nchi? Basi Ruksa alikula akiba!!/mbegu zaidi ya hapo akaenda ZNZ kunajisi hata ule mfumo wa kuhakiki unaopigania maskini. Ben aliweza kuimarisha Uchumi kidogo lakini akaharibu katika kuendekeza Rushwa! na kuuza mashirika kiholela! . Kwa sasa majibu yako kwa wote!!

Well said
 
Watu wanakuja na theory nyingi sna kuelezea vitu vidogo.Siku hizi hakuna tena hizo phase mnazozisema.maendeleo ya nchi siku hizi yana phase za kujitengenezea.Kama Mkapa alipunguza na kuondoa deni.Kikwete alipaswa weka akiba na si kufuja,kwani zoezi la kufuta deni si mchezo mrahisi nakurudisha deni ni kama mlevi anayeombea na kutubu huku akijiapiza kutolewa then baada ya kukutana na pombe bishara inaisha na kuokotwa ktk mitaro.

Sasa uchumi wa nchi ni kama daladala zinazofukuzana njiani, kila mmoja anampita mwenzi e akipakia na yeye anapitwa akishusha au kupakia kituo cha mbele.Sasa kama tz wanapakia na kushusha huku wanapiga story na mteja ni wazi wataachw avituo vingi sana na mwishowe hawataweza wahi popote tena.

Hila zinzoibwa nchini kila kukicha zinaweza jenga dar na miji mingine vyema sana na kuiacha Kenya,vipaumbele vya kijinga tunavyojiwekea navyo ni hasara yetu.Pamoja na kutokuwa waangaliafu au kutumia fursa tulizo nazo ndipo knapotulekea kuachwa miaka hii ya karibuni.N ahii haihusiani na wakoloni wala nini?Serikali haina popote inaporudhusu watu kufanya biashara na wakenya ina an official ways, sasa imefikia mahali wakenya wananunua madini, mbao, mazao mengine toka vinapozalishwa na kupeleke Kenya ambapo wanakwenda pata superprofits.Hizi faida zinaongeza mitaji yao nakuwafanya wawe na uwezo wa kuwahi opprotunities kadii zinapvyotokea kuliko sisi na masuperstar wetu wa siasa wa type ya le-mutuz.
 
Moja ya malengo ya Kenya Vision 2030 ni kuifanya nchi ya kenya kuwa information tech. hub ya Africa. Lengo hili litafikiwa kwa kuimarisha miundo mbinu ya mawasiliano ikiwemo mikonga. Baada mapinduzi ya kilimo, yakifatiliwa na mapinduzi ya viwanda ,dunia ipo kwenye wimbi la mapinduzi ya mawasiliano. Kenya imeliona hili mapema.
 
l

Bado nasisitiza, huwezi kuilinganisha Kenya na Tanzania leo hii kwavile Kenya walianza kujenga na kuusimamia uchumi wao miaka kadhaa iliyopita!! Ingawaje ni kweli kwamba Nyerere alijenga viwanda vingi sana lakini ukweli ni kwamba viwanda vingi havikuwa na efficiency na vingi vilikufa enzi za utawala wake

Huu ni uongo uliopitiliza,Viwanda havikufa kipindi cha Kambarage
 
Hawa viongozi wetu kwa kweli ni mzigo wa misumari tumebebeshwa..Inafika mahali mtu unakuwa not proud to be Tanzanian..Unaona aibu kwa kweli..

I hope haunisemi mimi,Nafivumilia sana kuwa mtanzania dada angu hii nchi ina madudu mengi sana
 
Back
Top Bottom