Mwanangu NasDaz ingawa kuna jembe kidogo za ukweli katika unayosema, nadhani wakati wa kumlaumu Nyerere umepita. Mie nadhani kusema eti Ujamaa ulitukwamisha si kweli. Tatizo ambalo hutaki kulikubali ni kwamba watawala wetu tangu Mwinyi ni wezi na wasio na visheni. Haiwezekani Kenya nchi isiyo na madini wala ardhi kama yetu watuzidi halafu tuanze kusingizia miaka 30 iliyopita. Nyerere aliacha mtandao mzuri wa kuweza kuendeleza nchi haraka. Hakuna kitu muhimu alichofanya Nyerere kama kulinda raslimali zetu ambazo leo watawala wetu wanazigawa kutokana na upogo. Hiyo Kenya unayosifia kuna kipindi inatumia raslimali zetu kama vile Tanzanite kujiingizia kipato. Nimalizie kwa kusema kuwa tatizo la Tz siyo Nyerere bali watawala vipofu na wezi.
Ewe Mzazi wangu,
Lazima nikubaliane nawe kwamba wakati wa kumlaumu Nyerere umepita lakini vile vile itakuwa si haki kueleza hali ya kiuchumi wa Tanzania bila kutaja awamu ya kwanza!! Baba angu; nafahamu wazazi wengi hampendi kusikia mtu akisema baya kuhusu utawala wa Nyerere, lakini hilo katu haliepukiki kwanini misingi ya nchi hii inatokana na utawala wa awamu ya kwanza! Mwalimu alikaa madarakani miaka 24 hivyo miaka yake madarakani ilikuwa na impact kubwa sana politically, economically and even socially!! Mbona tunapotaka kuzungumzia hali ya utulivu na mamani nchini tunapenda ku-refer mazuri yaliyofanywa na utawala wa Mwalimu lakini tunapotaka kuzungumzia mengine mnatukanya tusiwasemange marehemui?! Hebu nijuze babangu kutkana na busara ulizonazo kama mzazi!
Tukirudi kwenye suala la Ujamaa; si kwamba nasema matatizo yalitokana na mfumo wa Ujamaa bali ile hali ya kufanya njia kuu za uchumi kuwa fully controlled by the government na matoke kukawa hakuna efficiency kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi. Na ndio maana nikasema ingawaje KANU ilikuwa ni SOCIALIST part part lakini Kenyatta ali-practice mixed economy ili kuongeza efficiency kwenye sekta ya uchumi!!
Baba, na wale wenzako wote ambao mnaamini kwamba wakati wa Nyerere mambo yalikwa safi naomba niwaulize jambo moja:
ASSUME panatokea muujiza ambao Mungu anaamua kusimama at a certain point in Tanzania ambapo anaweza kusikika na kuonekana na kila MTanzania na kisha Mungu huyo akaongea kwa lugha itakayoeleweka na kila mtanzania; kisha akasema"
ENYI Watanzania, nawapa uwezo wa kuchagua mkitakacho.
1. Ama, nii-rewind Tanzania hadi back 1985 to the point kwamba Wote mliopo leo hii muwepo hiyo 1985 BUT economic status ya Tanzania isiwe hii ya 2012, bali iwe kama ilivyokuwa 1985!!
2.Option nyingine ni kwamba Tanzania ibaki kama hivi ilivyo 2012X
Naamii mzazi wangu utakuwa fair kwa mie kijana wako....mzazi mwenye busara ni yule asiye tayari kumwongopea mwanae! Je babangu, ungechagua lipi kati ya hayo?! Hivi kweli kutakuwa na Mtanzania yeyote atakayetaka TZ iwe rewinded back 1985?! Am afraid nobody, labda Kingunge ili arudi zama za CHAMA KUSHIKA HATAMU!!!