Tuache unafiki, tusijifanye hatufahamu chanzo cha Tanzania kuwa hapa ilipo hata baada ya miaka 50 ya Uhuru! Chanzo cha haya yote ni utawala wa Nyerere ingawaje wapo wasiotaka ukweli huu usemwe na kwamba yeyote atakayesema basi mtu huyo ana chuki na Nyerere!!! Mbaya zaidi, wapo wengine ambao wanafikia kiwango cha juu kabisa cha kushindwa kuficha upumbavu wao kwa kudai eti "Nyerere anachukiwa kwavile ni Mkristo!" RABISH!
Kiuhalisia kabisa, hivi sasa Kenya wapo kwenye second phase ya maendeleo yao. First phase, walishaifanya soon after uhuru wa nchi yao. Wakati wenzetu walianza mapema baada ya Uhuru, Tanzania ikatumia kipindi hicho katika kujishughulisha na ya wenzetu kwa kile tulichoita Kuhakikisha Ukombozi wa Afrika!!
Hata kama hilo nalo si jambo la kubeza, lakini tulitumia raslimali nyingi mno katika suala hilo. Mbaya zaidi, suala la Ukombozi Kusini mwa Afrika tulilisimamia vizuri zaidi kuliko tulivyoweza kuyasimamia mambo yetu wenyewe! Kwani, ingawaje utawala wa Nyerere ulijitahidi kufanya uwekezaji hapa nchini, lakini bado utawala huo ulishindwa kabisa kusimamia yale iliyoyaanzisha!!
Utawala wa Nyerere ulikuwa very efficiency katika kusimamia suala la ukombozi lakini ulikuwa very poor katika kusimamia mambo yake yenyewe! Matokeo yake, nchi ikageuka kuwa omba omba wa aibu, yaani hadi kufikia kuomba omba chakula na kuishia kuletewa hadi mahindi ya njano yanayosemekana yalikuwa ni chakula cha mifugo huko yalikotoka!
Wakati sie tukiitumia first phase kwa staili hiyo, wenzetu Kenya wakajikita kujenga uchumi wao! Wakatumia every available opportunity (including human resources, entrepreneurs) katika kujenga uchumi wao!! Wakajenga mashule, vyuo, viwanja vya ndege, barabara and almost every possible and necessary infrastructure. Pamoja na ugonjwa wa ufisadi uliopo in almost every African Country, lakini bado Kenya waliweza kuyasimamia waliyoyaanzisha; jambo ambalo sie lilitushinda!
Baada ya Nyerere kuondoka madarakani 1985, ndipo Tanzania ikaanza kufanya kile ambacho ilitakiwa kifanywe 20 years back!! And in fact, real move ikaanza baada ya Mkapa kuingia madarakani in 1995; huku ikiwa imeshapita zaidi ya miaka 30 ya uhuru! Kila ambacho Mkapa alijaribu kukifanya, tayari Wakenya walikuwa wameshakifanya more than 20 years back!!
Watu leo hii wanajaribu kudhihaki Treni ya Mwakyembe kwavile tu Kenya wamezindua Treni ya kisasa zaidi! So what did you expect?! Haya yanayofanywa na Mwakeymbe leo hii yalikuwa yawe yamefanyika more than 20 years back!
Ingekuwa ni kichekesho leo hii kufikiria kuwa na treni za kisasa kabisa wakati hata barabara za kupita magari ya kawaida hamna!! Itakuwa ni kichekesho kuwa na Super Highway wakati hata ordinary roads ambazo zilitakiwa kujengwa zaidi ya miaka 30 iliyopita bado hamna!
So, tu cut story short, haya yaliyopo sasa ni matunda ya sera za Nyerere! Wakati Kenya ipo kwenye second phase, or innovation phase, sie ndo kwanza tunaanza! Hata hivyo, am very sure kwamba, sooner or later tuna kila sababu ya kuiacha Kenya.