Kwa nini unasema mshindani wetu mkubwa ni Kenya? kivipi?
Nijuavyo mimi Bandari yetu hutumiwa (zaidi) na Nchi za Zambia, Malawi, Kongo, Burundi na Rwanda na hii ni kwa sababu za Kijiografia na sasa hivi Zambia na Malawi wanataka kuhamia Beira Msumbiji pale Miundo mbinu yote itakapo kamilika, kama bado haijakamilka hivyo anayekula Ugali wetu hapa kwenye upande wa Bandari ni Beira (Msumbiji) na SIYO Mombasa, kwa maana tunagawana wateja wa Malawi na Zambia, sasa Kenya tunagawana wateja gani? Momabsa wateja wao wakuu ni Uganda na Sudani na labda Ethiopia!
Kumbuka hapo naongelea Mizigo yenye Ujazo mkubwa na SIYO kufurushi kimoja kimoja!
Na kwa nini tusiweze kushindana au kuwa na Malengo ya kuwa na Bandari kama Durban au Djibouti? ukichukulia Durban ni Bandari Bora Afrika kama moja ya Bora Duniani?
Lazima ujipime najirani yako bwana