Kwanini katika Nchi zote Afrika, ni Kenya tu!

Kijakazi

Platinum Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
10,428
Reaction score
17,747
Hivi ni kwanini ktk nchi zooote barani Afrika zaidi ya 50, Watz wengi hupenda kujipima na kujilinganisha na Kenya tu?
Na hii ni kuanzia Viongozi mpaka Wananchi yaani kwa mfano kuna nchi nyingi sana Afrika ambazo zinaizidi Nchi yetu kiuchumi kwamba zina Uchumi mkubwa kuliko wetu, sasa ni kwa nini tuwe tunajilinganisha na Kenya tu?

Hata kwenye malengo ya Nchi utasikia Viongozi (wetu) mwaka fulani tutaipita Kenya, hata kama tukijenga Kiwanja cha mpira utasikia ni kikubwa AM nzima (na hapo wanamaanisha nchi mbili tu UG na hasa Kenya), hata kama ni ukumbi wa Disko tu utasikia ni mkubwa hata Kenya hamna, kwanini tusiseme hiki Kiwanja ni kikubwa Afrika Nzima?

Hata kwenye bandari lengo ni kuizidi Bandari ya Mombasa tu, sasa kwanini isiwe kuwa na Bandari kubwa na yenye ufanisi kushinda zote Afrika nzima? yaani tushindane na Beira, Durban, Djibouti n.k ni kwa nini Kenya tu?

Ukija kwenye Reli ni hivyo Mshindani na wakujilinganisha naye ni Kenya tu! Kwanini isiwe Kongo, Zambia, Malawi, Zimbabwe, Ethiopia n.k

Ukija kwenye Utalii ni hivyo hivyo lengo SIYO kupata watalii wengi kuliko nchi zote Afrika, hapana bali ni kuwa na Watalii wengi kuliko Kenya, sasa ni kwanini? Kwa nini Siyo lkuliko Zimbabwe au AK au Misri?

Kuna anaye jua sababu hasa, ni kwa nini Kipimo chetu ni Kenya tu? Na je kama tukifanikiwa kuwazidi Kenya Kiuchumi, tutakuwa tumefanikiwa nini hasa?
 
..ni kwasababu wa-Kenya nao wanapenda kujilinganisha na sisi.

..pia Kenya ndiyo mwenye ahueni kiuchumi kuliko nchi zote majirani zetu.

..pamoja na hayo nakubaliana na hoja yako kwamba, as a country, we need to dream bigger.
 
Wao ndo competitor wetu kwenye nyanja nyingi za kiuchumi. Kwa hiyo ni lazima kuhakikisha kwanza competitor wetu tunawapita then tunaende mbele zaidi.

Hatuna haja ya kushindana na mtu ambaye hana ushindani kwetu kiuchumi...
 
Ni kawaida ya viongozi au watu wanaopenda kuiga na kuishi ndoto za wengine. Hawana dream yaani hao watu hawana uwezo wa kubuni lao. Ni watu wavivu kufikiri na wanaona kila kitu hakiwezekani. Hatuitaji pesa kufanya mambo makubwa tunahitaji mipango mizuri. Nchi hii chini ya utawala wa sasa kuna mtu mmoja tu ambaye nimeona kidogo anacho hicho ninachotaka kusema. Huyu ni Neemia Mchechu peke yake.
 
Hivi ni kwanini ktk nchi zooote barani Afrika zaidi ya 50, Watz wengi hupenda kujipima na kujilinganisha na Kenya tu?
Na hii ni kuanzia Viongozi mpaka Wananchi yaani kwa mfano kuna nchi nyingi sana Afrika ambazo zinaizidi Nchi yetu kiuchumi kwamba zina Uchumi mkubwa kuliko wetu, sasa ni kwa nini tuwe tunajilinganisha na Kenya tu?

Hata kwenye malengo ya Nchi utasikia Viongozi (wetu) mwaka fulani tutaipita Kenya, hata kama tukijenga Kiwanja cha mpira utasikia ni kikubwa AM nzima (na hapo wanamaanisha nchi mbili tu UG na hasa Kenya), hata kama ni ukumbi wa Disko tu utasikia ni mkubwa hata Kenya hamna, kwanini tusiseme hiki Kiwanja ni kikubwa Afrika Nzima?

Hata kwenye bandari lengo ni kuizidi Bandari ya Mombasa tu, sasa kwanini isiwe kuwa na Bandari kubwa na yenye ufanisi kushinda zote Afrika nzima? yaani tushindane na Beira, Durban, Djibouti n.k ni kwa nini Kenya tu?

Ukija kwenye Reli ni hivyo Mshindani na wakujilinganisha naye ni Kenya tu! Kwanini isiwe Kongo, Zambia, Malawi, Zimbabwe, Ethiopia n.k

Ukija kwenye Utalii ni hivyo hivyo lengo SIYO kupata watalii wengi kuliko nchi zote Afrika, hapana bali ni kuwa na Watalii wengi kuliko Kenya, sasa ni kwanini? Kwa nini Siyo lkuliko Zimbabwe au AK au Misri?

Kuna anaye jua sababu hasa, ni kwa nini Kipimo chetu ni Kenya tu? Na je kama tukifanikiwa kuwazidi Kenya Kiuchumi, tutakuwa tumefanikiwa nini hasa?

ni kwasababu ndie jirani yetu pekee aliyetuzidi, ndio kipimo cha karibu cha ushindani. Mfano: bandari ya mombasa inashindana na bandari zetu hapa EAC, hakuna zingine, hatuwezi kushindana na Durban au Djibouti. Siku zote unashindana na jirani yako, ndio maana hata Nduli Kagame anadai eti "angekuwa na bandari ya Dar.....", kwa nini asiseme bandari ya Durban?
 
Kwa nini unasema mshindani wetu mkubwa ni Kenya? kivipi?
Nijuavyo mimi Bandari yetu hutumiwa (zaidi) na Nchi za Zambia, Malawi, Kongo, Burundi na Rwanda na hii ni kwa sababu za Kijiografia na sasa hivi Zambia na Malawi wanataka kuhamia Beira Msumbiji pale Miundo mbinu yote itakapo kamilika, kama bado haijakamilka hivyo anayekula Ugali wetu hapa kwenye upande wa Bandari ni Beira (Msumbiji) na SIYO Mombasa, kwa maana tunagawana wateja wa Malawi na Zambia, sasa Kenya tunagawana wateja gani? Momabsa wateja wao wakuu ni Uganda na Sudani na labda Ethiopia!

Kumbuka hapo naongelea Mizigo yenye Ujazo mkubwa na SIYO kufurushi kimoja kimoja!
Na kwa nini tusiweze kushindana au kuwa na Malengo ya kuwa na Bandari kama Durban au Djibouti? ukichukulia Durban ni Bandari Bora Afrika kama moja ya Bora Duniani?
 
Tutashindana na Durban na Djibouti kwa mizigo inayokwenda wapi?
 
Hakuna mahali niliposema kwamba tunashindana na Durban kwa kusafirisha Mizigo ya ktk A kwenda B, bali nimeongela Ushindani wa Ufanisi na uendeshaji wa Bandari, yaani tuweze kuifanya bandari yetu iwe na Ufanisi wa kila kitu kama ilivyo ya Durban ama Misri, kipimo chetu cha uendeshaji na Ufanisi kwa nini kiwe Mombasa? ndio hoja yangu!
 
Hakuna mahali niliposema kwamba tunashindana na Durbankwa kusafirisha Mizigo ya ktk A kwenda B, bali nimeongela Ushindani wa Ufanisi na uendeshaji wa Bandari, yaani tuweze kuifanya bandari yetu iwe na Ufanisi wa kila kitu kama ilivyo ya Durban ama Misri,kipimo chetu cha uendeshaji na Ufanisi kwa nini kiwe Mombasa? ndio hoja yangu!

ohooo, nimekupata, kama ndio hivyo basi ufanisi wetu unatakiwa kujipima na the best port in the world kabisa.
 
Kenya wako serious na makini katika mambo yao ya msingi. Wanafanya kazi kwa bidii. Wanatofauti zao na ukabila lakini kwenye mambo ya msingi ya kulijenga taifa lao hawataki mzaha hata kidogo.
 
Sasa hayo uliyoandika yana Uhusiano gani na Hoja na Mada hapa?
 
Sababu Kenya ndio wapinzani wetu na watani wetu.
 
Wakenya ndio wenye kelele, kwani umezisikia nchi nyingine zikipiga kelele. Wao ndio wanajiona wanaweza kutusumbua, tunachofanya ni kujibu tu. Wewe huoni Uchumi wa Ethiopia ni mkubwa kuliko hata wa kenya lakini husikii waethiopia wakitupigia kelele?
 
Back
Top Bottom