Tanzania ingekuwa na watu kumi wanaojiuliza maswali kama muanzisha mada, jameni ingekua mbali sana kiuchumi. Nimekua Bongo na kuona uwezo wake, uwezo wa kuwa nchi bora Afrika. Lakini hili la kuona Kenya katika kila hatua ndio tatizo kubwa. Nimeona hadi hata kwenye blogs za viongozi wenu, Kenya inatajwa sana zaidi hata ya Tanzania yenyewe.
Jameni kama taifa inafaa muwe na maono na malengo yenu yaliyoelekezwa mbali. Sisi Kenya tume elekeza maono yetu yote kwenye vision2030, ambayo kila Mkenya anahamasishwa kuielewa tena kwa undani. Inafunzwa hadi vyuoni. Huwezi pata kazi inayohusu usimamizi kwenye sekta yoyote Kenya bila kuhojiwa uelewa wako wa hii vision. Unakuta tunaongea kuihusu hadi kwenye bar tukinywa mabia. Makampuni yote yameelekeza maono yao kulingana na ono hili la taifa.
Sasa ingia Bongo, Tanzania inayo TDV vision 2025. Fanya utafiti tu kwa watu watano, usiende Mazense, bali tafuta wasomi na jamaa waliotulia Mikocheni n.k. halafu waulize swali rahisi tu kila mmoja kivyake, kwamba akutajie nguzo tano za hiyo vision 2025 ya nchi, watakushangaa sana. Haya muulize swali lingine labda kuhusu miundo mbinu, kwanza ataanza na bandari inayojengwa ya Bagamoyo, na jinsi hio bandari itakavyofunika yetu ya Mombasa. Hamna lengo lingine la maana zaidi ya vile Tanzania itaipita Kenya.
Ieleweke Kenya hata kama tunashindana na ninyi kiaina, malengo yetu hayahusiani na ninyi. Tunafahamu changamoto tunazo, nchi yetu ni ndogo na nusu yake ni kame tupu tofauti na yenu yenye rotuba kila sehemu. Lakini tunajituma bila kupoteza muda wa kulalamika kuhusu mapungufu yetu.
Kwa wale kama akina
Kimweri na
JokaKuu huimba kila siku kuhusu bandari ya Bagamoyo na jinsi itaimaliza Kenya, waelewe mipango yetu haihusiani kabisa na ushindani wa hiyo bandari. Kuna hata uwezekano mkubwa Wakenya tutanufaika sana na kwa kuitumia hiyo bandari ya Bagamoyo.
Sasa mipango yetu iko kama hivi
- Tunatengeneza bandarri ya Lamu kwa nia ya kutumika na Kenya, South Sudan and Ethiopia.
- Bandari ya Mombasa tayari tunaiyachia Uganda na kaskazini mwa DRC.
- Bandari ya Lamu ina miradi minginine ndani yake kama bomba za mafuta, Reli, Barabara kuu, resort city(isiolo), power lines fiber optic cables kati ya Kenya, Ethiopia, Uganda na South sudan.
- Kuna uwekano mkubwa wa kuunganisha bandari ya Lamu hadi Cameroon na atlantic ocean. Hiyo itatuwezesha kufuatilia mizigo ya West African ambayo inazunguka cape of good hope kutoka Uchina na Asia. Ongezea Kenya airways ambayo mipango yake ni kuwa indispensable logistics hub for east and central africa.
Bandari ya Bagamoyo labda itashindana na Durban. na ukiunganisha uwezo wake na wa Mombasa na Lamu hadi na hata ya Dar, Afrika Mashariki itakua eneo muhimu sana