Kwanini kabila la Watusi halipo miongoni ya makabila yanayopatikana nchini wakati limekuwepo kwa muda mrefu?

Watutsi inasemekana siyo kabila, ila ni jamii ya watu walipofika kusini mwa Afrika. Walijizolea umaarufu wa kuwa watu wema, wakaaminiwa, wakashiriki utawala na wakawa watawala.

Neno Mtutsi, wanasema linamaanisha mtu mwema. Siyo kabila. Wana kabila zao lakini walizipoteza, ndiyo maana hakuna lugha ya Kitutsi ila kuna watu wamepewa icon ya Ututsi.

Wakiwa na kabila fulani, huchukua mila hizo na hujiita wa kabila hilo. Wakiwa Kigoma ni Waha tu. Wakiwa Buhaya ni Wahaya, Uganda ni Wanankole, Usukumani watajiita Wasukuma.
Wakiwa mara WAZANAKI
 
Watusi ni moja kabila moja kubwa hapa nchini kwetu ambalo linapatikana haswa baadhi ya maeneo hapa nchini kama vile Tabora, Mpanda, Kigoma, Geita, Kagera, Karagwe, Bukoba na Kahama.

Ukifika maeneo ya Utusini katika hii mikoa, tamaduni nyingi za Kitusi zinafahamika kuanzia uvaaji, ufugaji na watu wanaofahamika. Lakini, je ni kwanini kabila hili halimo miongoni mwa makabila 120 yanayopatikana hapa nchini? Ukiangalia hili kabila ni la muda mrefu sana tangu karne ya 21 na pia kuna watemi wengi wa Kitusi .

Lakini twende mbele turudi nyuma, ni kwanini Watusi siyo miongoni mwa makabila yanayopatikana hapa nchini?

Wataalam wa historia nisaidieni.
Hakuna kabila hilo duniani.

Kama vile hakuna kabila linaitwa Wahutu. Hao wote ni Wanyarwanda na lugha yao ni kinyarwanda.
 
Umesema ni kabila ambalo limetapaa miongoni mwa mikoa ya Tanzania lakini ni kabila ambalo sio miongoni mwa makabila ya Tanzania.Lakini kule kutapakaa na kuonekana hapa nchini ni tayari ni miongoni mwa makabila ya Tanzania kwa sababu wapo na wametapakaa.
 
Watusi ni moja kabila moja kubwa hapa nchini kwetu ambalo linapatikana haswa baadhi ya maeneo hapa nchini kama vile Tabora, Mpanda, Kigoma, Geita, Kagera, Karagwe, Bukoba na Kahama.

Ukifika maeneo ya Utusini katika hii mikoa, tamaduni nyingi za Kitusi zinafahamika kuanzia uvaaji, ufugaji na watu wanaofahamika. Lakini, je ni kwanini kabila hili halimo miongoni mwa makabila 120 yanayopatikana hapa nchini? Ukiangalia hili kabila ni la muda mrefu sana tangu karne ya 21 na pia kuna watemi wengi wa Kitusi .

Lakini twende mbele turudi nyuma, ni kwanini Watusi siyo miongoni mwa makabila yanayopatikana hapa nchini?

Wataalam wa historia nisaidieni.
Kesho na keshokutwa utakuja na hoja ya kabila la wachina kwanini halipatikani hapa
 
Hawa ni sehemu ya Watusi hapa Tanzania.
1.Wahangaza,wanapatikana ngara na kigoma
2.Wasumbwa, wanapatikana kahama na wameshamezwa na wasukuma.
3.Waha,waha ni mchangnyiko wa watutsi wahutu na wakongo.
4.Wanyambo,hawa wanapatikana ngara na kahama.in sehemu ya watutsi.
5.Waswahili wa ujiji, hawa nimchanganyiko wa wajiji,watutsi,wabwari,wagoma nk
5.Wamanyema,hawa walihamia kutoka Kongo wakaoana na watutsi,waha nk
Watutsi hapa Tanzania ni wengi sana ila wamechanganyika na makabila mengine ni ngumu kuwapata katika kitongoji fulani wakiwa wenyewe tu kama walivyohamia kutoka North Afrika.
Tunaendelea kufanya uchunguzi.....
 
Back
Top Bottom