Kwanini kabila la Watusi halipo miongoni ya makabila yanayopatikana nchini wakati limekuwepo kwa muda mrefu?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Watusi ni moja kabila moja kubwa hapa nchini kwetu ambalo linapatikana haswa baadhi ya maeneo hapa nchini kama vile Tabora, Mpanda, Kigoma, Geita, Kagera, Karagwe, Bukoba na Kahama.

Ukifika maeneo ya Utusini katika hii mikoa, tamaduni nyingi za Kitusi zinafahamika kuanzia uvaaji, ufugaji na watu wanaofahamika. Lakini, je ni kwanini kabila hili halimo miongoni mwa makabila 120 yanayopatikana hapa nchini? Ukiangalia hili kabila ni la muda mrefu sana tangu karne ya 21 na pia kuna watemi wengi wa Kitusi .

Lakini twende mbele turudi nyuma, ni kwanini Watusi siyo miongoni mwa makabila yanayopatikana hapa nchini?

Wataalam wa historia nisaidieni.
 
Watutsi inasemekana siyo kabila, ila ni jamii ya watu walipofika kusini mwa Afrika. Walijizolea umaarufu wa kuwa watu wema, wakaaminiwa, wakashiriki utawala na wakawa watawala.

Neno Mtutsi, wanasema linamaanisha mtu mwema. Siyo kabila. Wana kabila zao lakini walizipoteza, ndiyo maana hakuna lugha ya Kitutsi ila kuna watu wamepewa icon ya Ututsi.

Wakiwa na kabila fulani, huchukua mila hizo na hujiita wa kabila hilo. Wakiwa Kigoma ni Waha tu. Wakiwa Buhaya ni Wahaya, Uganda ni Wanankole, Usukumani watajiita Wasukuma.
 
Ukiwa ikulu unajiita mzalendo ukiwa mbwekaji unajiita mwanaharakati
 
Watutsi inasemekana siyo kabila, ila ni jamii ya watu walipofika kusini mwa Afrika. Walijizolea umaarufu wa kuwa watu wema, wakaaminiwa, wakashiriki utawala na wakawa watawala.

Neno Mtutsi, wanasema linamaanisha mtu mwema. Siyo kabila. Wana kabila zao lakini walizipoteza, ndiyo maana hakuna lugha ya Kitutsi ila kuna watu wamepewa icon ya Ututsi.

Wakiwa na kabila fulani, huchukua mila hizo na hujiita wa kabila hilo. Wakiwa Kigoma ni Waha tu. Wakiwa Buhaya ni Wahaya, Uganda ni Wanankole, Usukumani watajiita Wasukuma.
Hauko serious mkuu
 
Kiongozi kama umeshabahatika kufika tabora kuna maeneo rasmi kama vile ukienda urambo, uyogo, kalemela,tabora mjini kuna maeno yanaitwa utusini ukifika ukiulizia utusini unapelekwaaa

Hapo ndipo utawakuta watu wa kabila la watusi ila lugha inayozungumzwa sio kitusi ila wao wanasena ni watusu
MSELA WA MANZESE

Kabila lazima liwe na ardhi na lugha yake!
Na ardhi sio mtaa, minimum ni ukubwa wa kijiji.
Na ardhi iwe ancestral land.
Lugha wanayo ila nayo ni shared na Wahutu, hawana specific lugha yao exclusively!
Watutsi hawana hivyo hapa TZ!
 
Hauko serious mkuu
Mimi namuunga mkono. Hakuna kabila la watusi ila ni clan. Warwanda wataitwa watutsi, bukoba wahinda na wahima. Lugha walilirithi kadri walivyowanamigrate wakawa wana adopt mila za pale. Tofauti yao na makabila mengine,wenyewe walipigana wakatawala makabila ya kibantu. Wenyewe hata muonekano wao ni tofauti. Warefu, siyo wasemaji saana na ni watemi.
 
Watusi ni moja kabila moja kubwa hapa nchini kwetu ambalo linapatikana haswa baadhi ya maeneo hapa nchini kama vile Tabora, Mpanda, Kigoma, Geita, Kagera, Karagwe, Bukoba na Kahama.

Ukifika maeneo ya Utusini katika hii mikoa, tamaduni nyingi za Kitusi zinafahamika kuanzia uvaaji, ufugaji na watu wanaofahamika. Lakini, je ni kwanini kabila hili halimo miongoni mwa makabila 120 yanayopatikana hapa nchini? Ukiangalia hili kabila ni la muda mrefu sana tangu karne ya 21 na pia kuna watemi wengi wa Kitusi .

Lakini twende mbele turudi nyuma, ni kwanini Watusi siyo miongoni mwa makabila yanayopatikana hapa nchini?

Wataalam wa historia nisaidieni.
Kagera, Karagwe na bukoba unamaanisha nini? halafu unaposema walikuwepo tangu karne ya 21 unajua sasa tupo karne ya ngapi?
 
Back
Top Bottom