Kwanini jamii Inawachukulia tofauti wahaya

mapenzi hasara

Senior Member
Feb 28, 2020
102
275
Habari wakuu poleni na tetemeko

Kwanza nikiri waziwazi kuwa Mimi nimezaliwa na nikaambiwa kabila langu ni muhaya, japo sikijui kihaya na sijawahi kwenda bukoba japo nawasiliana na ndugu walioko huko, na ninaamini siku moja nitaenda huko kisalimia ndugu zangu wengi,

Kuna Jambo ambalo akiri yangu imekuwa na ukakasi Sana pale mapokeo ya watu pindi unapojitambulisha kuwa wewe ni muhaya ikitokea umeulizwa kabila, (binafsi sipendi kuulizwa kabila)

Watu watakutafsiri katika makundi tofauti na bila kuona aibu wanakuambia

1. Mpenda sifa
2. Kujifanya umesoma
3. Malaya
4. Kujifanya unapesa or wanakuona unapesa

Mambo haya hutokea hata kama hauna hizo sifa hata moja, unaweza ukaishi kwenye jamii vizur bila kupewa hizo sifa tajwa hapo juu Ila punde jamii inayokuzunguka wakigundua kuwa ww ni muhaya basi utapewa sifa zote hapo juu. Na chochote utakachokifanya hata Kwa Hali ya kawaida au Kwa Hali ya utani watu wataambatanisha sifa zako na kabila,

Najiuliza Kwa nini jamii inamawazo Hasi kuhusu uhaya,

Hata kwenye swala la mahusiano mwenza akigundua kuwa ww ni muhaya anaanza kuondoa Imani na kuanza story Hasi kuhusu wahaya
Kuna nini kimejificha nyuma ya hili kabila
 
Pole Sana dadaangu. Naamini waathirika wa sifa hasi ni wakina dada zaidi kutokana na baadhi yao wachache kujihusisha na biashara ya ngono miaka mingi huko nyuma na sasa. Ingawa hivi Makabila mengi yanajihusisha na biashara hiyo lakini imebaki Kama vile neno machinga kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wanaotembeza hata akiwa Msukuma.
 
Me ni mwanaume mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom