Kwa kuwa hujajua wewe ni nani, hujajua uwezo wako, hujui zaidi ya ulimwengu wa huu, hujui kwanini unaishi, hujui unataka nini, hutumii uwezo wako wa kiroho, umeacha shamba lako kuwa "shamba la bibi", kila mtu anaiba apendavyo, hufahamu ukweli wa maisha haya, huzuii wanaochukua kilicho chako, unaridhika na hali yako mbaya, hupendi kuamua, hutumii utashi wako kutenda, unatenda kama mashine isiyo na roho, huna msimamo, ukigeuzwa nyuma unageuka, ukigeuzwa mbele unageuka, huna lako, humjui mwizi mkuu na hufanyi chochote dhidi yake, unafikiri ukifanya kazi karibia kufa ndio utafanikiwa, umedanganywa, umetapeliwa, unabadilisha sahani ya ugali kwa ng'ombe mzima, "umelogwa", unazalisha kwa ajili ya wengine huku wewe ukilala njaa, unadhulimiwa bila kufahamu, wewe ni kitega uchumi cha mtu fulani, yupo mtu anafaidika na kazi zako ngumu, yupo mtu anakunywa jasho lako kama juisi kila siku, hujui na hufanyi lolote dhidi yake!