Kwanini Hii inaitwa MBUZI?

Kwanini Hii inaitwa MBUZI?

basi kama ni hivyo kuna kuparamiwa na kupara
samaki

Kuna kuparamiwa, kupara miwa na kupara samaki

Kunanyimbo moja ya msondo inasema:

Ulitaka kuolewa, utampara samaki
Samaki huyo wa tasi, utampara samaki
Ana mwiba katikati, utampara samaki
BwanJuma huyo BwanJuma, ana mliowe akwereza
Akwereza vipi? Kwarara Kwarara
Ana mliowe akwereza Akwereza
 
Kumtoa magamba samaki ni kumparapata.
 
DSCN3065.JPG

sel+de+pili+2+titr%25C3%25A9.jpg
Hivi inaitwa mbuzi au kibao cha mbuzi?
 
Kuna kuparamiwa, kupara miwa na kupara samaki

Kunanyimbo moja ya msondo inasema:

Ulitaka kuolewa, utampara samaki
Samaki huyo wa tasi, utampara samaki
Ana mwiba katikati, utampara samaki
BwanJuma huyo BwanJuma, ana mliowe akwereza
Akwereza vipi? Kwarara Kwarara
Ana mliowe akwereza Akwereza
Hao Msondo nao wana mambo... hivi tasi unampara vipi wakati hana magamba?
 
naona tumehama mada.................kwa nazi za Bakhresa itafikia wakati hicho kibao cha Mbuzi kitakua ni simulizi....kwanza tumuulize mleta hoja ni kwa nini anajiita Mbuzi Mzee
 
Hao Msondo nao wana mambo... hivi tasi unampara vipi wakati hana magamba?

Hao sio Msondo bali ni huo msondo 🙂

Utajua mwenyewe utakavyompara tasi licha ya kuwa hana magamba, si umetaka kuolewa?
 
Zamani zilitengenezwa kwa mtindo wa kuweka nafasi kwa chini kwenye vibao vyake na kuonekana kama miguu ya mnyama yaani mbuzi.yaani vibao havikuwa vya mstatili kama picha hapo juu viliachanishwa na kuonekana kama miguu ya mbele na nyuma ya mnyama mbuzi.na ndipo jina mbuzi likashika hatamu!Ila jina lililobora ni "Kibao cha kukunia Nazi"
 
Labda kuparura

Tangu ninazaliwa hadi umri huu, nimesikia tangu bibi zangu, shangazi na mama zangu wakisema "kupara samaki" na passive tense yake ikiwa "samaki wameshaparwa" kama kamusi lilivyo ainisha

Anaetumia "kupaa samaki" atalazimika kutumia "samaki amepaiwa" na si "samaki ameparurwa" maana mizizi yake hailingani

Besides, kupara (kupaa) na kuparura yana maana tofauti
 
Mi nadhani kwasababu mbuzi akiwa amegoma kwenda, anafanania na icho kibao.
 
Tangu ninazaliwa hadi umri huu, nimesikia tangu bibi zangu, shangazi na mama zangu wakisema "kupara samaki" na passive tense yake ikiwa "samaki wameshaparwa" kama kamusi lilivyo ainisha

Anaetumia "kupaa samaki" atalazimika kutumia "samaki amepaiwa" na si "samaki ameparurwa" maana mizizi yake hailingani

Besides, kupara (kupaa) na kuparura yana maana tofauti

Uko sahihi hasa, mweledi!
 
Mie nina jibu la ukweli ila kwa sharti la kwanza kwako Mbuzi mzee...ebu badilisha avatar yako iwe mbuzi ya kukuna nazi (yaani uwe mbuzi mzee cha kukuna nazi) ....Jibu lake hutakubaliana nalo
 
Mie nina jibu la ukweli ila kwa sharti la kwanza kwako Mbuzi mzee...ebu badilisha avatar yako iwe mbuzi ya kukuna nazi (yaani uwe mbuzi mzee cha kukuna nazi) ....Jibu lake hutakubaliana nalo

Mkuu "Kukuna" nazi kuna maana nyingi. Maana, nazi ukunwa halafu inatoa tuwi la maziwa ziwa, nategemea umenielewa. @ geophysics

Kwahiyo, sharti lako naligopa, ikiwa ninavyo fikiria ndivyo unavyo fikiria.
 
Back
Top Bottom