Kwanini hatutengenezi barabara za zege tunakomaa na lami?

Kwanini hatutengenezi barabara za zege tunakomaa na lami?

mkuu barabara ya zege haiwekewi nondo, sio gorofa hakuna reinforcement inayohitajika

Njoo mbagala uone mwendo kasi barabara inavyotengenezwa nindo zinawekwa sema sio ndefu wanaweka tuvipande mkuu nondo ni lazima


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
mkuu barabara ya zege haiwekewi nondo, sio gorofa hakuna reinforcement inayohitajika
Inawekwa nondo,zinawekwa za kulazwa na vitu vingine. Inasaidia zege lisipasuke ndani ya muda husika.
Screenshot_2020-03-24-20-19-28.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda shokapu zilikuwa zimeisha
Mtaalamu hakusema hivyo. Yeye alisema kuwa barabara nyingi zinajengwa kwa lami badala ya zege kwa sababu zege ina mitikisiko zaidi kuliko lami. By the way, wewe unadhani ni kwa nini wanatumia lami zaidi kuliko zege, wakati gharama za kujenga barabara kwa zege zinaweza kuwa ziko chini kidogo kuliko za barabara zilizojengwa kwa lami? Logic yake ni nini? Au wajenzi wa barabara wanapenda watumie hela nyingi zaidi kwenye miradi yao ili wafurahi?
 
Ile mitikisiko ni matokeo ya maungio ya vipande vya zege au section za maungio...... Na hiyo haiwezi kuwa shida sababu kuna namna ya kuvipoteza......

Na kwa upande wa gharama na ubora si kweli kuwa zipo sawa ni tofauti..... Upande wa matengenezo ya zege inazidi ya lami but katika gharama za kurepair ya zege haina kabisa sababu huwa haiharibiki labda itokee tetemeko la ardhi kubwa sana ambayo ni nadra.

Ila kwa upande wa zege inadumu kwa miaka mingi zaidi ni miaka 45 kwenda juu kwa lifespan lami ni 20 years na ni ngumu kuzidi hapo ikizidi basi ni kwa kudura za MUNGU.

Fanya research yako upya utaona ninachokwambia....

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu haya mambo mimi wala sijui kitu chochote, isipokuwa nilikuwa namnukuu mtaalamu ambaye niliwahi kumsikia akiongea kwenye media. Tukirudi tena sasa kwenye swali letu la msingi, je ni kwa nini basi wahandisi wanapendelea zaidi kujenga barabara kwa kutumia lami na si zege?
 
Mtaalamu hakusema hivyo. Yeye alisema kuwa barabara nyingi zinajengwa kwa lami badala ya zege kwa sababu zege ina mitikisiko zaidi kuliko lami. By the way, wewe unadhani ni kwa nini wanatumia lami zaidi kuliko zege, wakati gharama za kujenga barabara kwa zege zinaweza kuwa ziko chini kidogo kuliko za barabara zilizojengwa kwa lami? Logic yake ni nini? Au wajenzi wa barabara wanapenda watumie hela nyingi zaidi kwenye miradi yao ili wafurahi?
Sio kweli mkuu mitikidiko Ni poor workmanship, Kuna hii barabara ya mwanza musoma Ina mawimbi utafikiri unasafiri kwa jahazi
 
Sio kweli mkuu mitikidiko Ni poor workmanship, Kuna hii barabara ya mwanza musoma Ina mawimbi utafikiri unasafiri kwa jahazi
Mawimbi na mitikisiko barabarani ni vitu viwili tofauti. Mawimbi yanatokana na barabara iliyojengwa chini ya kiwango, imebonyea baada ya uzito husika kuwa umeigandamiza (pressure) wakati mitikisiko inatokana na aina ya material yaliyotumika kujenga barabara, kwenye bararabara iliyojengwa kwenye viwango vya hali ya juu, na ambayo haina kasoro yoyote katika ujenzi wake, na wala haiona mawimbi ya aina yoyote ile. Kwa hiyo mitikisiko na mawimbi vinatokana na sababu zisizofanana!
 
tuwatengenezee za kudumu afu tukale wapi?au hujui kuwa ni dili za watu hizo mkuu?
 
Pia mfano mwingine ni kwenye daraja la Nyerere la kigamboni pale baada ya sehemu ya kulipia kama upande unaotokea town kwenda kigamboni, kuna kipande cha zege mita kadhaa
Barabara ya Zege na ya Lami gharama zake karibia ziko sawa, na hata life span yake almost the same. Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu mmoja nadhani kutoka TANROADS, ambaye niliwahi kumsikia siku moja akihojiwa kwenye media. Tofauti iliyopo kati ya barabara hizi ni kwamba Zege ina mitikisiko mikubwa sana wakati lami haina mitikisiko mikubwa. Nadhani kama hivi karibuni, umewahi kuendesha gari kwenye kipande cha barabara ya kutoka Mwenge kuja Ubungo, kuanzia karibu na pale pale ambapo wanajenga interchange, au karibu na njia panda ya Chuo Kikuu, unaweza kukubaliana na mtaalamu huyo kwamba Zege ina mitikisiko zaidi kuliko lami. Kipande hicho mpaka leo kuna Zege iko pale.

Uthibitisho mwingine ni kwenye Viwanja vya ndege, angalia unapokuwa upo kwenye ndege, inapotaka kupaa au kutua, mtikisiko pamoja na kelele zilizopo. Runways zingekuwa za lami, mitikisiko na kelele wakati wa kupaa na kutua, isingekuwa mikubwa kiasi kile. Lakini sasa hamna namna kwa sababu ndege inahitaji ardhi iliyo ngumu mithili ya jiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu na wewe hapo kwenye mitikisiko umekubaliana nae? Siku moja panda mwendokasi kwa majaribio
Mtaalamu hakusema hivyo. Yeye alisema kuwa barabara nyingi zinajengwa kwa lami badala ya zege kwa sababu zege ina mitikisiko zaidi kuliko lami. By the way, wewe unadhani ni kwa nini wanatumia lami zaidi kuliko zege, wakati gharama za kujenga barabara kwa zege zinaweza kuwa ziko chini kidogo kuliko za barabara zilizojengwa kwa lami? Logic yake ni nini? Au wajenzi wa barabara wanapenda watumie hela nyingi zaidi kwenye miradi yao ili wafurahi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli mkuu mitikidiko Ni poor workmanship, Kuna hii barabara ya mwanza musoma Ina mawimbi utafikiri unasafiri kwa jahazi
[emoji28][emoji28][emoji28] na kuna kipande kimerudiwa lakini mawimbi yaliyopo bora wangeacha tu! Nitashangaa sana mamlaka ikipokea barabara inayofanana vile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu na wewe hapo kwenye mitikisiko umekubaliana nae? Siku moja panda mwendokasi kwa majaribio

Sent using Jamii Forums mobile app
Tairi za gari za mwendokasi haziwezi kuwa sawa na za gari zetu ndogo. Ubapa na ukubwa wa tairi una mchango katika kuficha mitikisiko. Ukitaka ujue vizuri zaidi, panda mwendokasi inayotembea kwenye lami, halafu ukapande tena mwendokasi inayoembea kwenye zege, hapo ndo utaweza kulinganisha vizuri. Usilinganishe kwa kuangalia gari ndogo inaytembea kwenye lami, na gari kubwa inayotembea kwenye zege. Ukifanya hivyo, kisayansi utakuwa unafanya makosa makubwa
 
Barabara za zege hazina friction au msuguano mkubwa ukilinganisha na lami.
Material inayotumika kutengeneza Matairi ya magari Inafanya Tairi ziwe na msuguano imara(traction) ikiwa kwenye lami kuliko kwenye zege.

Mfano mzuri ni parking zilizopo ghorofani mara nyingi utakuta unapopanda tairi zina slip sana hii ni kukosa msuguano imara kati ya tairi na concrete surface.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hitimisho
tungetumie ujenzi huu tungekuwa na viwanda vingi vya cement+Nondo kila mkoa =watanzania wangepata ajira ,serikali ingekusanya P.A.Y.E kwa waajiriwa,vijana wangekuwa bize.
 
Back
Top Bottom