Tanzania tuwe na barabara za lami za aina mbili.

Tanzania tuwe na barabara za lami za aina mbili.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,554
Reaction score
110,042
Ingefaa Tanzania tuwe na barabara za lami za aina mbili au madaraja mawili. Aina ya kwanza iwe na barabara za lami za kudumu na aina ya pili iwe barabara za lami za muda.

Barabara za lami za kudumu iwe ni zile zinazokaa hadi miaka 15 bila kuharibika. Barabara za lami za muda iwe ni zile zinazokaa miaka miwili tu zinaanza kuwa na mashimo na kuwekewa viraka kila mahali.

Screenshot_20261010-130253~2.jpg

Barabara nchi nzima zina hali hii, 2030 nchi haitakuwa na barabara ya lami.

Tukutane 2030.
 
Hatuna barabara za kudumu, ukiachilia mbali zilizojengwa na mkoloni.

Nimepita karibuni Arusha kwenda Singida, dereva lazima awe na PhD (Pot holes Dodger).

Barabara ikijengwa, ndani ya miaka mitano imejaa viraka na ukarabati wa kudumu.
 
Ingefaa Tanzania tuwe na barabara za lami za aina mbili au madaraja mawili. Aina ya kwanza iwe na barabara za lami za kudumu na aina ya pili iwe barabara za lami za muda.

Barabara za lami za kudumu iwe ni zile zinazokaa hadi miaka 15 bila kuharibika. Barabara za lami za muda iwe ni zile zinazokaa miaka miwili tu zinaanza kuwa na mashimo na kuwekewa viraka kila mahali.

View attachment 3687920

View attachment 3687921
Kwanini tusiwe na barabara zinazodumu tu?! Kweli unashauri tuwe na barabara zinazokaa muda mfupi halafu zinaharibika? Mnapokuwa mmelewa achaneni na mitandao
 
Back
Top Bottom