Kwanini duniani kuna watu weusi (black people) na weupe (white people) wakati asili yetu ni moja?

DonaGee

Member
Jun 2, 2019
8
41
Habari wadau. Mimi ni mwanachama mpya humu. Nina jambo ambalo limekuwa likinichanganya kwa siku nyingi. Kwa mwenye uelewa japo kidogo ninaomba kufahamishwa.

Wadau ni kwa nini duniani kuna watu weusi (black people) mostly Africans na white people? Ilikuwaje kukawa na matabaka haya ya weusi na weupe?

Kwanini wote hatukuwa kama ni weusi basi wote duniani tuwe weusi kama weupe wote tuwe weupe. Wanasayansi wanatuambia tulitokana na sokwe maana yake chimbuko letu ni moja sasa kwa nini wengine wawe weupe wengine weusi?

Kwa upande mwingine wa dini tunaambiwa sisi ni chimbuko la Adam na Hawa maana yake chimbuko letu ni moja sasa kwa nini wao ni weupe sisi weusi?

Kama ni mabadikiko ya tabia nchi (climatic change) mfano mionzi ya jua (radiation), je sisi tulikuwa weupe tukapigwa jua tukawa weusi ama? Na kama ni hivyo, je nikienda sehemu isiyo na mionzi mikali ya jua nitabadikika kuwa mweupe (mzungu)?

Na je watu weupe wakija huku Africa wakapigwa mionzi mikali ya jua watakuwa weusi kama tulivyo sisi waafrica? Na kama ni hivyo itachukua muda gani? Napata utata sana juu ya maswali haya.

Na kama chimbuko letu binadamu hapa duniani ni moja je sisi weusi tulikuwa weupe baadae kutokana na climatic change tukawa weusi au watu weupe ndio walioanza kuwa weusi kisha kutokana na climatic change wakawa weupe? Ilikuwaje ikawa hivi ilivyo Leo? Kwa mwenye mchango au uelewa wowote hapa will be highly appreciated. Asante
 
Mimi naamini ni swala la kigeografia zaidi (jua, upepo, humidity n.k) na vyakula tunavyokula. Ndiyo maana wengine tukienda mikoani kwetu tunakuwa weusi tii..tukirudi Dar tu ngozi zinakuwa light!
 
Wanadamu wote wanaoishi leo ni wa aina moja, Homo sapiens, nao wote wametoka katika ukoo mmoja. . . . Tofauti za kimaumbile kati ya wanadamu husababishwa na tofauti katika urithi na athari za mazingira juu ya urithi huo. Mara nyingi, tofauti hizo husababishwa na mambo hayo mawili. . . . Mara nyingi tofauti kati ya watu mbalimbali katika jamii moja au katika kundi moja la watu ni kubwa kuliko tofauti za wastani kati ya jamii mbalimbali au makundi ya watu.”—Baraza la kimataifa la wanasayansi lililoitishwa na UNESCO, ambalo lilinukuliwa katika kichapo.....

maelezo yote yapo kwenye link
 
Jibu ni evolution mkuu.

Google that.

Your link was much helpfulness. Kwa kiasi kikubwa imezungumzia UV environment na heredity by birth. Ila imejikita zaidi kwenye mazingira referring to exposure to sun light and that means Africa tuko exposed zaidi na sunlight. If so what makes Arabic countries eg Egypt and Morocco kuwa weupe wakati sisi huku ni weusi and we are all in africa? How did this happen?
 
Asante kwa link
 
Kwaiyo tulikuwa wazungu kwanza kisha ndio tukawa weusi kwa sababu hizo ulizotaja au wazungu ndio walianza kuwa weusi kisha evolution ikawafanya wawe weupe?
Inawezekana tulikuwa weupe, jua likatuchoma, genes zikareact ili kuendana na mazingira ndo tukawa blacks..
We unadhani kwanini watu weupe ni wengi kuliko weusi?
 
Rangi tofauti za ngozi zinategemea uwezo wa seli maalumu katika kanda la kizazi la epidemisi kutengeneza kiasi kikubwa au kidogo cha melanini.

Melanini ni kemikali inayokaa ndani ya epidemisi yenye kazi ya kuzuia au angalau kupunguza athira za mnururisho wa jua. Mnururisho huo unaweza kuwa wa hatari kama jua ni kali na kuchoma seli, hasa kusababisha kansa.
Sehemu mbalimbali za mwili zinaweza kushika viwango tofautitofauti za melanini: ngozi ya makofi kwa kawaida ina melanini kidogo tu.

Uwezo wa kutengeneza melanini unarithiwa. Hivyo watu "weusi" huzaliwa na kiwango kikubwa cha melanini ya kudumu kwenye ngozi. Watu "weupe" wana kiwango kidogo.
 
Mwili wetu unahitaji vitamini D na hapo asili ya tofauti ya rangi ya ngozi.
Maana mwili unajenga vitamini D ama kwa msaada wa vyakula maalumu au kwa msaada wa nuru ya Jua. Dawa la melanini pamoja na kukinga mwili na miale ya Jua inapungua pia kujenga kwa vitamini D.

Katika mazingira yenye jua kidogo rangi nyeupe ina faida. Rangi nyeupe inasaidia kupokea nuru nyingi hivyo inasaidia kuongeza vitamini D. Kama mtu "mweusi" anaishi katika mazingira yenye jua kidogo anaweza kupata uhaba wa vitamini hiyo.

Kinyume chake wingi wa nuru inaongeza hatari ya kushika kansa ya ngozi. Watu wa Australia waliotoka katika koo za Wazungu wa Ulaya ilhali wanaishi katika nchi ya tropiki yenye jua kali wana kiwango kikubwa cha kansa ya ngozi.

Tabia hizo zimesababisha ya kwamba mara nyingi watu katika nchi za jua kali ni "weusi" zaidi, lakini watu kwenye nchi za jua kidogo ni "weupe" zaidi, maana tofauti za rangi ya ngozi zinasababisha faida au hasara za kiafya kulingana na mazingira.

Pale ambako hali ya jua ni ya katikati watu wa kila rangi wanaweza kuishi bila matata, lakini wakizaa pamoja kwa kawaida urithi wa ngozi nyeusi zaidi hushinda juu ya urithi wa rangi nyeupe.
 
Wataalamu wa biolojia ya evolusheni huamini siku hizi kwamba watu wa kwanza waliotoka Afrika na kuenea kote duniani walikuwa weusi-weusi kiasi (shauri ya Jua kali katika Afrika). Lakini kadri walivyofika kaskazini penye Jua kidogo rangi ilikuwa hasara, kwa sababu ya matatizo ya vitamini D. Hapo watoto waliozaliwa na melanini kidogo walipata faida. Faida hii ilisababisha kuongezeka kwa watu wenye rangi "nyeupe" (yaani wenye melanini kidogo).

Ajabu ni watu wanaoishi kazkazini kabisa, karibu na ncha, wana rangi nyeusi kiasi: akina Inuit = Waeskimo. Ku a maelezo mawili 1) mababu walihamia kutoka maeneo ya Asia (kusini zaidi) si muda mrefu bado. kwa hiyo mabadiliko hayakutokea. 2) watu hao wanakula sana sana samaki, chakula chenye vitamini D nyingi (maana kilimo haiwezekani pale, wanaishi kwenye barafu ya kudumu) kwa hiyo ngozi hii si hasara katika mazingira yao.
 
Your link was much helpfulness. Kwa kiasi kikubwa imezungumzia UV environment na heredity by birth. Ila imejikita zaidi kwenye mazingira referring to exposure to sun light and that means Africa tuko exposed zaidi na sunlight. If so what makes Arabic countries eg Egypt and Morocco kuwa weupe wakati sisi huku ni weusi and we are all in africa? How did this happen?
Siri yake ni uhmiaji. Angalia bahari ya Shamu (Red Sea). Upande wa Afrika (Sudan, Eritrea) kuna watu weusi sana, Kumbe mababu wao wamekaa pal miaka mielfu mingi. Miale ya Jua imefanya kazi kwa vizazi vingi na kuondoa wale "weupe", badala yake kuongeza kiwango cha "weusi". Pia kabla ya kunea kwa Uislamu, ambayo si muda mrefu, hawakuzoea sana kutumia nguo.

Upande mwingine wa bahari (Uarabuni na Yemen) wtu si weusi sana (isipokuwa watoto wa watumwa wa zamani). Kumbe mababu yao waliingia si muda mrefu vile. Pia wanajifunika kabisa kwa kuvaa nguo nyingi. Maana waliwasiliana na mataifa ya kaskazini wenye utamaduni ya nguo (sghauri ya baridi) n tangu miaka mielfu waliweza kufanya biashara nao .

Pia wako akina Khoikhoi na San wa Afrika Kusini wasio weusi sana. Mababu yao walifika pale miaka mingi sana; wako mbali na ikweta, kuna baridi tayari na Jua limepungua. Labda hao wako karibu zaidi na "rangi ya kiasili" maana wengine katika Afrika ya kitropiki waliongeza rangi kama kinga, sawa na Wahindi wa Kusini ambao ni weusi sanaaa.
 
Your link was much helpfulness. Kwa kiasi kikubwa imezungumzia UV environment na heredity by birth. Ila imejikita zaidi kwenye mazingira referring to exposure to sun light and that means Africa tuko exposed zaidi na sunlight. If so what makes Arabic countries eg Egypt and Morocco kuwa weupe wakati sisi huku ni weusi and we are all in africa? How did this happen?
UV exposure ya watu wa kaskazini ukitoka equator ukiwa unanyemelea tropic of cancer ni pungufu ukilinganisha na watu wanaoishi karibu na equator. Vivyo hivyo kama unaenda kusini ya equator kuelekea tropic of capricorn utaona watu asilia wa maeneo haya (non-bantus) ngozi yao ni nyeupe kama njano fulani mfano Khoisan aka "bushmen" na makabila mengi asilia ya Afrika Kusini. Yale makabila asilia ya kusini ya Afrika kabla ya ujio aka migration ya Wabantu kutoka kaskazini wengi wana ngozi nyeupe (siyo kama Wazungu lakini) au njano hivi mfano Xhosa, na makabila lukuki ambayo siyo Wabantu wenye asili yao kusini mwa bara la Afrika.
 
Kwaiyo tulikuwa wazungu kwanza kisha ndio tukawa weusi kwa sababu hizo ulizotaja au wazungu ndio walianza kuwa weusi kisha evolution ikawafanya wawe weupe?
Kwaiyo = Kwahiyo. Kimsingi ni kuwa hakuna mzungu aliyekuwa mweusi wala hakuna mweusi aliyekuwa mzungu. Kulingana na sayansi mwanzo wa binadamu ni cell zilizojiunga zikaendelea kubadilika kulingana na muda na kuwa viumbe complex. Sasa kadiri muda ulivyokuwa unaenda viumbe walizidi kuwa complex na hatimae wakatokea wanadamu. Wanadamu walipotokea walisambaa sehemu mbali mbali na kila aliyesambaa alibadilika kulingana na sehemu alikokuwa anaishi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom