Kwanini Dkt. Bashiru na Makonda wamekuwa waungwana kwa kukaa kimya, lakini Harakaharaka yuko mbio sana

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Nawapongeza sana Mkonda na Dr. Bashiru kwa kuwa waungwana hasa wakinata na ile methali isemeyo mtu mzima akivuliwa nguo uchutama. Wahishimiwa hawa waungwana na watu ambao walifanya kazikubwa sana wanaweza kuwa vijana wa mfano wa kuigwa na vijana wengine kutokana na upepo ambao ulikuwa ukisuma tanga zao kukata ghafla kutokana na kuwa dunia inajizungusha na kuzunguka jua, wamekuwa na hikima na kutambua kuwa hizo ni nguvu za asili.

Hari hii imekuwa tofauti kabisa kwa ndugu yangu na jamaa yangu huyo kwani baada tu ya upepo kukata na jaazi kusimama yeye amevua shati na kuanza kupepea tanga kwa mikono yake. Tumemshuhudia akituma kripu za kucheza shoo na kujichekesha kanakwamba anabadilisha gia angani kuwa mcheza shoo na kina Dimond na wenzake.

Licha ya kuwa tayari anaitwa katika kamati mbali mbali za maadili na nidhamu kujitetea, tayari anaandaa makongamano kanakwamba upepo hajui kama ulishakata.

Huyu jamaa anaubunge wa kuteuliwa ambao ni raisi kutenguliwa, ingependeza kama na yeye angechuchumaa chini kidogo atafakari. Hata hivyo mimi kama mtoto wa mchungaji narudisha lawama zote kwa viongozi waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi kwa kumwacha kijana wao bila kunfanyia kanseli, na kibaya zaidi hata kuniita mimi mtumishani wa Mungu kwenda kumkanseli.

Kijana huyo ambaye aliwai kufanya mambo makubwa wakati upepo ulipokuwa ukivuma nadhani ifike wakati tutambue mchango wake hasa kwa kipindi hiki kigumu cha upepo kukata kwa kumfanyia tu kanseli na si kumpeleka katika vikao vya maadili na kumjadili wakati tatizo mnalijua.

Nachuku fursa hii kuwahasa vijana na wazee pia kuwa uongozi ni upepo tu au pepo zinakataga, na wakati mwingine zinakata upo katikati ya bahari na hujui kuogelea utafanyaje. Vyeo ni dhamana na pia nawahasa kuto kutuiga sisi watu wa kanisa kwani sisi tumepewa kibari na Mungu kukusanya sadaka mpaka kifo na si watu wa siasa.

Nawasilisha.
 
Makonda hata kuachia ofisi ya ukuu wa mkoa alijua perfectly what gona happen ...!! Anajua kila kitu na akaona the best option ni kukaa kimya mana ashajijenga kiuchumi Kwa kiwango cha kuridhisha
 
Nawapongeza sana Mkonda na Dr. Bashiru kwa kuwa waungwana hasa wakinata na ile methali isemeyo mtu mzima akivuliwa nguo uchutama.
Hawa siyo kwamba wamechutama, bali ni wanafiki. Wamekaa kimya mwa lengo la kumfurahisha mfalme ili awafikirie kwenye teuzi
 
Kwa kweli waliosema kiburi si maungwana walinena jambo kubwa sana leo hii Bashiru anateseka kwa aibu hadi basi.
 
Nawapongeza sana Mkonda na Dr. Bashiru kwa kuwa waungwana hasa wakinata na ile methali isemeyo mtu mzima akivuliwa nguo uchutama. Wahishimiwa hawa waungwana na watu ambao walifanya kazikubwa sana wanaweza kuwa vijana wa mfano wa kuigwa na vijana wengine kutokana na upepo ambao ulikuwa ukisuma
Hao ni wahanga wa ile kauli ya wehenga kuwa malipo ni hapahapa duniani. Na wametafakari hilo na kuona kuwa dunia ni ya Mungu.
 
Yule sio mwanasiasa bali ni mwanaharakati. Huko kwenye siasa alibakwa tu ndomaana ameamua apumue kwa nguvu sasa hivi.
 
Back
Top Bottom