Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

MTU kauliza swali tu..
Lkn cha kustaajabisha mamtu washaanza kutoa POVU..labda niwasaidie Mimi kumjibu huyo mleta mada hilo swali.
DEREVA AMEKIMBIZWA NAIROBI FASTA ILI AKAPANGILIWE STATEMENT JINSI YA KUONGEA NA KUJIBU MASWALI ATAKAYOHOJIWA NA JESHI LA POLISI...SIKU ZOTE KWENYE TUKIO AU AJALI YA BARABARANI IKITOKEA MTU WAKWANZA KUCHUKULIWA MAELEZO NI DEREVA..kama nimekosea kujibu naomba mnirekebishe..
NATAMANI NIMJIBU KUA NI MGONJWA LKN KAMA NAE NI MGONJWA ANGEONGOZANA NA MWENZAKE WKT AKISAFIRISHWA!!!!!

Sent from Calculator Phone vesion007
LIKE, LIKE,
Hivi hapa kwetu hakuna polygraphic test?
 
wewe wangapi hapa... naona unakaribia dirishani..hahahahaaa
wewe utakuwa ni huyo mwenye bakuli la rangi yenyu😀😀😀😵
mqdefault.jpg
Ama kweli wewe ni bavicha. Ndio akili yako ilipoishia hapo?
 
Kuna mengi sana nyuma ya pazia, Pure and Professional Pyschologists wapo wengi sana, ila mambo ya siasa huwa yana mengi ndani yake, yaweza kuwa usalama pia.
 
Mkuu hilo lipo wazi kabisa..walijisahau kwa huyo Dereva(Adam)lkn wangelijua tangia mwanzo nae angeambatana nao ktk hio safari..
Siku zote Mungu hua anabainisha na atazidi kubainisha.
Na hivi jamii yoote inaishutumu serikali ya awamu ya 5 ndio husika mkuu!!!!
Ona sasa opereshen inayofanyika watahakikisha hadi wakamatwe na wataje.
Kwa makusudi ZAIDI wamewaita mpaka FBI (Shirika LA Upelelezi Marekani)..kuwaomba watoe ushirikiano juu ya huu unyama uliofanywa ili tu,,iwabainishe hao wanaowashutumu

Sent from Calculator Phone vesion007
Sidhani kma itawezekani FBI kufanya kazi, kumbuka Tanzania ni nchi huru mkuu huwexi leta mtu yeyote kufanya shughuli za kiusalama bila makubaliano na serikali, kma unakumbka kule kenya kipindi aliuawa Robert Ouko, kulikuwa na scotland yard lkn ilikuja kwa makubaliano ya serikali, hivyo mtu binafsi hawezi kuwaita bila ridhaa ya serikali.
 
kwani kina mbowe hawakujua kama dereva wa lissu lazima atatakiwa kuhojiwa? je huyu dereva atawah kurudi au atarudi na mgonjwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya tukio, police walitakiwa kumchukua dereva na kumhoji as soon as possible. Dereva kaondoka almost 12 hours after bila kuhojiwa. Hiyo inaonyesha kuna mapungufu makubwa kwenye vyombo vyetu vya usalama.
 
Mie naamini kabisa dereva sio aliempiga lissu risasi,bali anaweza kusaidia kujua walianza kufuatiliwa tokea wapi,wakati anavamiwa alifanya nini kujiokoa n.k
 
Mkuu hawa watu sijui kama wanajitambua kuwa ni wajinga. Mie nafikiri wakae pembeni wawaache Chadema wafanye yao. Wameshindwa kumuua Lissu wakubali matokeo, anatibiwa na chama chake na hayo hayawahusu wao wauaji
Mimi nilikuwa bado siamini kama serikali au COM inahusika lakini kwa jitihada hizi za utetezi mitandaoni na kujifanya kila Buku7 ni mpelelezi wa jinai naanza kutoka shaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyepashwa kumuwahi Driver na kuhakikisha anahojiwa ni mbowe au wewe? Tangu muwa Tundulisu, hadi wanaondoka kwenda Nairobi ni muga gani ulipita hapo katikati?

Kama kweli mgelikuwa mnajali mngeacha Driver wa watu aokotwe na wasamalia wema waanze kushughulikia afya yake ndipo mseme mnataka kumhoji? Upumbavu!

Hamjui effects za post-traumas, kwenye interrogations? \

Mlidhani ni ngedere kama msiofahamika, kwamba mabavu tu yanaweza kuwapa taarifa sahihi na yakinifu?

Mlisema mwenye taarifa awaletee huko mliko. Utaalamu wa kuzitafuta bila shaka hamna ndioy sababu hamkuona umuhimu wa huyu baba. Au mlidhani kazi mmeimaliza?

Kingine, Mbowe na CHADEMA, UKAWA, wako maili 1000 mbele zenu. Tazama wawatangulia katika kila kitu!.

KAMA UNATAKA TAARIFA, ANZA KWANZA KUMHOJI BASHITE, KUNA TETESI ALIONEKANA GAIRO SIKU YA TUKIO LILE SAA MBILI USIKU. ALIKUWA AKITOKA NA KWENDA WAPI?




Tuliza hesabu zako vizuri, ideally, kama Mbowe hana stake kwenye hili alipaswa kuona Dereva ametoa maelezo yake ili yatoe msingi kwa upelelezi wa tukio, kwahali hii ya kutopenda kuona Dereva akitoa maelezo ni vema yale magari (Nissan ) yakaachiliwa
 
Polisi wanatafuta Dereva kumbambikia kesi tu hakuna hoja.Kama RPC anasema hakumuona Dereva siku ya tukio wakati alikuwa bwelele hospitali kwanini Hawa kumuuliza??

Suspect wa kwanza walitakiwa kuwa Polisi wanaolinda nyumba hizo mpaka Leo haqajaguswa unaenda kumtafuta dereva.

Hivi huyu dereva aliweza.kuwa interviewed na waandishi wa habari siku ya tukio askari walikuwa wapi??

Hakuna Mtanzania asiyejua namna Polisi wetu wanavyofanya kazi,Dereva hakutakiwa kuwa suspect Bali ushahidi number moja.

Anataka awe Suspect ili mumfungulie kesi ya Mauaji.muacha wauaji.Hili limekula kwa CCM na Serikali yake mmezoea kuua,kutesa na kuteka.

Mawili anataka kutekwa,kuteswa au kuua wa maana hawajui anajua hao watu kwa kiasi gani.

Ni bora kama wameshindwa Polisi waseme wameshindwa.Uuaji na ubambikiaji RAIA kesi unajulikana sana.

Mbowe yuko sahihi kabisa ni rahisi sana kumbambikia kesi kijana wa watu na kumuweka mahabusu kosa usalama wake.

RPC alipoulizwa siku ya tukio alisema hajafika kwenye tukio sababu alikuwa na mikutano,hivi jambo kubwa hivyo bado kiongozi unasuboroa chai na sambusa badala ya kwenda kupona tukio??

Hatuna polisi kwa sasa tuna matawi ya CCM. Naona ndiyo sababu mmemteua Jaji Mkuu anataka kesi ya Lissu isakiziwe kijana wa watu.

Miaka 55 ya Chama Cha Mauaji Tanzania bado masikini wa kutupwa mnachojua ni kujilimbikizia Mali tu
Hoja yako ina mashiko sana na pointi zimejipanga vzri ila unakosea pale unapoimalizia kwa milengo ya kisiasa...anyway hata mtoto mdgo atajiuliza, mtu wa kwanza kuhojiwa siku ya tukio na within the first 15 minutes alikuwa ni huyu dreva, hizi story ambzo polisi inakuja nazo kwa sasa ni uzembe kazini, mi nashauri polisi waliokuwa kwenye tukio pia wachunguzwe kwa huu uzembe. Dreva alikuwepo muda wte hadi hospitalini picha zipo amebeba nguo za Lissu, wanakujaje saa hizi kutwambia kuws hawakumhoji, hadi Lissu anapelekwa Nairobi walikuwa kumbe hawajaanza kazi ya kuwatafuta wahalifu.
 
Eneo analoishi lissu wanaishi mawaziri na kuna ulinzi. Hiyo gari isiyojulikana iliwezaje kupita getini? Hakuna kitabu kinachoorodhesha magari yanayoingia na kutoka? Tuanze na walinzi wa eneo husika
Ilitakiwa waanze na walinzi wa eneo husika wao wanamsaka dereva eti,, kweli bongo maigizo hayaishi
 
Mheshimiwa Mbowe anasema eti dereva ameenda Nairobi kwa ajili ya kuwekwa sawa kisaikolojia. Kwa nini asingeojiwa kwanza ndio akaenda huko Nairobi. Kulikuwa kuna uharaka gani wakati yeye alikuwa mzima kabisa? Je hao wanasaikolojia hapa hawapo mpaka Nairobi? Au kwa usalama wake nae kama Lissu? Najaribu kuwaza tu wadau.

​


Sent using Jamii Forums mobile app

Dereva wa nini mlitaka kumuua Mungu akamsaidia, mnataka kummalizia?
 
Tuliza hesabu zako vizuri, ideally, kama Mbowe hana stake kwenye hili alipaswa kuona Dereva ametoa maelezo yake ili yatoe msingi kwa upelelezi wa tukio, kwahali hii ya kutopenda kuona Dereva akitoa maelezo ni vema yale magari (Nissan ) yakaachiliwa
Mbowe ni ofisa upelelezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom