Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

Polisi wanatafuta Dereva kumbambikia kesi tu hakuna hoja.Kama RPC anasema hakumuona Dereva siku ya tukio wakati alikuwa bwelele hospitali kwanini Hawa kumuuliza??

Suspect wa kwanza walitakiwa kuwa Polisi wanaolinda nyumba hizo mpaka Leo haqajaguswa unaenda kumtafuta dereva.

Hivi huyu dereva aliweza.kuwa interviewed na waandishi wa habari siku ya tukio askari walikuwa wapi??

Hakuna Mtanzania asiyejua namna Polisi wetu wanavyofanya kazi,Dereva hakutakiwa kuwa suspect Bali ushahidi number moja.

Anataka awe Suspect ili mumfungulie kesi ya Mauaji.muacha wauaji.Hili limekula kwa CCM na Serikali yake mmezoea kuua,kutesa na kuteka.

Mawili anataka kutekwa,kuteswa au kuua wa maana hawajui anajua hao watu kwa kiasi gani.

Ni bora kama wameshindwa Polisi waseme wameshindwa.Uuaji na ubambikiaji RAIA kesi unajulikana sana.

Mbowe yuko sahihi kabisa ni rahisi sana kumbambikia kesi kijana wa watu na kumuweka mahabusu kosa usalama wake.

RPC alipoulizwa siku ya tukio alisema hajafika kwenye tukio sababu alikuwa na mikutano,hivi jambo kubwa hivyo bado kiongozi unasuboroa chai na sambusa badala ya kwenda kupona tukio??

Hatuna polisi kwa sasa tuna matawi ya CCM. Naona ndiyo sababu mmemteua Jaji Mkuu anataka kesi ya Lissu isakiziwe kijana wa watu.

Miaka 55 ya Chama Cha Mauaji Tanzania bado masikini wa kutupwa mnachojua ni kujilimbikizia Mali tu
 
Kwan polis wamekosa nauli ya kwenda kumhoji au mpaka awekwe sero ndo mahojiano yanakamilika ?
 
mtu anakaa kabisa anatujaza ujinga eti dereva ameenda kuwekwa sawa kisaikolojia. kwanini asiwekwe sawa kisaikolojia mkewe tundu. dereva na mkewe tundu nani ameathirika zaidi? fools carry themselves. watu wa ndio mzee. mambo ya kitoto kabisa mnaleta


Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa wa kulaumiwa ni nani?! Dereva au police ?! Dereva amekuepo kwenye tukio na wameshambuliwa wote, dereva ndiye aliyemsaidia Lisu asiuawe , dereva amekuepo hospital Dom , Dereva amehojiwa pale na wahandishi wa habari na police sasa wakiwepo lakini kazi yao sasa ilikuwa ni kudhibiti watu hospital. Kuanzia pale police walitakiwa watoe maelekezo kwa huyo shahidi namba moja lakini wamengoja mpaka siku ya tatu ndiyo waseme hajaripoti kituoni na wanamtafuta ?! Na watu wenyewe wanawindwa kwa nini asihofu maisha ?! Police wanajuwa wajibu wao namna gani wapeleleze hii kesi lakini wasiingie mkenge wa ki siasa na vitisho !!. Waonyeshe ueledi wao wasisubiri maelekezo toka sehemu.

Swala la Lisu alishalalamika kufuatiliwa kitambo lakini hakuna aliyejali!!! Walidhani ni siasa!! Sasa leo yametokea na upelelezi ndio huo wa kumtafuta dereva siku ya tatu baada ya tukio

Cairo's
 
IMG-20170911-WA0000.jpg
 
Mhhhh...Hii wanaiita "synchronization"...lazima story ya Lissu na Dereva waziweke ziendane sawa...aisee...kuna uwalakini hapa...am smelling a rat!

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa taarifa yako maelezo ya kupanga huwa yanaonekana pindi ukienda mahakamani. Huo mchezo wa kipuuzi huwa unafanywa sana na mashahidi wa serekali/ccm. Ndio maana huishia kuwa vituko mahakamani. Asikudanganye mtu, ushahidi wa kupanga huwa ni vichekesho tu.

Kwa ujumla hakuna upelelezi polisi wanaofanya kwani wangekuwa na nia hiyo wangeanza siku ileile.
 
alaf kama ni maswala y saikolojia, kwa nini asingefanyiwa hapa hapa tu. kwa nini waondoke na mtuhumiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wanaenda ulaya kutibiwa saikolojia sembuse Nairobi?
Kwanini umpangie mtu sehemu ya kutibiwa?
Yule dereva unafahamu kuwa ni mtoto wa dada ake lissu? Imagine uwe wewe unamuona mjomba ako anamiminiwa risasi najua haja zote zingekutoka hapo na kwa mshtuko ungewezz hata poteza fahamu.
Last, najua wengi mi ma layman humu someni kitu kinaitwa post traumatic psychosis! Huu ni ugonjwa wa saikolojia anaweza pata mtu alieshuhudia ajali au aliepata ajali so ni kawaida na madaktari wake specifically ni wachache sana Tanzania hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtu anakaa kabisa anatujaza ujinga eti dereva ameenda kuwekwa sawa kisaikolojia. kwanini asiwekwe sawa kisaikolojia mkewe tundu. dereva na mkewe tundu nani ameathirika zaidi? fools carry themselves. watu wa ndio mzee. mambo ya kitoto kabisa mnaleta


Sent using Jamii Forums mobile app

..wote wameathirika.

..lakini.uwezekano mkubwa dereva ameathirika zaidi kwasababu alikuwepo eneo la tukio.

..lakini pia cdm inaelekea cdm hawaamini kama polisi watafanya uchunguzi wa kina na kutenda haki.

..nadhani hiyo ndiyo imesababisha dereva wa Lissu kupelekwa Nairobi.
 
kitendo cha dereva kutokuwepo kinawapa shida sana na msongo wa mawazo watu waliyo husuka maana hawajuwi kama walionekana au la kwa vyovyote vile kama watu hawakuchanganyikiwa na maajabu ya mungu kutenda miujiza kwa lisu kupona bila shaka wangemdaka mda ule ule kila mtu aombe mungu wake tunacho kipanda kitakuja geuka moto kwetu akina lisu wakiisha wata wageukia nyie mnaojuwa wahalifu ni kina nani mkawaficha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo analoishi lissu wanaishi mawaziri na kuna ulinzi. Hiyo gari isiyojulikana iliwezaje kupita getini? Hakuna kitabu kinachoorodhesha magari yanayoingia na kutoka? Tuanze na walinzi wa eneo husika
 
Back
Top Bottom