Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

MTU kauliza swali tu..
Lkn cha kustaajabisha mamtu washaanza kutoa POVU..labda niwasaidie Mimi kumjibu huyo mleta mada hilo swali.
DEREVA AMEKIMBIZWA NAIROBI FASTA ILI AKAPANGILIWE STATEMENT JINSI YA KUONGEA NA KUJIBU MASWALI ATAKAYOHOJIWA NA JESHI LA POLISI...SIKU ZOTE KWENYE TUKIO AU AJALI YA BARABARANI IKITOKEA MTU WAKWANZA KUCHUKULIWA MAELEZO NI DEREVA..kama nimekosea kujibu naomba mnirekebishe..
NATAMANI NIMJIBU KUA NI MGONJWA LKN KAMA NAE NI MGONJWA ANGEONGOZANA NA MWENZAKE WKT AKISAFIRISHWA!!!!!

Sent from Calculator Phone vesion007
Hii si ajali ya barabarani, hapa hakuna kutumia sheria za usalama barabarani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo Mbowe kapotea stepu, kama wanavyosema watoto wa mujini.
HUYU DEREVA HAMUMPATI KABSAAA!! Subirini atakuja akiwa pamoja na KAMANDA LISSU afu tuone mtakavyochonga kutaka kumbebesha zigo lenu la mauaji ya wapigania uhuru wa NNJI HII
 
Mheshimiwa Mbowe anasema eti dereva ameenda Nairobi kwa ajili ya kuwekwa sawa kisaikolojia. Kwa nini asingeojiwa kwanza ndio akaenda huko Nairobi. Kulikuwa kuna uharaka gani wakati yeye alikuwa mzima kabisa? Je hao wanasaikolojia hapa hawapo mpaka Nairobi? Au kwa usalama wake nae kama Lissu? Najaribu kuwaza tu wadau.

​


Sent using Jamii Forums mobile app


Sentensi yoyote inayoanzia na 'ETI' inaonyesha uongo.Ulitaka huyo dereva akimbizwe central Police?/ALiyetoa taarifa ni nani??Huyu Dereva ndiye aliyemfikisha Lissu hospital hata kwenye picha anaonekana alikuwa hospitali walishindwa kumuhoji??

Anyway mwenyewe alitamka hawezi kusema chochote sababu hayuko sawa kiakili na kimwili,poleni wanachama wa Chama Cha Mauaji.Miaka 55 mnajua kuua na kutesa watu tu
 
Dereva alikuwepo eneo la tukio hadi hospitalini for the whole day,kwanini polisi hawakumchukua siku hiyo na kwenda kumhoji?
 
ngoja tumuhamishie Chato basi ili ufurahi.

bunge la tanzania ni "rubber stamp" ya serikali ya magufuli
 
Magonjwa Mtambuka,
Kama jina lako eqwe ni Mgonjwa wa akili na ndo maana watu husema heri Mungu akunyime utajiri lakini asikunyime akili au hikma...!!! Serikali na Jeshi la Polisi ndo aliopotea stepu au wameingia choo cha kike........!!! Kama una busara ulitakiwa ujiulize kwanini Dreva wa TL hakukamatwa on day 1 baada ya tukio?????Kwa taarifa yako ni kwamba baada ya kushindwa kumwua Tundu Lisu na huyo Dreva kuponea chupuchupu inaonekana WAUAJI HAWA wanamtaka dreva kwa udi na uvumba na hasa baada ya Tundu Lissu kuzinduka jijini Nairobi na kusema ALIWATAMBUA WALIOTAKA KUMWUA. Kwa maneno hayo ya TL ina maana hata Dreva aliwaona hawa wauaji. Kinachotafutwa hapa kwa sasa ni kuhakikisha huyu aliyewaona, kuwatambua na kuwajua hawa watu'' WASIOJULIKANA''wanamnyamazisha haraka kabla hajaweka mambo hadharani........!!!!

Freeman Mbowe kama Mwenyekiti wa Chama(T) na Kiongozi wa KUB ana haki zote za kuhakikisha TL na Dreva wake hawaingii kwenye mikono ya WAUAJI a.k.a WASIOJULIKANA. CHADEMA ina haki zote za kuhakikisha watu hawa 2 waliokuwa wamelengwa kuuawa wanakuwa kwenye mikono salama mpaka siku ya siku mambo yatakapowekwa hadharani!!Kwa hiyo wewe pamoja na hao wenzako WASIOJULIKANA vuta subira!! Muhimu sasa ni kuokoa maisha ya TL lakini pia kuhakikisha huyu Dreva hadhuriki kwa namna yoyote ile...!!!
Akili hizi za kibavicha unazijua mwenyewe.
 
Hawakuwa na nia ya kumhoji kwa sababu walijua amekufa. Alikaa toka saa 7 mchana mpaka saa 6 usiku hakuna aliyetaka kumhoji. Waliamua kumpeleka Nairobi kwa usalama wake maana washambuliaji walitaka amalizwe kabla ya maelezo yake kutolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini ile premio mmeblock access za kupata usajili wake?
 
Hawakuwa na nia ya kumhoji kwa sababu walijua amekufa. Alikaa toka saa 7 mchana mpaka saa 6 usiku hakuna aliyetaka kumhoji. Waliamua kumpeleka Nairobi kwa usalama wake maana washambuliaji walitaka amalizwe kabla ya maelezo yake kutolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi sana maana mtu kapiga mpaka picha inamaana hawakuliona hilo hao polisi itakuwa tayari wameshapewa maelezo kutoka juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kuna watu wana moyo wa kusema wanachokisema. Serikali kwa hilo lililotokea hamtoki sema tu vile hatuna pakusemea lkn serikali watuua. Na dhambi hii haitamuacha MTU kabisa.
 
Washambuliaji wamemtafuta dereva kwa siku 3 ili wammalize, baada ya kumkosa, ndiyo wanatangaza kuwa wanamhitaji!

Dereva alikuwa hospitali ya Dodoma toka saa 7 mchana mpaka saa 6 usiku, hakuna mpelelezi aliyetaka hata kusikia lolote toka kwa dereva. Siku ya 3, wanasema wanamhitaji. Huu ni usanii hasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila shaka wewe ama ni mmoja wa watu wasiojulikana AU halmashauri yako haina mikutano.

Vuta subira wenye uwezo wa kuelewesha vichwa vigumu kuelewa na vyepesi kusahau waje kukusaidia.
Tuliza hesabu zako vizuri, ideally, kama Mbowe hana stake kwenye hili alipaswa kuona Dereva ametoa maelezo yake ili yatoe msingi kwa upelelezi wa tukio, kwahali hii ya kutopenda kuona Dereva akitoa maelezo ni vema yale magari (Nissan ) yakaachiliwa
 
Back
Top Bottom