Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

Kwanini Dereva wa Lissu akimbizwe Nairobi?

Kuna vitu watanzania tunajitia ujuzi, ila kiuhalisia tunakuwa hatuna ujuzi wala hatujawahi kukutana navyo. Mtu kanusurika kifo, tena kwa risasi halafu unaongea kirahisi rahisi tuu.

Kama umewahi kuvamiwa japo na majambazi nyumbani kwako unaweza ukapata picha halisi anayopitia huyo Dereva ndani ya hizi siku mbili tatu.

Naamini Siku ikifika kiu ya kutaka kuujua ukweli itakwisha maana kila muhusika atatoa maelezo yake kwa jinsi polisi watakavyoona inafaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli watanzania sijui tumelogwa na nani????? Gali lile limeripotiwa mara nyingi kwa kuwafuatilia baadhi ya viongozi na inasemekana watu wale wale na idadi ile ile waliomtolea mheshimiwa Nape bastora alafu hapa mnamuongelea dereva badala ya kuuliza kama watu na lile gali wameshahojiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa Mbowe anasema eti dereva ameenda Nairobi kwa ajili ya kuwekwa sawa kisaikolojia. Kwa nini asingeojiwa kwanza ndio akaenda huko Nairobi. Kulikuwa kuna uharaka gani wakati yeye alikuwa mzima kabisa? Je hao wanasaikolojia hapa hawapo mpaka Nairobi? Au kwa usalama wake nae kama Lissu? Najaribu kuwaza tu wadau.

​


Sent using Jamii Forums mobile app



Wewe inakuhusu nini na kama unawaza sio lazima utujazie thread zako za kiushuzi Wa Lumumba
 
Mheshimiwa Mbowe anasema eti dereva ameenda Nairobi kwa ajili ya kuwekwa sawa kisaikolojia. Kwa nini asingeojiwa kwanza ndio akaenda huko Nairobi. Kulikuwa kuna uharaka gani wakati yeye alikuwa mzima kabisa? Je hao wanasaikolojia hapa hawapo mpaka Nairobi? Au kwa usalama wake nae kama Lissu? Najaribu kuwaza tu wadau.

​


Sent using Jamii Forums mobile app

Nahisi kwa usalama wake. Ikumbukwe kuwa yeye ndiye aliyemshauri mheshimiwa kutoteremka na inawezekana hata alivyolala yeye mdiye alimshauri. Pengine leo tungekuwa tunasema mengine. Waliohusika na hii operesheni watakuwa wamechukia sana, hivyo dereva yuko hatarini sana sana. Hatujui ni nani anahusika zaidi ya viashiria ambavyo wote tunapoint in one direction. Kama hiyo direction ni kweli anaweza kuuliwa ili kupoteza ushahidi.
 
Hivi wauaji wa Chacha Wangwe serkali yenye dhamana ya ulinzi wa raia ilishindwa kuwapata wauaji? Mbona hapa jamvini baadhi ya wachangiaji wanaonekana kuwajua vyema. Si hao ndio wangeisaidia polisi ili haki itendeke? Au vyombo vya Dola viliamua kupotezea? Na hapo iitakuwa sahihi wakati damu ya mtu imemwagika?
Halo Kijana acha uchochezi!naomba tuonane kesho Ijumaa pale central kwa mahojiano.
 
Haya wote mlio-like comment yangu inaonekana mnawajua watu wasiojulikana sasa naomba wote kesho ijumaa tukutane central kwa mahojiano zaidi hasa uyu kijana anaitwa Mshana Jr,anaonekana atakua msaada kwenye kipengele cha tunguli.Natania jamani.
 
Kwenye hii move Mbowe ndo engeneer na organizer wa kila kitu. Alijua kabisa kuwa dreva ndo atakuwa mhojiwa wa kwanza, yeye akamtorosha kwenda Nairobi, eti kwenda kutibiwa kisaikolojia. Alijua mpango wake wa kumchachawangwe lissu utafichuka. Cha ajabu eti wafuasi wa chadema wanajifanya kama hamnazo, hawaelewi. Yatafumuka tu mtayaelewa.
 
Back
Top Bottom