[HASHTAG]#Wakati[/HASHTAG] Lisu anapelekwa Nairobi walitajwa watu wanne tu ndio waliopanda ndege iliyokuwa imembeba Mgonjwa. Alipanda Mbowe, akapanda Mke wa Lisu na akapanda mchungaji msigwa na Mwisho alikuwepo Dr Toka timu iliyomhudumia mwanzo pale Dodoma Hospital.
[HASHTAG]#Wakati[/HASHTAG] kamanda wa polisi anatoa maeelezo kwa mara ya kwanza kuhusiana na shambulio la Lisu alisema Dereva wa Lisu yupo Daresalam na ameona habari zake kwenye magazeti ya Mtanzania na Tanzania Daima.
[HASHTAG]#Hakuna[/HASHTAG] hata siku Moja chadema ilisema Dereva yule yupo Nairobi baada ya Kutakiwa kuripoti Polisi tu baada ya Masaa 12 inatoka Taarifa kuwa na yeye alipelekwa Nairobi. Ameenda kupatiwa matibabu ya Kisaikolojia.
[HASHTAG]#Kwa[/HASHTAG] Mlolongo Huo inaonyesha Dhahiri kuwa Dereva huyu kapelekwa Nairobi baada ya kusikia anahitajika Polisi. Cha Kushangaza ni kwa nn hawataki tena kutoa Ushirikiano kwa Polis.... huku nairobi kaitwa kwenda kuivishwa nini cha Kusema. Tukumbuke Mbowe naye yupo Nairobi.....
[HASHTAG]#Kwa[/HASHTAG] Nini Mbowe harejei Nchini kama kiongozi mkuu wa chadema huku akituma watu wengine Nairobi kwenda kumshughulikia Lisu wakati yeye akiwa anashughulikia Maswala ya kiucnguzi na Team yake? Kwa nini na yeye anajichimbia Nairobi? Katibu mkuu wa Chadema kwa kuwa yeye ni Dr alitosha kuwa na team Ndogo na kwenda kushughulika na Mgonjwa kule Nairobi huku Mbowe na Dereva wakiwa Tanzania na Team Ndogo wakipush uchunguzi kwa Kushirikiana na Polisi?
[HASHTAG]#Nafikiri[/HASHTAG] wanapaswa kushiriki uchunguzi huu kwa Asilimia 100 huku wakilazimisha pia assumptions za waliompiga lisu Risasi zitumike kupata pia majibu. Hata wao wanaweza kwenda TRA kwa kubali cha polis kwenda Kujua mmiliki wa gari wanayoilalamikia kumfuatilia Lisu kwa muda mrefu ni nani.
[HASHTAG]#Mbowe[/HASHTAG] kitaalamu baada ya kumfikisha Lisu Nairobi angepaswa arudi ila hataki Kurudi anaogopa Lisu Atasema nn? Namuona anazurura na skafu hapo Nairobi na Kuongea na vyombo vya Habari tu ila huyu alipaswa awepo nchini Kupush uchunguzi.
[HASHTAG]#Kitendo[/HASHTAG] cha Yeye kungangania kukaa na Waathirika wote wawili Nairobi kinatia shaka Kubwa sana..
[HASHTAG]#Huyu[/HASHTAG] ni mtu wa pili Muhimu kwenye kambi yake Lisu anapatwa na mabalaa. Niliwahi kuwaambia Ben Saanane alikuwa ni kijana aliyekuwa akiandaa vuguvugu la Kuhakikisha Lisu anakuwa Mwenyekiti wa Chama. Alipopotea Kubenea ambaye ni mshiriki mkuu Wa Mbowe alijitokez na kusema Ben hajapotea na hata kwenye mwanahalisi aliandika kwa nini tunashindwa kuungsnisha haya matukio? Je hatuna Akili?
[HASHTAG]#Kwa[/HASHTAG] mara ya kwanza walalamikaji wanawakimbia Polis. Katika Kesi zote walalamikaji ndio watu ambao hufanya kazi na Polisi kwa asilimia Mia moja Katika kesi hii Upande wa Lisu ni wa walalamikaji matokeo yake wanawakimbia polisi.
#Ni sawa na Jambazi avamie Nyimbani kwenu mlinzi wa Nyumbani akiyewaona akatae kwenda polisi au aipige chenga polisi......
Ole Mushi