Kwanini demokrasia ya watu ‘ya mchakato mzima’ ya China inafanya kazi?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111370967754.jpg

Ni jambo lisilopingika kwamba demokrasia ni thamani inayotafutwa na binadamu wote bila kujali tofauti za tamaduni na mipaka ya nchi, na haiwezi kukiukwa.

Lakini kwa sababu za kihistoria, haki ya kutafsiri na kueleza demokrasia imekuwa mikononi mwa nchi za magharibi, ambazo zinaona kuwa ni haki yao kuweka kigezo cha demokrasia, na sehemu nyingine duniani lazima zikikubali na kukifuata.

Kwa muda mrefu, Marekani imekuwa ikijiona kuwa mlinzi wa demokrasia duniani, ikifanya kazi kama "mwendesha mashitaka" na "hakimu" wa demokrasia, na kuamua ni nchi gani ni ya kidemokrasia na nchi gani si ya kidemokrasia.

Mwaka jana, Marekani ilifanya kile kilichoitwa "mkutano wa kilele wa demokrasia" chini ya mwavuli wa "demokrasia", lakini iliziondoa karibu nusu ya nchi zote duniani. Nia na madhumuni ya mkutano huo ni dhahiri, na kwamba Marekani haikuficha msingi wa itikadi na kuendeleza maslahi yake ya jiografia za kisiasa.

"Democracy" ni neno linalotokana na lugha ya Kigiriki, ambapo "demos" inamaanisha mtu na "kratos" ni madaraka, hivyo demokrasia inaweza kutafsiriwa kama "madaraka ya watu". Katika lugha ya Kichina, neno "democracy" ni "Min Zhu", ambayo maana yake ni wananchi ni mabwana wa nchi.

Kwenye uchaguzi mkuu unaowakilisha zaidi demokrasia ya kimagharibi, migogoro kati ya vyama tofauti huwa ni vigumu kuondolewa. Wanasiasa wanaweza kutumia utaifa, ubaguzi wa rangi au msimamo mkali wa kidini kujipatia kura na kuleta mpasuko kwenye jamii.

Machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2020 ndio mfano dhahiri wa jinsi demokrasia ya aina hiyo inavyoisambaratisha jamii. Wakati huo huo, demokrasia ya kimagharibi mara nyingi ni mchezo wa matajiri na wenye nguvu.

Sauti za watu wa kawaida ambao ndio idadi kubwa zaidi katika jamii, haziwezi kusikilizwa, sembuse kulinda maslahi yao kupitia kuchagua wawakilishi wao. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, hayati Kofi Annan aliwahi kusema: "Demokrasia inahusisha zaidi uchaguzi.

Tunapojaribu kutathmini kiwango cha demokrasia ya nchi moja, inaleta maana zaidi kwa kuzingatia matakwa ya watu badala ya mfumo au mwundo wa kupigia kura." Kwa hivyo, demokrasia haipaswi kuonekana kwa sura tu, au wakati wa uchaguzi, demokrasia inapaswa kuwa mchakato mzima wenye ushiriki mpana na endelevu wa wananchi, kwa lengo la kuleta maisha bora kwa watu wote.

Mnamo mwaka 2019, Rais Xi Jinping wa China alipokagua mji wa Shanghai, alitaja kwa mara ya kwanza kwamba "demokrasia ya watu ni demokrasia ya mchakato mzima". Hali halisi ni kuwa "demokrasia ya watu ya mchakato mzima" kwa muda mrefu imekuwa na mizizi katika dhana ya utawala wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC unaozingatia watu, na watu ndio wakuu wa nchi, ambayo ni kiini na msingi wa demokrasia ya China.

Mwaka jana, Xi Jinping alisema katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC kuwa "Katika safari ndefu mpya, tunapaswa kuwategemea watu kwa karibu kuunda historia na kushikilia dhamira kuu ya Chama ya kuwatumikia wananchi kwa moyo wote. ... Kuendeleza demokrasia ya watu ya mchakato mzima, kulinda usawa na haki kwenye jamii na kujitahidi kutatua matatizo ya maendeleo yasiyo na uwiano na yale yanayowatia wasiwasi watu."

"Demokrasia ya watu ya mchakato mzima" inawawezesha watu wa China kushiriki kwa mapana na marefu katika shughuli za kisiasa za kila siku kutoka uchaguzi, mashauriano ya kisiasa, kufanya maamuzi na usimamizi, na inaweza kufikia kwa ufanisi kila raia wa China yenye watu wengi zaidi duniani.

Tofauti na demokrasia za magharibi, ambazo zina sifa ya majadiliano ya muda mrefu kati ya makundi tofauti ya kisiasa ili kufikia lengo binafsi, "demokrasia ya watu ya mchakato mzima" ya China inaangalia kujenga maelewano.

Inajumuisha mifano miwili ya demokrasia - demokrasia ya uchaguzi na demokrasia ya mashauriano, kitu ambacho kimeonyeshwa ipasavyo katika “Mikutano Miwili” ya China inayofanyika mwezi Machi kila mwaka, ambapo washiriki kutoka nyanja mbalimbali, ambao si tu wanatoka makundi ya watu mashuhuri, bali hata mkandaji wa miguu anaweza kuwa mjumbe wa bunge la umma la China ambalo ni chombo cha ngazi ya juu cha kutunga sheria, hivyo ina uwakilishi mpana zaidi.

Wachina husema kwamba “kama viatu vinafaa au la, anayejua ni mvaaji”. Waswahili pia wanasema kila chombo kwa wimbile. Duniani hakuna mtindo wa demokrasia unaokamilika.

Kinachoitwa "kila mtu ana kura moja" ni aina moja tu ya demokrasia, si mtindo pekee wa demokrasia. Badala ya kuiga mfano wa demokrasia ya Magharibi, China imeunda mtindo wake wa demokrasia, ambayo inafikia watu bilioni 1.4 kutoka makabila yote 56, na kuwezesha ushiriki mpana na endelevu wa watu wote.

Huu ni mchango mkubwa wa China katika fikra na suluhu kwa maendeleo ya siasa ya binadamu.
 
"demokrasia ya watu ni demokrasia ya mchakato mzima". Hali halisi ni kuwa "demokrasia ya watu ya mchakato mzima" kwa muda mrefu imekuwa na mizizi katika dhana ya utawala wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC unaozingatia watu, na watu ndio wakuu wa nchi, ambayo ni kiini na msingi wa demokrasia ya China.
 
China hakuna demokrasia, kuna udikteta wa Chama. Chama cha CCP kimehodhi mfumo mzima wa utawala wa nchi.
 
Chama cha CCP
Msomi anapo andika “CCP” badala ya “CPC” napataka shaka juu ya uelewa wake wa Mambo ya siasa za kimataifa, huyo mtu hana tofauti na mtu anaye andika “Chadomo” badala ya “Chadema”.

Hakuna chama cha siasa China kinacho itwa CCP bali kuna chama cha Communist Party Of China[CPC].

: Jielimishe siku nyingine usirudie haya makosa mara kwa mara.
 
China hakuna demokrasia, kuna udikteta wa Chama. Chama cha CCP kimehodhi mfumo mzima wa utawala wa nchi.
Halafu kingine kwa msaada wako mkuu jielimishe dhima nzima ya demokrasia nini chimbuko lake, sababu yake mpaka ikatokea, kwa nini demokrasia ina husishwa na maamuzi ya watu.

Kitu kilicho andikwa na Idleo kuhusu China ni rahisi sana kueleweka kwa msomi ila kwa mjinga ni ngumu sana kueleweka.

Usiwe kama mashabiki wa Simba na Yanga ambao kitu pekee wanacho jua wao ni Simba kumkosoa Yanga na yanga kumkosoa Simba na sio Simba kujifunza mambo ya faida kutoka yanga na yanga kujifunza Mambo ya faida kutoka simba.

Xi Jinping ni mkomunisti lakini miongoni mwa vitabu ambavyo ana soma mara kwa mara na vingine ambavyo amekwisha kusoma ni vinavyo husu ubepari naamini kwako hili jambo lisinge wezekana:-
i, Capitalism and freedom
ii, Capital in the twenty- first century.

: Kuna mwana falsafa mmoja wa kirumi ana sema ” Learning never exhaust the mind ” ishi na falsafa hii itakusaidia sana na kukujengea future nzuri kwenye mambo mbalimbali tofauti na sasa unavyo tafasiri mambo mbalimbali.
 
CCP ni kifupisho kilochozoelezaka zaidi nje ya China, CPC inatumika na wenye chama chao zaidi, hii ni petty issue.
Msomi anapo andika “CCP” badala ya “CPC” napataka shaka juu ya uelewa wake wa Mambo ya siasa za kimataifa, huyo mtu hana tofauti na mtu anaye andika “Chadomo” badala ya “Chadema”.

Hakuna chama cha siasa China kinacho itwa CCP bali kuna chama cha Communist Party Of China[CPC].

: Jielimishe siku nyingine usirudie haya makosa mara kwa mara.
 
China hakuna demokrasia, kuna udikteta wa Chama. Chama cha CCP kimehodhi mfumo mzima wa utawala wa nchi.
Mwisho kwa faida yako na ya wasomaji wote, kasome kuhusu haya:-
i, Min Zhu
ii, Democratic Centralism
iii,Consultative Democracy
 
CCP ni kifupisho kilochozoelezaka zaidi nje ya China, CPC inatumika na wenye chama chao zaidi, hii ni petty issue.
Hili ni kosa la pili tena una rudia hakuna kitu kinachoitwa China Communist Party [CCP], bali kuna Communist Party Of China [CPC], sames to Vietnam hakuna kitu kinacho itwa Vietnam Communist Party[VCP] bali kuna Communist Party Of Vietnam[CPV].
 
Back
Top Bottom