Kwanini China inapendwa na Marais wa Afrika?

Kwanini China inapendwa na Marais wa Afrika?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Pamoja na nchi za Afrika kutaka kujitegemea ila viongozi wake wamekuwa wepesi sana kutaka sifa za kijinga kwa kununua au kukopeshwa fedha kupitia miradi ambayo hugeuka mzigo kwa wananchi.

Mikataba ya China hufanywa siri kubwa wakati miradi inaanza ila unapofika muda wakuilipa ndipo mijadala uibuka kutoka kona mbalimbali kuhusu kitanzi watawala walivyotuvisha.

Je, nani anawadanganya viongozi wa Afrika kwamba kutengeneza madeni yasiyo na tija kutainufaisha nchi siku za mbeleni?

Natamani viongozi wetu wawe na:

1. Vipaumbele
2. Wawazi kwa wananchi
3. Hofu ya Mungu hasa kuhusu kudanganya waliowapa kura
4. Waadilifu
5. Wakubali kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi
 
Sasa hapo namba moja (vipaumbele) ndio wanapoanzia kufanya hicho unacho kipinga.

Yaani kiongozi wa juu kama Raisi kwenye mambo ya fedha hasa mikopo anatakiwa ashauriane kwa kina na bunge
 
Sasa hapo namba moja(vipaumbele) ndio wanapoanzia kufanya hicho unacho kipinga.
Yaani kiongozi wa juu kama Raisi kwenye mambo ya fedha hasa mikopo anatakiwa ashauriane kwa kina na bunge

Bunge lenyewe lipi? Hilo bunge ambalo yeye ndio kalipitisha ndio watashauriana? Kwa bunge hili kibogoyo yeye ataliagiza na lenyewe litaishia kutii tu.
 
Kwa sababu wana mashart nafuu ambayo baadae husababisha bandari na viwanja vya ndege kuendeshwa na wachina wenyewe..
 
Kwa sababu wana mashart nafuu ambayo baadae husababisha bandari na viwanja vya ndege kuendeshwa na wachina wenyewe
Masharti nafuu? Wachina wanaiteka africa kwa mikopo mikubwa ambayo wanajua dhahiri haito lipika. Ndipo hapo huja kwa back door na kudemand rasilimali.

Ni wajanja sana.
 
Masharti nafuu? Wachina wanaiteka africa kwa mikopo mikubwa ambayo wanajua dhahiri haito lipika. Ndipo hapo huja kwa back door na kudemand rasilimali.

Ni wajanja sana.
Nadhani hujaelewa nilicho andika tumemaanisha kitu kimoja
baadae husababisha bandari na viwanja vya ndege kuendeshwa na wachina wenyewe
 
Sasa hapo namba moja(vipaumbele) ndio wanapoanzia kufanya hicho unacho kipinga.

Yaani kiongozi wa juu kama Raisi kwenye mambo ya fedha hasa mikopo anatakiwa ashauriane kwa kina na bunge
Bunge lenyewe, wenye PhD na Masters zao wanafikiri kama kibajaji? Ukiwa upande ule wimbo ni mmoja tu sifiaaaaa tumbo liendelee kukua
Au nasema uongo jamani?🦹🦹
Mitano tenaaaa
 
Masharti nafuu? Wachina wanaiteka africa kwa mikopo mikubwa ambayo wanajua dhahiri haito lipika. Ndipo hapo huja kwa back door na kudemand rasilimali.

Ni wajanja sana.
Tulisoma kwenye historia Open door policy by USA na Neo-Colonialism. Wajukuu wetu watasoma mfumo mpya unaohasisiwa na China sijui utaitwaje labda Loa - Resourcism policy by China
Au nasema uongo jamani?
Ndukiii.......
 
Hahahh mambo yale yale yanajirudia. Ila bwana ni tofauti
 
Uhusiano wa China na viongozi wa kiafrika.
tapatalk_1536724762447.jpg
 
Mikopo ya China haina ufuatiliaji kwani wao wanajua pa kuja kuwashikia (mrejesho na riba) hata mkigawana haiwahusu.
Mikopo ya wazungu hupenda pia kujua inatumikaje (kitu ambacho hakipendwi sana na 'wakopaji')
 
Pamoja na nchi za Afrika kutaka kujitegemea ila viongozi wake wamekuwa wepesi sana kutaka sifa za kijinga kwa kununua au kukopeshwa fedha kupitia miradi ambayo hugeuka mzigo kwa wananchi.

Mikataba ya China hufanywa siri kubwa wakati miradi inaanza ila unapofika muda wakuilipa ndipo mijadala uibuka kutoka kona mbalimbali kuhusu kitanzi watawala walivyotuvisha.

Je, nani anawadanganya viongozi wa Afrika kwamba kutengeneza madeni yasiyo na tija kutainufaisha nchi siku za mbeleni?

Natamani viongozi wetu wawe na:

1. Vipaumbele
2. Wawazi kwa wananchi
3. Hofu ya Mungu hasa kuhusu kudanganya waliowapa kura
4. Waadilifu
5. Wakubali kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi
Kichwa chako cha Habari kingekuwa 'Kwanini China inapendwa sana na Marais Mbumbumbu baadhi wa Afrika?' Kingependeza na Kueleweka mno.
 
China ndie mfadhili mkuu wa madikteta yote afrika, madikteta upenda China sababu china kwake demokrasia halina nafasi hata mkiuwana mkaisha nyote hana shida, mabeberu Wana utu uheshimu utu na awapo tayari kufadhili au kutoa Pesa kwenye miradi yenye dhuluma mfano kutoa pesa kujenga barabara ambao watu wametendewa unyama wa kubomolewa nyumba zao Kama mifugo hapa beberu Pesa yake upati ya mchina utapata, kupita bila kupingwa beberu atoi pesa mchina anatoa.
Baada ya Uhuru watawala wa kiafrica walifunga ndoa na China Ili iwasaidie kukaa mda mrefu madarakani huku wakikiuka haki za binadamu kwa kuwageuza waafrika bucha.Walikwepa kambi ya magharibi sababu waliogopa mambo ya demokrasia,haki za binadamu, kutawala kwa kuachiana.
 
Back
Top Bottom