Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

Chato ni kubwa kuliko Butiama?, morogoro,na TANGA?
USINITUKANE JIBU SWALI.

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
Kiukweli Chato ni ndogo.
Tanga kubwa, mfano Morogoro ikigawanywa kuwa mikoa miwili, haitochukua ardhi kutoka wilaya ya mkoa wowote, labda yenyewe ndiyo igawe maeneo kwa mikoa jirani..

Kwanini serikali ianzishe mjadala wa Mkoa wa Chato, utakaoleta migogoro ya ardhi baina ya mikoa?? Kwani mikoa ya Kigoma na Kagera wameridhia kumegwa??

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Ni kwasababu Rais aliepita alitaka hivyo. Kwanini alitaka hivyo? ni kwasababu Chato ni kwao. Kwa hiyo jibu ni ubinafsi.

Bora wangegawa Moro watu wangewaelewa.
Hata mkoa wa Mara ukigawanywa ina make sense tena sana tu. Kwa mfano wilaya ya Serengeti ndiyo liwe jina la mkoa. Wilaya ya Bunda iwe makao makuu ya mkoa wa Serengeti. Ukerewe itolewe Mwanza iletwe mkoa wa Serengeti. Mugumu iwe wilaya ndani ya mkoa wa Serengeti. Kuugawa hivi mkoa wa Mara kutachochoea ukuwaji wa uchumi kwa kiasi kikubwa sana hasa ukizingatia ukubwa wa mkoa wenyewe lakini pia jina la Serengeti litazidi kuwa hewani zaidi hasa ukizingatia kwamba jina la mbuga ya Serengeti lataendelea kubaki kama lilivyo.
Hapa hakuna siasa ila Chato ni siasa.
 
Kiukweli Chato ni ndogo.
Tanga kubwa, mfano Morogoro ikigawanywa kuwa mikoa miwili, haitochukua ardhi kutoka wilaya ya mkoa wowote, labda yenyewe ndiyo igawe maeneo kwa mikoa jirani..

Kwanini serikali ianzishe mjadala wa Mkoa wa Chato, utakaoleta migogoro ya ardhi baina ya mikoa?? Kwani mikoa ya Kigoma na Kagera wameridhia kumegwa??

Everyday is Saturday............................... :cool:
Mkuu, mkoa wa Geita bado ni mchanga sana kuweza kuuvunja tena. Labda wasubiri 20 years to come. Morogoro ni kuuuubwa mno ndio inayopaswa kuvunjwa.
 
..kuna mtu amependekeza mkoa wa Geita ubadilishwe jina kuitwa mkoa wa Chato.

..nadhani uamuzi huo ni mrahisi zaidi kuliko kuunda mkoa mpya toka mikoa ya Geita na Kigoma.
Bado tu haijakaa vizuri kwa nini chato?
Hivi ikiachwa kama ilivyo nini kitatokea? Tanzania yetu hii bhana
 
Bado tu haijakaa vizuri kwa nini chato?
Hivi ikiachwa kama ilivyo nini kitatokea? Tanzania yetu hii bhana
..kuna watu wanahitaji FARAJA kutokana na msiba wa Magufuli.

..na wanalilia mkoa wa Chato kama faraja na namna ya kumuenzi Magufuli.
 
..kuna watu wanahitaji FARAJA kutokana na msiba wa Magufuli.

..na wanalilia mkoa wa Chato kama faraja na namna ya kumuenzi Magufuli.
Inatakiwa waendelee kua mkoani Geita sababu Magufuli amezaliwa mkoa humo wilaya ya Geita na ndipo walihamia chato.
Kwahiyo inatakiwa wabaki ili kuwe na muunganiko
 
Unauliza maswali ya kitoto kweli utafikiri hujaenda shule, ni kwamba serikali ndio yenye mamlaka ya kugawa au kutokugawa mikoa kutokana na vigezo ilivyojiwekewa. Hakuna mwenye mkoa wake hapa
Kiukweli Chato ni ndogo.
Tanga kubwa, mfano Morogoro ikigawanywa kuwa mikoa miwili, haitochukua ardhi kutoka wilaya ya mkoa wowote, labda yenyewe ndiyo igawe maeneo kwa mikoa jirani..

Kwanini serikali ianzishe mjadala wa Mkoa wa Chato, utakaoleta migogoro ya ardhi baina ya mikoa?? Kwani mikoa ya Kigoma na Kagera wameridhia kumegwa??

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom