Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

Sina shida na jina, na nadhani kila mwenye akili timamu alivyo. Tatizo kubwa ni kuwa hakuna sababu ya msingi.
Mkuu unajua umbali uliopo kutoka ngara kwenda Bukoba??? Kwa nini reason ya kusogeza huduma haiku-convice?? Hata serikali kuhamia Dodoma moja ya factor ni hyo kwa sababu ni katikati
 
Wewe ulimpenda, endelea kumenda? I hate him and will hate him forever. Kila mtu ashinde mechi zake. This Mwendazake shot Ben Saanane by his own pistol while under torture. Kisa Ben Saanane anataka Mwendazake athibitise PhD yake kama siyo ya kunakili kwa Dr Y Philip

He was a DEVIL!! Alimtuma Paul Makonda na kundi la WASIOJULIKANA wakammuue Tundu Lissu na akapanga akazikwe Ikungi chap chap bila kuletwa kuagwa DSM.

Yeye kafoji PhD halafu anawatoa kazini waliofoji Certificate za Form IV tu. Akapotezea Forgery ya kwake, ya Makonda, Palamagamba, Kigwangalla na Mwigulu. Mungu hapendi double standards, kama vipi angewapotezea wote.

Alidhani kuwa Rais wa Tz ni sawa na kuwa Mungu. Takataka mkubwa yule Mungu akamuonyesha kuwa wewe si lolote si chochote pamoja na ulinzi wa ma helicopter, mabunduki na mitambo ya internet akafa kwa COVID19.
Marehemu hasemwi mkuu
😭😭😭
 
Kwani Nyakanazi iko Mkoa wa Kigoma ? Nyakanazi iko wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, kwanini uwaze kuunganisha na Kakonko na Kibobdo ?
Kwa maneno yako mwenyewe umedai watu wa Kakonko walilalamikia umbali kufikia mkoani, na hii mmeifanya kuwa sababu ya kumega mkoa wa Kigoma, kama nia haina hila, basi Nyakanazi inafaa kukidhi vigezo vya kuwa mkoa kuliko Chato. Nyakanazi inakua haraka sana na tayari imeimeza Biharamlo na Ngara pia, Mila na desturi za watu wa Nyakanazi ni zile zile utakazozikuta Kibondo, Biharamlo, Ngara na Nyakanazi yenyewe lakini pia miundombinu imeanza kukaa sawa.
 
Muundo wa mikoa na wilya hutegemea idadi ya watu; haitegemei historia au ukubwa wa eneo! Halafu maamuzi haya yanafanyika wakati Magufuli hayupo tena, je yangefanyika akiwa hai ingekuwaje?
Sasa kama Mkoa unakizi vugezo kwa nini mchukue Kakonko toka Kigoma na Busanda toka Geita. Ni UJINGA tu mnaendekeza
 
Mkuu unajua umbali uliopo kutoka ngara kwenda Bukoba??? Kwa nini reason ya kusogeza huduma haiku-convice?? Hata serikali kuhamia Dodoma moja ya factor ni hyo kwa sababu ni katikati
Nafahamu sana. Hakuna mkoa ambao sijawahi kufika. Huwezi kusema umewapunguzia madhira ya umbali kufika makao makuu ya mkoa watu wa Ngara kwa kuweka makao makuu ya mkoa Chato. Chato ipo karibu sana na Geita.
 
..suluhisho ni kupeleka huduma Kakonko, Kibondo, na kwingine ambako wananchi wako mbali na makao makuu ya mkoa.
Sahihi kabisa!!, lakini kuna agenda ya Siri hapa katika kuanzisha mkoa wa Chato nayo ni uchu wa madaraka, kupeana vyeo na ulaji, hakuna kingine hapo.
 
Sengerema kiuhalisia ilitakiwa kuwa Geita maana ilikuwa ndani ya wilaya ya Geita hadi 1975.
Huo ndio uharibifu uliofanywa makusudi na watu walioaminiwa na kupewa Mamlaka, Je tukae kimya wakati hila zile zile zikifanyika kuunda mkoa wa Chato hata kama haukidhi vigezo?
 
Wizara ndio yenye mamlaka. Siyo hao waha wa Kakonko
Kauli kama hizi ndizo hutolewa na watu waliolewa madaraka, kumbuka Mamlaka yote waliyonayo viongozi na watendaji huko maofisini yanatoka kwa wananchi.
 
hawajamaa sitompigia kura kiongozi yeyote anaetoka hiyo mikoa maana wananongwa sana hawa jamaa.kiongozi amefariki amefariki kwa ugonjwa tu, wao wanaichukia serikali iliyopo sasa hata rais mtaafu.Hayo mambo kama rais mama Samia hakiukataa huo mpango wa mkoa mpya, utawaona watakavyomchukia
 
Nafahamu sana. Hakuna mkoa ambao sijawahi kufika. Huwezi kusema umewapunguzia madhira ya umbali kufika makao makuu ya mkoa watu wa Ngara kwa kuweka makao makuu ya mkoa Chato. Chato ipo karibu sana na Geita.
Uko sahihi kabisa ndo maana nasema pingamizi liwe kwa makao ya mkoa kuwa chato na si kupinga kuundwa mkoa
 
sasa hapo chtto kuna nini mpaka useme hivyo au hizo barabara mlizojengewa kwa hila au huo uwanja usiotumika?
Tofautisha Chato wilaya na Chato mkoa. Je wilaya za Kakonko, Bihalamulo, Ngara, Chato na Bukombe haziwezi kuunda mkoa.
 
Chato kuwa mkoa haijakaa vyema. Hii ilipaswa kuachwa kama wilaya ndani ya mkoa wa Geita.

Kwanini chato iwe mkoa kutoka kwenye mkoa mchanga wa Geita?

Ikumbukwe Geita ilitengwa kua Mkoa mwaka 2010 kipindi cha Jakaya tena iweje mkoa mchanga utoe mkoa mwingine wa Chato? Soma Kikwete atangaza mikoa, wilaya mpya

Serikali ingepaswa kuangalia mikoa mingine mikubwa ndio iweze kuikata kuzaa mikoa mingine, mfano mikoa inayostahili inaweza kua Tabora, Morogoro, Tanga, Singida, Ruvuma, n.k

Kuna haja gani ya kuunda mkoa Mpya wa Chato? Serikali iliangalie hili lasivyo kutakua na utitiRi wa mikoa kwa kila Rais ajae.

View attachment 1800958
_______________________________
Rejea Taarifa hizi

Geita yaridhia kuanzishwa Mkoa wa Chato. RCC yatoa mapendekezo. Baadhi ya maeneo kutoka mikoa jirani. RC Geita Mhe Rosemary Sitaki awashukuru Wananchi kukubaliana kwa hekima bila ushabiki.

Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa - REGIONAL CONSULTATIVE COMMITTEE (RCC), Kilichokaa kama kikao Maalum leo kwaajili ya Mapendekezo ya kuunda Mkoa Mpya wa Chato, Kimependekeza yafuatayo:

1. Mkoa Mama wa Geita ubakiwe na Wilaya tatu ambazo ni Wilaya ya Geita, Mbogwe na Wilaya ya Nyang'hwale.

2. Imependeleza iombwe Wilaya ya Sengerema ambayo ipo Mkoa wa Mwanza, ili iweze kukamilisha Wilaya nne za Geita pamoja na Wilaya Pendekezwa ya Busanda.

3. Mkoa wa Chato imependekezwa kwa iundwe na Wilaya za Geita ambazo ni Chato yenyewe, na Wilaya ya Bukombe.

4. Pia imependekezwa kutoka Kigoma, iombwe eneo kutoka Wilaya ya Kakonko, pia kutoka Kagera imependekezwa ziombwe Wilaya mbili ambazo ni Biharamulo na Wilaya ya Ngara.

Mapendekezo haya yamekamilika na yamekubaliwa na wajumbe wote wa RCC.

Sasa yatapelekwa kwenye Wizara husika ili yaweze kufanyiwa kazi.

Nini maoni yako kwenye hili?
Hapa ndipo mtu unajiuliza "hivi sisi watanzania ukomo wetu wa kufikiri unakomea wapi!!???" Tunafuata maslahi ya nchi au ni maslahi ya siasa zisizo na faida ya muda mrefu kwa taifa???
 
Back
Top Bottom