Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
6,642
2,000
Chato kuwa mkoa haijakaa vyema. Hii ilipaswa kuachwa kama wilaya ndani ya mkoa wa Geita.

Kwanini chato iwe mkoa kutoka kwenye mkoa mchanga wa Geita?

Ikumbukwe Geita ilitengwa kua Mkoa mwaka 2010 kipindi cha Jakaya tena iweje mkoa mchanga utoe mkoa mwingine wa Chato? Soma Kikwete atangaza mikoa, wilaya mpya

Serikali ingepaswa kuangalia mikoa mingine mikubwa ndio iweze kuikata kuzaa mikoa mingine, mfano mikoa inayostahili inaweza kua Tabora, Morogoro, Tanga, Singida, Ruvuma, n.k

Kuna haja gani ya kuunda mkoa Mpya wa Chato? Serikali iliangalie hili lasivyo kutakua na utitiRi wa mikoa kwa kila Rais ajae.

FB_IMG_16222622301036184.jpg

_______________________________
Rejea Taarifa hizi

Geita yaridhia kuanzishwa Mkoa wa Chato. RCC yatoa mapendekezo. Baadhi ya maeneo kutoka mikoa jirani. RC Geita Mhe Rosemary Sitaki awashukuru Wananchi kukubaliana kwa hekima bila ushabiki.

Kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa - REGIONAL CONSULTATIVE COMMITTEE (RCC), Kilichokaa kama kikao Maalum leo kwaajili ya Mapendekezo ya kuunda Mkoa Mpya wa Chato, Kimependekeza yafuatayo:

1. Mkoa Mama wa Geita ubakiwe na Wilaya tatu ambazo ni Wilaya ya Geita, Mbogwe na Wilaya ya Nyang'hwale.

2. Imependeleza iombwe Wilaya ya Sengerema ambayo ipo Mkoa wa Mwanza, ili iweze kukamilisha Wilaya nne za Geita pamoja na Wilaya Pendekezwa ya Busanda.

3. Mkoa wa Chato imependekezwa kwa iundwe na Wilaya za Geita ambazo ni Chato yenyewe, na Wilaya ya Bukombe.

4. Pia imependekezwa kutoka Kigoma, iombwe eneo kutoka Wilaya ya Kakonko, pia kutoka Kagera imependekezwa ziombwe Wilaya mbili ambazo ni Biharamulo na Wilaya ya Ngara.

Mapendekezo haya yamekamilika na yamekubaliwa na wajumbe wote wa RCC.

Sasa yatapelekwa kwenye Wizara husika ili yaweze kufanyiwa kazi.

Nini maoni yako kwenye hili?
 

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,413
2,000
Chato itabakia kuwa Gbadolite ya Tanzania. Mungu hakupenda ujinga na UPUMBAVU wa Mwendazake kuchukua raslimali za nchi na kwenda kuzirundika kijijini kwake Chato.

Ndiyo maana akamdedisha. Magufuli alikuwa IBILISI. Ni misukule yake tu ndiyo imebaki inamuita shujaa wa Afrika. Labda wa Afrika Sana pale Corner bar alipopatia UKIMWI
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,745
2,000
Chato iliandaliwa iwe Mkoa na ndio maana wakaweka kila kitu ili iwe na hadhi ya Mkoa
Ila kama tutaendelea hivi tutajikuta kila Rais ataamua anavyotaka

Bora majimbo machache na kila jimbo kujitegemea kwa uzalishaji wake na maendeleo pia
 

GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
2,052
2,000
Najiuliza tu, hivi wakazi wa wilaya ya Kakonko au mkoa mzima waliulizwa kuhusu wilaya ya mkoa wa Kigoma kumegwa na kutengeneza mkoa wa Chato? Je, waliafikiana na mpango huo?.

Kama lengo ni kugawanya ili kusogeza huduma za kiutawala karibu na wananchi, ni kwa nini Tanzania nzima isigawanywe upya ili kuwe na usawa katika mgawanyo kwa kuzingatia vigezo vinavyofahamika?.
 

nizakale

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
2,317
2,000
Mtakufa kwa vijiba moyo
Chato itabakia kuwa Gbadolite ya Tanzania. Mungu hakupenda ujinga na UPUMBAVU wa Mwendazake kuchukua raslimali za nchi na kwenda kuzirundika kijijini kwake Chato.

Ndiyo maana akamdedisha. Magufuli alikuwa IBILISI. Ni misukule yake tu ndiyo imebaki inamuita shujaa wa Afrika. Labda wa Afrika Sana pale Corner bar alipopatia UKIMWI
 

nizakale

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
2,317
2,000
Mmpeleka mapendekezo serikalini enyi watu wafupi mkakataliwa ?
Ni kwasababu Rais aliepita alitaka hivyo. Kwanini alitaka hivyo? ni kwasababu Chato ni kwao. Kwa hiyo jibu ni ubinafsi.

Bora wangegawa Moro watu wangewaelewa.
 

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
1,944
2,000
1. Morogoro
2. Pwani
3. Tabora
4. Lindi hii ni ya kukata kwanza kabla ya Geita iyo changa na ndogo
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
14,071
2,000
Andiko zuri sana.
Kama hawatakusikiliza basi waache lakini kiburi kitawaumbua kama kinavyowaumbua kwa kuanzisha mikoa waliyokurupuka.
Wakati wanataka kuanzisha mkoa wa Katavi walipendekeza Wilaya ya Kaliua iende mkoa wa Katavi, Mungu mwema wale Wanyamwezi waligoma katakata na wengi tuliwasapoti.

Kutoka Kaliua hadi Mpanda hakuna barabara ya moja kwa moja kuna reli tu. Ukiwa na gari mpaka urudi Tabora/Sikonge then Mpanda. Lakini pia wakasema wanaenzi utamaduni na asili yao inayowanasibisha na Mtemi Mirambo. Leo unawachukua Waha wa Kakonko na kuwafurusha kwenda Chato? Wakikubali nitajua Mha kabadilika.

Bora hata wangeanzisha mkoa wa Kahama, au wangeigawa Morogoro mara mbili maana ukubwa wake unatisha.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,325
2,000
Kupitia hizo data ulizo ziweka hapo juu, Tabora na Morogoro ndiyo Mikoa sahihi iliyostahili kupewa kipaumbele cha kugawanywa. Huo upuuzi unaoitwa Chato hauna lolote la maana zaidi tu ya kuendeleza ujinga, ubaguzi na upendeleo wa wazi uliofanywa na magufuli enzi za uhai wake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom