The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,950
- 12,549
Hebu tuwaulize na ninyi CCM (tena baadhi tu wapuuzi na wajinga wa mpaka kisogoni!) kwa nini mmeng,ang'ania hii kitu mnaouita "MWENGE WA UHURU?". Si ni kwa sababu mnachangisha fedha kwa lazima kwa wananchi kwa ajili ya kujinufaisha? Mfano wa hili uko wazi sana na nakupa picha ya mambo yalivyokuwa takribani mwezi mmoja uliopita jinsi watu walivyopata adha katika maeneo ya huku ninapoishi eti kwa sababu ya mwenge;
KWA NINI CHADEMA WANAUPINGA MWENGE WA UHURU?
Kwanza naomba nikusahihishe kwa kukuambia kuwa you are making a big mistake unapokuwa hutaki kufanya mabadiliko ya kifikra, unapokuwa hutaki kubadili mitazamo yako (mindset) katika mambo mbalimbali kwa kudhani kuwa kila kinachopingwa/kosolewa na CHADEMA kinachotokana/asisiwa na serikali ya CCM basi ni kibaya!!.
Aidha si tu CHADEMA wanaopinga hili hata CCM wanaathiriwa sana na sera na mipango ya serikali yao wenyewe.Mfano leo ktk Bunge katika mjadala wa ishu hii ya Mwenge karibu kila Mbunge bila kujali itikadi zao za kisiasa walikuwa wanaonekana wazi kutoridhishwa na majibu ya serikali kuutetea mwenge.Na mmoja wa wabunge wa CCM waliopata nafasi ya kusema kuhusu mwenge ni mbunge Kessy nadhani ni wa huko Nkasi - Mpanda. Huyu bwana ni CCM na alionesha wazi kutoridhishwa na falsafa ya MWENGE WA UHURU kwa sasa kwani dhima nzima iliyokusudiwa imeshapitwa na wakati na badala yake mwenge ni kama vile unaongeza matatizo ambayo ulipaswa kuyatowesha mfano; umaskini, Rushwa na ufisadi,maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa njia ya ngono nk nk
Kwa hiyo basi CHADEMA hawaoni umuhimu wa Mwenge wa Uhuru kwa sasa kwa sababu logic nzima ya Mwenge ilishapotoshwa na CCM na badala yake mwenge umekuwa ukileta adha isiyo kifani kwa wananchi. Na ndiyo kusema kwamba CHADEMA wanaongea yaliyo miyoni mwa wananchi, wanawakilisha mawazo halisi ya wananchi.!!
- Kwanza ni MICHANGO YA LAZIMA iliyosimamiwa na wakuu wa wilaya kupitia kwa watendaji wa vijiji na kata na kwa watumishi wakurugenzi waliagiza wakuu wa idara kuchangisha fedha toka kwa watumishi walio chini yao na kwa kwa hiyo;
- Kila mtumishi alilazimishwa kuchangia Tshs 2,000/=
- Kila taasisi zililazimishwa kuchangia fedha mfano; Tshs. 10,000/= (shule za msingi), Tshs. 20,000/= (shule za sekondari) nk nk kutegemea na ukubwa wa taasisi
- Kila mfanyabiashara alilazimishwa kuchangia kati ya Tshs 2,000; 3,000; 5,000 na 10,000 kutemea na ukubwa wa biashara
- Mwenge huleta usumbufu sana kuliko manufaa na kinyume na malengo unapokuwa unapita katika maeneo ya watu; mfano ni kusimama kwa shughuli nyingi za kiofisi na uzalishaji katika taasisi nyingi za umma kwa sababu wengi wa maafisa hasa katika ngazi ya wilaya hujikuta wako bize kwa shughuli za mwenge na watu kukosa huduma kwa hata wiki nzima bila sababu yoyote ya msingi zaidi ya hii kitu MWENGE WA UHURU iliyopitwa na wakati!!