Tanzania kama nchi nyingine za Afrika zinahitaji misaada ili kutoa huduma kwa wananchi. Unapozouia misaada maana yake unadhamiria kuwanyima watoto huduma za chanjo, matibabu na elimu. Unawanyima wananchi huduma za barabara, madaraja na pembejeo. Hasara kubwa sana kwa wananchi kuliko kwa viongozi.
Wanafiki kweli nyie..
Kumbe sio mabeberu tena ila ni wahisani wa kuwapa misaada?
Je, Lisu ana thamani hiyo?
Absolutely, Yes...
Nijuavyo mimi kuinyima serikali misaada kutoka kwa wahisani kunasababisha yafuaatayo:
Mpaka hapa uko sahihi kabisa...
Kwamba inayokatwa miguu na mikono kwa kukatiwa misaada ni serikali na sio wananchi...
Kumbuka kuwa serikali ni kikundi kidogo tu cha watu chenye mamlaka ya kufanya maamuzi ya uendeshaji wa mambo ya nchi/taifa kwa niaba ya wananchi wote...
Kuna serikali halali zilizotwaa madaraka kwa ridhaa ya wananchi kupitia chaguzi huru, wazi na za haki...
Lakini pia zipo serikali dhalimu na za kidikteta zilizojiweka madarakani kwa nguvu ya mtutu wa bunduki, Mapinduzi ya kijeshi or through manipulated elections...
Serikali dhalimu zilizojiweka madarakani ndizo ambazo hupigwa vita ndani na nje ya nchi. Hizi ndizo huwekewa vikwazo vya kiuchumi kama njia ya kuzikata miguu na mikono Ili zikose uwezo wa kuendelea kuvunja haki za binadamu, kuteka, kutesa na kuua watu, kuiba na kufisadi rasrimali za umma ikiwemo misaada ya kifedha toka washirika wa maendeleo na udhalimu mwingine...
Itasaidia nini kuipacmisaada ya kifedha serikali dhalimu na ovu yenye viongozi wezi na mafisadi ambapo fedha badala ziende kwenye kuhudumia watu wapate barabara, maji, umeme, madawa nk wao wanaiba na kuzitumia kujilinda kwa kufadhili vikundi vya viongozi hawa vya utekaji, utesaji na mauaji ya raia wanaowakosoa..??
Ni kweli kwa kuwekewa vikwazo hivi, madhara yake yatatukuta sote kwa sababu:
👉 Serikali iliyoko madarakani itakosa uwezo wa kutoa huduma za kijamii kwa wananchi wake kama vile maji, madawa hospitalini, ujenzi wa barabara, miradi kama SGR kukwama kuendelea nk
Hii ikitokea, wananchi wataanza kuilalamikia na kuishutumu CCM na serikali na serikali yao na sio CHADEMA kwa sababu CHADEMA hawaongozi serikali...
Kwa hiyo ni ujinga uliopindukia kwako wewe
kavulata kudhani kuwa wananchi ni wajinga kama ulivyo wewe na wenzako huko CCM kwamba mambo yanapokwenda mrama ktk nchi hawajui wamlaumu nani...!!
Hali hii mbaya ikizidi, ndipo hapo wananchi hukasirika na kufanya direct confrontation njia mbalimbali ikiwemo maandamano, migomo na sehemu zingine physical confrontation (mapigano) lengo likiwa ni kuifurusha serikali iliyoko madarakani kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake kuhudumia wananchi wake...
Serikali yenye viongozi wenye akili huwa haisubiri hali hii itokee. Bali husikiliza wananchi wanasema nini, wanatoka nini kifanyike na Kisha kuchukua hatua before it's too late...
Lakini hii ya Samia Suluhu Hassan, akili ni kisoda. Ni serikali iliyo chini ya washenzi, wasioelewa kitu na wako tayari kufa kama inzi kufia kwenye kidonda...!