Kwanini CHADEMA bado inastahili kuadhibiwa kwenye sanduku la kura? Soma hapa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,305
Leo nimeona nitumie haki yangu ya kikatiba kueleza sababu chache za muhimu kwanini CHADEMA bado wanastahili kuadhibiwa kwenye sanduku la kura na wazalendo wote. Kwanza kabisa niseme kuwa sina chuki yoyote na hiki chama kinachojifia. Mimi kama mkristo ninaamini kila kitu kina mwisho wake isipokuwa Mungu tu. Siwezi kuzuia mwisho wa CHADEMA. Tatizo ni huu mwisho umekuwa wa ghafla. Huwa tunasema "nimevipiga vita vilivyo vizuri, na mwendo nimeumaliza" lakini kwa CHADEMA vita walivipiga ila mwendo ukakatishwa mwaka 2015 kwa tamaa za watu wachache walioamua kumuuzia chama mtu waliyemwita fisadi.

Pamoja na kwamba ni chama kilichopo kwenye mwisho wa uhai wake bado kinastahili kuendelea kupokea adhabu kali kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wowote ndani ya Tanzania. Sababu zifuatazo zizingatiwe;

1. KUTOTII KATIBA YAO WENYEWE: Hii sababu inaweza kuwa inatosha kabisa kusema CHADEMA hakistahili kushinda uchaguzi wowote. Kabla ya utawala wa Sultani Mbowe hiki chama kilikuwa kinafuata katiba yake na kuheshimu sana vipindi vya uongozi. Ila kwa sababu anazozijua Mbowe akaamua kubadili katiba na kujiruhusu kugombea uenyekiti kwa nyakati zote. Watu wote waliojitokeza kutaka uenyekiti waliishia pabaya. Kama ndani ya chama hali ni hii vipi wakipewa nchi?

2. UKANDA, UDINI NA UKABILA: Hii ni kansa ambayo imeshindikana kutibiwa. Imeshaitafuna CHADEMA vya kutosha. Tunaona walioko mstari wa mbele kwenye hatari zote ni watu wa kanda zingine na makabila mengine kama Mdude na Lissu. Ila wamiliki wa chama toka kaskazini huwakuti kwenye hekaheka zozote. Kuhusu udini sina haja ya kuelezea sana kwa sababu CHADEMA wenyewe waliamua kujitokeza hadharani kuonyesha rangi zao kwa kupitia mkutano wa kisiasa uliohutubiwa na viongozi wa dini. Mkutano wa Temeke ni doa baya lisilofutika kwenye siasa za CHADEMA.

3. UBADHIRIFU NA UFISADI WA FEDHA ZA CHAMA: Hapa viongozi na makada wa chama hiki huwa wakali sana wanapoulizwa kuhusu matumizi ya fedha za chama. Kimsingi fedha za hiki chama zinatafunwa na wajanja wachache. Kumekuwa na matumizi ya hovyo yanayoacha maswali mengi. Hadi leo michango ya Join The Chain haijulikani ilitumikaje. Viongozi wote wanakwepa kuongelea. Bilioni 1.5 wametumia kununua pagale huko Mikocheni. Yaani thamani ya pesa haionekani unapotazama lile pagale na 1.5b. Hawa wakipewa hazina ya nchi si itakuwa balaa?

4. KUTOKUWA NA SERA WALA AGENDA: Hili tatizo halikuwepo kabisa kabla ya 2015 lakini baada ya hapo chama kimebaki na makada watupu vichwani wanaowaza kutukana tu. Wanatukana hadi Rais wa jamhuri Hata kwenye huu uzi wanaweza kujitokeza. Baada ya cream nzima ya CHADEMA kuondoka na kuunga mkono juhudi za serikali ya CCM ikawa pigo kubwa kwa Mbowe na chama chake. Kimsingi viongozi na wanachama waliopo kwa sasa hawana hoja zaidi ya matusi.

5. KUTOKUWA NA MSIMAMO:
Hili tatizo linarekebishika kwa kupata wanachama wapya watakaopata nafasi ya kuongoza. Hiki chama kimekosa msimamo na kuamua kudandia kila hoja itakayojitokeza mbele yake. Kuna wakati chama kizima kilijitokeza kupinga mwanamuziki Diamond Platinumz asipigiwe kura kwenye tuzo. Ilikuwa ni aibu.

6. HAKINA HESHIMA KWA WANAWAKE: Hapa hakuna cha kuongea sana kwasababu kila kitu kipo wazi. CHADEMA kuwaita wabunge wake wa viti maalum Covid19 ni jambo watakalojutia daima. Kina mama waliokipigania chama kwa jasho na damu walizawadiwa jina la Covid19. Hii ni laana. Bahati nzuri hata wanawake wa CHADEMA kupitia BAWACHA walishatambua janja janja ya kina Mbowe na kuamua kumwalika Mama Samia kuwa mgeni rasmi kwenye siku yao. Hii inamaanisha kuwa 2025 wanawake wote kura kwa Samia.

Nimalize kwa kuwasihi wazalendo wote wa nchi hii kufanya kama tulivyokubaliana. Ni kukiadhibu chama cha Mbowe kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wowote ule.
 
Mleta mada ni mpumbavu sana
IMG-20230912-WA0001.jpg
 
Hii mada ni ya CCM, umeamua kuweka CHADEMA badala ya CCM! Kila penye CHADEMA Weka CCM then utaona kitu kitakavyosomeka vizuri
 
Umekula? Uchawa usio na faida huo. Tafuta hotuba ya nape kule mkuranga uisikilize Kisha urudi hapa Kama hujaishiwa nguvu na kulegea!
 
Wahuni wa ndani ya Chama na Serikali walipoona Mama nawaelewa sana Chadema na anataka kuwapa maridhiano ambayo yanaweza kuhatarisha Mustakbali wa Chama hapo 2025 ikabidi wawasukumie Chadema fupa la Bandari nao wakalivamia na matokeo yake Maridhiano yamezikwa

wanafurahi sana kwa chini kwa chini maana maridhiano yangeweza kuleta athari kwny vyeo vyao.

Pengine ( sina hakika ) Wahuni waliowatoa 2014 Bungeni ili wasimalizie mchakato wa Katiba mpya ndio hao hao waliwapa hoja ya Bandari
 
Huu wimbo wa CHADEMA kuuawa nilianza kuusikia tang awamu ya jiwe na ubabe wote lkn CDM naona imezid kuimarika!! NB; Endelea kutafuta vyanzo muhimu vya hbr ili ukija kuishambulia CDM angalau uwe na facts!!
 
Daaah!....
Hata waasisi wa CCM hawezi kuandika hoja kwa upendeleo kama hivi..Fuatilia hata hotuba za Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere utaona alivyokuwa akikisemea chama.
 
Leo nimeona nitumie haki yangu ya kikatiba kueleza sababu chache za muhimu kwanini CHADEMA bado wanastahili kuadhibiwa kwenye sanduku la kura na wazalendo wote. Kwanza kabisa niseme kuwa sina chuki yoyote na hiki chama kinachojifia. Mimi kama mkristo ninaamini kila kitu kina mwisho wake isipokuwa Mungu tu. Siwezi kuzuia mwisho wa CHADEMA. Tatizo ni huu mwisho umekuwa wa ghafla. Huwa tunasema "nimevipiga vita vilivyo vizuri, na mwendo nimeumaliza" lakini kwa CHADEMA vita walivipiga ila mwendo ukakatishwa mwaka 2015 kwa tamaa za watu wachache walioamua kumuuzia chama mtu waliyemwita fisadi.

Pamoja na kwamba ni chama kilichopo kwenye mwisho wa uhai wake bado kinastahili kuendelea kupokea adhabu kali kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wowote ndani ya Tanzania. Sababu zifuatazo zizingatiwe;

1. KUTOTII KATIBA YAO WENYEWE: Hii sababu inaweza kuwa inatosha kabisa kusema CHADEMA hakistahili kushinda uchaguzi wowote. Kabla ya utawala wa Sultani Mbowe hiki chama kilikuwa kinafuata katiba yake na kuheshimu sana vipindi vya uongozi. Ila kwa sababu anazozijua Mbowe akaamua kubadili katiba na kujiruhusu kugombea uenyekiti kwa nyakati zote. Watu wote waliojitokeza kutaka uenyekiti waliishia pabaya. Kama ndani ya chama hali ni hii vipi wakipewa nchi?

2. UKANDA, UDINI NA UKABILA: Hii ni kansa ambayo imeshindikana kutibiwa. Imeshaitafuna CHADEMA vya kutosha. Tunaona walioko mstari wa mbele kwenye hatari zote ni watu wa kanda zingine na makabila mengine kama Mdude na Lissu. Ila wamiliki wa chama toka kaskazini huwakuti kwenye hekaheka zozote. Kuhusu udini sina haja ya kuelezea sana kwa sababu CHADEMA wenyewe waliamua kujitokeza hadharani kuonyesha rangi zao kwa kupitia mkutano wa kisiasa uliohutubiwa na viongozi wa dini. Mkutano wa Temeke ni doa baya lisilofutika kwenye siasa za CHADEMA.

3. UBADHIRIFU NA UFISADI WA FEDHA ZA CHAMA: Hapa viongozi na makada wa chama hiki huwa wakali sana wanapoulizwa kuhusu matumizi ya fedha za chama. Kimsingi fedha za hiki chama zinatafunwa na wajanja wachache. Kumekuwa na matumizi ya hovyo yanayoacha maswali mengi. Hadi leo michango ya Join The Chain haijulikani ilitumikaje. Viongozi wote wanakwepa kuongelea. Bilioni 1.5 wametumia kununua pagale huko Mikocheni. Yaani thamani ya pesa haionekani unapotazama lile pagale na 1.5b. Hawa wakipewa hazina ya nchi si itakuwa balaa?

4. KUTOKUWA NA SERA WALA AGENDA: Hili tatizo halikuwepo kabisa kabla ya 2015 lakini baada ya hapo chama kimebaki na makada watupu vichwani wanaowaza kutukana tu. Wanatukana hadi Rais wa jamhuri Hata kwenye huu uzi wanaweza kujitokeza. Baada ya cream nzima ya CHADEMA kuondoka na kuunga mkono juhudi za serikali ya CCM ikawa pigo kubwa kwa Mbowe na chama chake. Kimsingi viongozi na wanachama waliopo kwa sasa hawana hoja zaidi ya matusi.

5. KUTOKUWA NA MSIMAMO: Hili tatizo linarekebishika kwa kupata wanachama wapya watakaopata nafasi ya kuongoza. Hiki chama kimekosa msimamo na kuamua kudandia kila hoja itakayojitokeza mbele yake. Kuna wakati chama kizima kilijitokeza kupinga mwanamuziki Diamond Platinumz asipigiwe kura kwenye tuzo. Ilikuwa ni aibu.

6. HAKINA HESHIMA KWA WANAWAKE: Hapa hakuna cha kuongea sana kwasababu kila kitu kipo wazi. CHADEMA kuwaita wabunge wake wa viti maalum Covid19 ni jambo watakalojutia daima. Kina mama waliokipigania chama kwa jasho na damu walizawadiwa jina la Covid19. Hii ni laana. Bahati nzuri hata wanawake wa CHADEMA kupitia BAWACHA walishatambua janja janja ya kina Mbowe na kuamua kumwalika Mama Samia kuwa mgeni rasmi kwenye siku yao. Hii inamaanisha kuwa 2025 wanawake wote kura kwa Samia.

Nimalize kwa kuwasihi wazalendo wote wa nchi hii kufanya kama tulivyokubaliana. Ni kukiadhibu chama cha Mbowe kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wowote ule.
7. Makamu Mwenyekiti wao, Tundu Lissu kujionesha wazi wazi kuwa anatumikia nchi za ulaya kufanikisha kutwaa nchi yetu. Ni wazi kabisa huyu jamaa ni kibaraka na jasusi wa hizo nchi
 
Highlights tu juu Nilipoona mwishoni Umeandika ujinga kuhusu COVID 19 nikaona uzi wote umekata ladha.

Inshort umeandika Mavi
 
Back
Top Bottom