Kwanini CAG, TRA na TAKUKURU Wasimchunguze Makonda?

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (Daudi Bashite?) ni miongoni mwa wakuu wa mikoa maarufu sana kwenye serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli. Pamoja na mambo mengine ni mtu anayaonekana ana dhamira ya kuibadili Dar es salaam kuwa mji wenye maendeleo ya vitu mbali mbali.

Makonda anatoa hela na ahadi kwenye miradi mbali mbali wakati mwingine ahadi zake zinafikia hadi mabilioni ya shilingi. Inasemwa kwamba alipoingia tu Ofisini kama Mkuu wa Mkoa alibadili kabisa muonekano wa ofisi ile tofauti na ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Mzee Meck sadiq.

Kuleta maendeleo si jambo baya lakini kama kiongozi wa umma ni lazima hela za kuleta hayo maendeleo vyanzo vyake vifahamike na viwe safi na kusiwe na muingiliano wa kimaslahi kati ya hao watoa hela na nafasi uliyo nayo kisiasa.

Ahadi kama kusaidia kujenga jengo la BAKWATA ni ahadi kubwa sana na kama Makonda ataitekeleza basi inabidi aeleze hela za kutekeleza ahadi hiyo kaitoa wapi. Juzi tumeambiwa yeye mwenyewe kwa "juhudi zake" amefanikisha kukarabati magari kadhaa ya Polisi yaliyokuwa yameshindikana kukarabatiwa kwa kipindi kirefu sana.

Inabidi TRA wachunguze kama hao "wanaomsadia" Makonda wanalipa kodi stahiki kwa biashara zao wanazofanya ama wanatumia "misaada" wanayotoa kwa Makonda kama kichaka chao cha kujificha wasilipe kodi stahiki wanayotakiwa kulipa?

CAG naye achunguze kama kweli fedha za umma ndizo zinatumika kwenye miradi ambayo makonda anaiwezesha kutekelezwa. Hii ni muhimu kwani kwa mujibu wa sheria zetu ofisi ya Mkuu wa mkoa hazina fungu la maendeleo bali Halmashauri zilizo katika mkoa husika.

CAG aangalie kama maafisa maduhuri na masuhuri kwenye Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam na Ofisi ya Mkoa ni wao wanaoidhinsha matumizi ya fedha hizo ama kazi yao ni kuandika tu taarifa baada ya fedha kutumika.

TAKUKURU nao wachunguze kama misaada inayotolewa kwa Makonda haina dalili ya kirushwa. Maana fedha zinazotolewa kibinafsi zinakujaje kufanya kazi za umma kama huyu mtoaji hana dalili za kutoa rushwa. Ni kwa nini hao watoa "misaada" wasiitoe kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam badala yake wanaikabidhi kwa Makonda binafsi na si kama Mkuu wa Mkoa?
Atachunguzwa awamu hii ikipita, kwa sasa hizo taasisi unazozitaja zimepigwa ganzi. Usije
 
Hizo Pesa atakuwa kapewa rushwa na wapiga deal wakwepa kodi. Hana uwezo wa kuwa na fedha hizo anazotoa misaada hovyo hovyo. Kama Si hivyo basi atakuwa amepewa Hazina ili kumfanyia publicity!!! Na hii inawezekana kabisa kwani Ngosha kwa Bashite hapindui!!! Kila anachokisema Bashite lazima Ngosha akubali!! Atakuwa alimpeleka kwa Mganga si bure hili Limbwata!!![emoji3]
Makonda hatoi pesa mfukoni mwake.kuongoza ni sayansi tu,nenda TBL,waambie nina shida ya vyoo 100 mkoani mwangu,watakujengea walau kimoja kwa sababu pesa hiyo wanayo,inatengwa kila mwaka kurudisha faida kwenye jamii
 
Nashanga sijui kwanini hatafutwi,yaani ana mali kibao,anatumia magari ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya,yet anatoa mapesa na vitu kibao pesa anatoa wapi ya hayo yote???
 
Wewe umeshapimwa mkojo? Kumchunguza huyo ni sawa na kumchunguza baba yake. Angalia nyuma yako inakuja Nissan patrol nyeupe na ndani kakaa mwenye kapero shauri yako
 
Sorry muanzisha thread hivi majibu ya ile iliyosomwa bado hajaanza kujibu???Maana kesho kutwa inatimiza wiki/siku saba
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (Daudi Bashite?) ni miongoni mwa wakuu wa mikoa maarufu sana kwenye serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli. Pamoja na mambo mengine ni mtu anayaonekana ana dhamira ya kuibadili Dar es salaam kuwa mji wenye maendeleo ya vitu mbali mbali.

Makonda anatoa hela na ahadi kwenye miradi mbali mbali wakati mwingine ahadi zake zinafikia hadi mabilioni ya shilingi. Inasemwa kwamba alipoingia tu Ofisini kama Mkuu wa Mkoa alibadili kabisa muonekano wa ofisi ile tofauti na ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Mzee Meck sadiq.

Kuleta maendeleo si jambo baya lakini kama kiongozi wa umma ni lazima hela za kuleta hayo maendeleo vyanzo vyake vifahamike na viwe safi na kusiwe na muingiliano wa kimaslahi kati ya hao watoa hela na nafasi uliyo nayo kisiasa.

Ahadi kama kusaidia kujenga jengo la BAKWATA ni ahadi kubwa sana na kama Makonda ataitekeleza basi inabidi aeleze hela za kutekeleza ahadi hiyo kaitoa wapi. Juzi tumeambiwa yeye mwenyewe kwa "juhudi zake" amefanikisha kukarabati magari kadhaa ya Polisi yaliyokuwa yameshindikana kukarabatiwa kwa kipindi kirefu sana.

Inabidi TRA wachunguze kama hao "wanaomsadia" Makonda wanalipa kodi stahiki kwa biashara zao wanazofanya ama wanatumia "misaada" wanayotoa kwa Makonda kama kichaka chao cha kujificha wasilipe kodi stahiki wanayotakiwa kulipa?

CAG naye achunguze kama kweli fedha za umma ndizo zinatumika kwenye miradi ambayo makonda anaiwezesha kutekelezwa. Hii ni muhimu kwani kwa mujibu wa sheria zetu ofisi ya Mkuu wa mkoa hazina fungu la maendeleo bali Halmashauri zilizo katika mkoa husika.

CAG aangalie kama maafisa maduhuri na masuhuri kwenye Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam na Ofisi ya Mkoa ni wao wanaoidhinsha matumizi ya fedha hizo ama kazi yao ni kuandika tu taarifa baada ya fedha kutumika.

TAKUKURU nao wachunguze kama misaada inayotolewa kwa Makonda haina dalili ya kirushwa. Maana fedha zinazotolewa kibinafsi zinakujaje kufanya kazi za umma kama huyu mtoaji hana dalili za kutoa rushwa. Ni kwa nini hao watoa "misaada" wasiitoe kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam badala yake wanaikabidhi kwa Makonda binafsi na si kama Mkuu wa Mkoa?
We kakuchunguza nan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanafikiri Makonda anatoa hela mfukoni mwake...makondo ni mpiga debe tu.
Kila zama zina wenyewe .
Nashanga sijui kwanini hatafutwi,yaani ana mali kibao,anatumia magari ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya,yet anatoa mapesa na vitu kibao pesa anatoa wapi ya hayo yote???
Hata kama kuna ubabe awamu hii, je ni kweli kuwa halmashauri ya jiji haina la kufanya?, kuwa na ma meya kwenye majiji makubwa kumewapa upinzani advantage gani?, najua hawawezi kusimama jukwaani na kupinga vitu vya maendeleo, lakini at least wanajua wana nguvu gani?, when to play which card etc...?
 
Wale Watu alienda nao kwenye mawingu kuna Mkuu yeyote wa mkoa umewahi kuona anao; waacha alale maisha kwenye nchi ya kikundi cha Watu!!
 
baadhi ya vyanzo vinajulikana mkuu, kama ujenzi wa makao makuu ya bakwata unaoendelea ni GSM ndo wanagharamia bila kukosea mfalme wa morroco nae alitoa ahadi ya ujenzi wa msikiti pale, pia kuna akina azim dewji siku za karibuni nao wanatoa misaada ni. kidogo huu utaratibu sasa hivi hatujauzoea wa viongozi kudeal na matatizo ya wananchi wao rather than their stomach, tutazoea and its party of social responsbility kwa makampuni na watoaji wa misaada hiyo. let us build our mother land regardless of our differences. big up MAKONDA
 
Umesahau alichofanywa Nape baada ya kumchunguza huyo Bashite a.k.a Maliyamungu???
 
M najiulizaga office yake inafanana na office za wakuu wa mikoa mingine au?maana hata mshahara nasikia ni sawa kwa wote so hata ubora wa office zao lazma uwe sawa naona yy anavitu vya kutoka nchi mbalimbali humo ndani
 
baadhi ya vyanzo vinajulikana mkuu, kama ujenzi wa makao makuu ya bakwata unaoendelea ni GSM ndo wanagharamia bila kukosea mfalme wa morroco nae alitoa ahadi ya ujenzi wa msikiti pale, pia kuna akina azim dewji siku za karibuni nao wanatoa misaada ni. kidogo huu utaratibu sasa hivi hatujauzoea wa viongozi kudeal na matatizo ya wananchi wao rather than their stomach, tutazoea and its party of social responsbility kwa makampuni na watoaji wa misaada hiyo. let us build our mother land regardless of our differences. big up MAKONDA
Tatizo watu hata mambo ya maendeleo ya wananchi wanaingiza siasa. Sipendi watu wa dizain hii, kama binadam ana mapungufu yake ila kwa mazuri tuyaunge mkono..
 
Kuna tatizo kubwa hapo.Kuna upiga dili wa kufa mtu nyuma ya pazia.
Kuna tetesi kuwa anajenga jumba la ghorofa tatu mwanza.Ana magari ya kifahari.
Swali:Mtumishi wa umma anapata wapi mabilioni ya hela mpaka anafikia kutoa misaada ya mamilioni ukizingatia ugumu wa maisha tulio nao watanzania wengi?
 
Back
Top Bottom