Kwanini CAG, TRA na TAKUKURU Wasimchunguze Makonda?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,283
33,889
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (Daudi Bashite?) ni miongoni mwa wakuu wa mikoa maarufu sana kwenye serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli. Pamoja na mambo mengine ni mtu anayaonekana ana dhamira ya kuibadili Dar es salaam kuwa mji wenye maendeleo ya vitu mbali mbali.

Makonda anatoa hela na ahadi kwenye miradi mbali mbali wakati mwingine ahadi zake zinafikia hadi mabilioni ya shilingi. Inasemwa kwamba alipoingia tu Ofisini kama Mkuu wa Mkoa alibadili kabisa muonekano wa ofisi ile tofauti na ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Mzee Meck sadiq.

Kuleta maendeleo si jambo baya lakini kama kiongozi wa umma ni lazima hela za kuleta hayo maendeleo vyanzo vyake vifahamike na viwe safi na kusiwe na muingiliano wa kimaslahi kati ya hao watoa hela na nafasi aliyo nayo kisiasa.

Ahadi kama kusaidia kujenga jengo la BAKWATA ni ahadi kubwa sana na kama Makonda ataitekeleza basi inabidi aeleze hela za kutekeleza ahadi hiyo kaitoa wapi. Juzi tumeambiwa yeye mwenyewe kwa "juhudi zake" amefanikisha kukarabati magari kadhaa ya Polisi yaliyokuwa yameshindikana kukarabatiwa kwa kipindi kirefu sana.

Inabidi TRA wachunguze kama hao "wanaomsadia" Makonda wanalipa kodi stahiki kwa biashara zao wanazofanya ama wanatumia "misaada" wanayotoa kwa Makonda kama kichaka chao cha kujificha wasilipe kodi stahiki wanayotakiwa kulipa?

CAG naye achunguze kama kweli fedha za umma ndizo zinatumika kwenye miradi ambayo makonda anawezesha kutekelezwa kwake. Hii ni muhimu kwani kwa mujibu wa sheria zetu ofisi za Wakuu wa mkoa hazina fungu la maendeleo bali Halmashauri zilizo katika mkoa husika.

CAG aangalie kama maafisa maduhuri na masuhuri kwenye Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam na Ofisi ya Mkoa ni wao wanaoidhinsha matumizi ya fedha hizo ama kazi yao ni kuandika tu taarifa baada ya fedha kutumika.

TAKUKURU nao wachunguze kama misaada inayotolewa kwa Makonda haina dalili ya kirushwa. Maana fedha zinazotolewa kibinafsi zinakujaje kufanya kazi za umma kama huyu mtoaji hana dalili za kutoa rushwa. Ni kwa nini hao watoa "misaada" wasiitoe kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam badala yake wanaikabidhi kwa Makonda binafsi na si kama Mkuu wa Mkoa?
 
Wewe jamaa una nia ovu kwa sisi watumishi hususani viongozi wa hizo taasisi ulizotaja!

Yaani unataka tumchunguze right hand man wa Mkulu wa Kaya!

Hivi huoni unatuambia tuchunguze watu ambao tutakuta source ya hayo yote ni kule kule?!
 
kama mtu anakutuma kufanya umafia kwa nini akunyime hela..
una vyeti feki unaambiwa piga kazi..
unavamia unaambiwa upo kazini..
unateka unaambiwa mchapa kazi..
bashite alipaswa kuwa gerezani..
si kupewa nafasi ya kujitoa kimasomaso kwa kutoa ofa za hapa na pale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom