Kwanini BoT wasiprint pesa nyingi ili Serikali ifanyie mambo yake?

mtafiti muelewa

Senior Member
Oct 16, 2013
186
98
Habari wana jamvi?
Natumai mu wazima wa afya.

Leo nina swali ambalo naamini likijibiwa hapa nitakuwa nimefumbuliwa macho ya fikra, pia watu wengi watakuwa wamefumbuliwa.

Swali: Ni vigezo gani huwa vinaangaliwa mpaka Serikali inaprintiwa pesa?

Kwa nini wasprint nyingi tukalipa madeni ya nje, tukakamilisha miradi mikubwa ya maendeleo, tukanunua madawa ya hospital na vyote ambavyo tunapungukiwa kama nchi?

Wanauchumi karibuni mtupe ABCs za hili jambo ili tupate kujifunza.
 
Tricky question.

In a layman explanation.

Once upon a time we had barter trade. Trading by exchanging things by things on hands. Now what if I have 1 cow and i want to trade this 1 cow for only 1 goat. Since 1 cow and 1 goat aren't worth the same. Cow worth's higher than goat. So I need 1 goat and remaining value of my cow i.e the change. I don't want anything, I just want a goat and the remaining value. How would I be paid?

In early days if you had much golds you're a rich. So gold didn't solve the scenario above of barter trade.
The idea of money came in our heads. What we need is something that will trade things at different values and the remaining changes, hence making life simple. Just a single paper in pocket worth cows, car and a house.

How would the first money worth? Well do we have something very rarely and highly valued than other things? Yes it's Gold.

How do we value a single paper per gold?
Just make $ 1 paper per 1 milligramme of gold (just an example, not really how it works). That means 100 mg of gold and you have $100 in pockets.

You seeeeeeee!

If a cow worth $3, it would need me 3 mg of golds, now I'll give only $3 of paper money instead of golds and get my changes back.

Printing bunch of paper $ thinking you'll wake-up a rich is a dumb idea, it doesn't mostly work. Zimbabwe and Venezuela tried and failed.

Imagine a country prints trillions of paper $ and procure to every citizen in the country. Now everybody has $1000 in their pockets without sweat, I mean easily you get $ without production!. All of people need is rice to survive. It used to cost $1 for 1 kg of rice. Everyone has money now everyone will need to buy tonnes of rice and put them at their homes. Rice will be scarce in the market. Demand of rice will rise and hence firms and farmers will need to hire workers to work harder and produce more rices. Workers will demand high wages. And hence firms won't stand longer paying higher wages to rice producers. Now firms will consider raising the price of 1 kg of rice to $ 10. It's a hide and seek game😀😀.

Value of the currency drops (PPP). I mean PPP of rice in China may be is $0.5 but yours is $10.

You wanna buy rice in China by your currency you'll need 10/0.5 = 20 PPP of your currency. 😅

As long as your government continue printing more moneys without considering its gold reserve, imports and exports its economy will crush.

Economy of the country grows by making things, selling them and of course the currency's value is determined by gold reserves. Gold is rarely and valued thing you know.
 
Ukiprint hela nyingi:
1. Utasababisha mfumuko wa bei.
2. Pesa yako itapungua thamani.
3. Dunia itapoteza imani na pesa yako.
4. Utakuwa umefanikiwa kuua uchumi wa nchi yako.

Zimbabwe walijaribu hii kitu.
file-20181217-185255-1g29p8.jpg
 
Ukiprint hela nyingi:
1. Utasababisha mfumuko wa bei.
2. Pesa yako itapungua thamani.
3. Dunia itapoteza imani na pesa yako.
4. Utakuwa umefanikiwa kuua uchumi wa nchi yako.

Zimbabwe walijaribu hii kitu.
View attachment 1622051
Rejea swali mzee, ni vigezo gani huwa vinaangaliwa vinavyopelekea serikali iprint pesa?
Tunashukuru umetupa athari za kuprint pesa bila kufuata utaratibu.
 
Habari wana jamvi?
Natumai mu wazima wa afya.

Leo nina swali ambalo naamini likijibiwa hapa nitakuwa nimefumbuliwa macho ya fikra, pia watu wengi watakuwa wamefumbuliwa.

Swali: Ni vigezo gani huwa vinaangaliwa mpaka serikali inaprintiwa pesa?

Kwa nini wasprint nyingi tukalipa madeni ya nje, tukakamilisha miradi mikubwa ya maendeleo, tukanunua madawa na vyote ambavyo tunapungukiwa kama nchi?

Wanauchumi karibuni mtupe a,b,c za hili jambo ili tupate kujifunza.
Itatokeabonge la inflation kiasi kwamba tutaanza kununua mkate hata kwa laki. Pesa haiprintiwi hivi hivi inakuwa backed na shughuli za kiuchumi na demand.
 
Rejea swali mzee, ni vigezo gani huwa vinaangaliwa vinavyopelekea serikali iprint pesa?
Tunashukuru umetupa athari za kuprint pesa bila kufuata utaratibu.
Inabidi pesainayo printiwa iendane na uzalishaji na shughuli za kiuchumi otherwise uchumi utaanguka. Pia mahitaji ya pesa kweney mzunguko
 
Tunalipa kwa kutumia foreging currency mkuu siyo kwa pesa yetu ya madafu
Kwani si tunanunua foreign currency kwani tuna print, tukinunua nani anabaki na foreign currency na nani anabaki na pesa zetu baada ya kununua foreign currency
 
Kwani si tunanunua foreign currency kwani tuna print, tukinunua nani anabaki na foreign currency na nani anabaki na pesa zetu baada ya kununua foreign currency
Shughuli za kiuchumindizo zinaleta foreign currency kwenye nchi, mfano wakija watalii tukiuza mazao nje kama korosho, tunalipwa kwa dollar, lakini wakulima wanapewa ela yao kwa pesa ya madafu inamaana. Pia serikali inaweza kuissue bonds in foregin currency.
 
Shughuli za kiuchumindizo zinaleta foreign currency kwenye nchi, mfano wakija watalii tukiuza mazao nje kama korosho, tunalipwa kwa dollar, lakini wakulima wanapewa ela yao kwa pesa ya madafu inamaana. Pia serikali inaweza kuissue bonds in foregin currency.
Kwani bidhaa zikiuzwa nje ya nchi watu wanalipwa wananunua bidhaa nyingine kula wanaleta huku iyo pesa itakuwaje huku sasa, tuseme pesa tunayoipata ni ya watalii kuja tu na makampuni yanayouza bidhaa nje ya nchi halafu wanalipwa dola kuja kwenye akaunti yetu huku.
 
kwani bidhaa zikiuzwa nje ya nchi watu wanalipwa wananunua bidhaa nyingine kula wanaleta huku iyo pesa itakuwaje huku sasa, tuseme pesa tunayoipata ni ya watalii kuja tu na makampuni yanayouza bidhaa nje ya nchi halafu wanalipwa dola kuja kwenye akaunti yetu huku
Labda nikupe mfano... mfano mimi kazi ninazozifanya nalipwa kwa dollar. Ina mana nimefanya kazi, mzungu ananilipa assume dollar 500 ambayo kwa tshs ni kama 1.2 mils, anafanya wire transfer inafika bank local bank wanapokea dollar ila mimi kwenye my account wanaweka tshs: ambayo 1.2 mls. wao dollar wanabaki nazo na mwisho zitaenda BOT maana wana kiasi cha pesa ya kigeni wanachoruhusiwa kuwa nacho kikizidi wanapeleka BOT.

Hay assume umeuza kitu nje viatu vya kimasai, umeuza mzigo wa dollar 1000, mnunuzi kalipa, lakini wewe kwenye account utawekewa Tshs. Hapo unaona kupitia shughuli zetu za kiuchumi serikali inapata pesa pia. Kuna kuuza madini pia yanauzwa kwa foreign currency. Hata Kahawa na kadhalika.

Siyo kila anayeuza bidhaa nje akilipwa ananunua kitu analeta huku. Na ndiyo maana uchumi illi ufanye vizuri export inabidi iwe kubwa kuliko import, ikiwa na maana tunaingiza pesa ya kigeni nyingi kuliko tunayotoa.
 
Back
Top Bottom