Kwanini bei ya mafuta Haishuki Tanzania?

Geeky

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
307
Reaction score
181
Hivi kwanini bei ya gas kwa ujumla ikiwemo petrol haishuki Tanzania ihali ktk soko la dunia imeshuka sana?

As of :

5th Jan 2014
Oil prices have fallen to $50 a barrel
According to Bloomberg.

Bloomberg.com
 
Hivi kwanini bei ya gas kwa ujumla ikiwemo petrol haishuki Tanzania ihali ktk soko la dunia imeshuka or should we say 'the bulk procurement contracts had no futures clauses. I think this is also a ticking time bomb' . Napita tu #uwajibikaji
Kabla ya kutoa conclusion, awali ya yote tunatakiwa kuangalia trend na kufahamu bei ya mafuta ilianza kushuka lini na kwa upande mwingine tuangalie mzigo wa mwisho Tanzania ulikuja lini. Ikiwa bei, say imeanza kushuka two weeks ago wakati mzigo ulio sokoni umeingia kabla ya hapo then there's no way bei itashuka... mafuta sio kama maharage ya Mbeya kwamba, ukishasikia bei ya maharage imeshuka, siku hiyo hiyo unaweza kwenda na kesho kurudi na mzigo wa bei ya chini.
 
Hivi kwanini bei ya gas kwa ujumla ikiwemo petrol haishuki Tanzania ihali ktk soko la dunia imeshuka or should we say 'the bulk procurement contracts had no futures clauses' . I think this is also a ticking time bomb . Napita tu. Tunataka #uwajibikaji

Delivery ina matter sana katika bei za mafuta.

Mzigo unaoshushwa leo utakuta ulipakiwa na kununuliwa kabla bei hazijashuka.

Lakini tumeona toka kuanzishwa mfumo huu bei zikipanda na kushuka. Tutegemee bei za miezi miwili au mitatu ijayo kuwa zitakuwa na unafuu.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Kabla ya kutoa conclusion, awali ya yote tunatakiwa kuangalia trend na kufahamu bei ya mafuta ilianza kushuka lini na kwa upande mwingine tuangalie mzigo wa mwisho Tanzania ulikuja lini. Ikiwa bei, say imeanza kushuka two weeks ago wakati mzigo ulio sokoni umeingia kabla ya hapo then there's no way bei itashuka... mafuta sio kama maharage ya Mbeya kwamba, ukishasikia bei ya maharage imeshuka, siku hiyo hiyo unaweza kwenda na kesho kurudi na mzigo wa bei ya chini.

Katika commodity trading kuna futures contracts and this goes both ways kwa mlaji na muuzaji kama marekani na nchi lukuki bei imeshuka kureflect reality then huu hapa kwetu ni wizi hasa ukizingatia umuhimu wa bidhaa yenyewe ktk uchumi. They must allow free interprise in this venture I am strongly opposed to bulk procurement contracts
 
Delivery ina matter sana katika bei za mafuta.

Mzigo unaoshushwa leo utakuta ulipakiwa na kununuliwa kabla bei hazijashuka.

Lakini tumeona toka kuanzishwa mfumo huu bei zikipanda na kushuka. Tutegemee bei za miezi miwili au mitatu ijayo kuwa zitakuwa na unafuu.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Kweli FaizaFoxy ila transparency hakuna na hawa jamaa si wenzetu si unakumbuka walivyoigomea ewura
 
mbona mimi huku nlipo.imeshuka kama week 3 au mbili nyuma.
nakumbuka nlikuwa nanunua 2482/litre ila sasa hivi ni 2120.
 
Kaka mkubwa ktk soko la dunia bei imeshuka hadi viwango vya miaka 10 iliyopita sasa crude ni $70 kwa pipa toka mia na ushee.
 
Mbona ikipanda leo na kesho wanapandisha hawa subiri mzigo uliopo ndo uishe?
Hii mchi huwa haina mwenye uchungu na mwananchi
 
Naam nakumbuka na sababu zao ilikuwa, walikuwa bado wana mafuta waliyoyanunuwa bei ya juu.

Kuhusu "transparency" sijakuelewa kwani najuwa ukipitia website ya ewura vingi viko wazi.

Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA)

Yep ninachomaanisha ni kwamba wao tunawasikia tu pale magazeti yakiwachokoza na bei zikipanda they should be pro active. Tbs wanachoma bidhaa wazi hadharani tunawaona, tcra kila leo wako na sisi ila hawa jamaa wako passive sana sijaona petrol stations zikifuatiliwa, au sio mamlaka hii. Price ikishuka 40-60% mie nina uhakika ingekua news na nafuu sana kwa raia.
 
Katika commodity trading kuna futures contracts and this goes both ways kwa mlaji na muuzaji kama marekani na nchi lukuki bei imeshuka kureflect reality then huu hapa kwetu ni wizi hasa ukizingatia umuhimu wa bidhaa yenyewe ktk uchumi. They must allow free interprise in this venture I am strongly opposed to bulk procurement contracts
Future contract sawa lakini kwenye suala hili doesn't apply... lazima tuangalie mzigo uliopo ni wa lini. Na ikiwa mathalani mzigo umeingia leo, maana ak ni kwamba umekuwa procured zaidi ya mwezi mmoja uliopita under old pricing lakini linapokuja suala la ku-control bei bulk procurement inakuwa ni rahisi sana ku-monitor bei kuliko uagizaji wa mtu mmoja mmoja! Kama utakumbuka, zamani ilikuwa EWURA wakitangaza bei mpya ya mafuta (kwa maana bei ya chini) kutokana na kushuka bei ya mafuta soko la dunia, baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wanakahidi na kusema wao walinunua kabla bei haijashuka na ku-confirm na hadi ukapitie mafaili lakini kwa sasa hakuna wa kusema hivyo coz' mzigo unaotumiwa na X ndio ule ule unaotumiwa na Y!
 
Bei ya mafuta ya petrol imeshuka sana leo lita moja ya mafuta hayo inauzwa Tsh 1909
 
Nakubaliana na wewe ila ktk futures trading kuna bima hata ya futures derivative products, kama serekali imeweza kuanzisha bima ya Amana kwa wateja wa mabenki hadi billion tano kwanini isitoe guarantee kwa hawa watu kama ndiyo shida yao kwa sababu (ironically, inaonesha hawataki risk). Ni part mbili zinakubaliana tu. Au ikishindikana wafanye huria. Free interprise ndilo jibu.
 
Wapi dar au mikoani? Hapa tanga wanauza 2,300/lita
 
Hiyo ni Temporary kwa masaa tuu ! kesho bei itapaa juu!! Utaona au kusikia.... BongoTZ hii!
 
Ukiona hivyo mafisadi wameanza kunyofoa mirija yao.

yatazidi kushuka. Ishu ya Escrow imesaidia kuwatetemesha wapiga dili.
 
Bei ya mafuta ya petrol imeshuka sana leo lita moja ya mafuta hayo inauzwa Tsh 1909

Mbona imeshuka kidogo sana?? Wakati bei ya pipa moja katika soko la dunia imeshuka toka $68 had $40.
 
Back
Top Bottom