Kwanini bei ya mafuta Haishuki Tanzania?

Kwanini bei ya mafuta Haishuki Tanzania?

PESA ya kufanyia kampeni zetu ccm unafikiri tutapata wapi.na wahisan ndio hao washakimbia.
 
Hii ndo Bongo danganyika zaidi ya unavyoijua, subiri siku wasikie mafuta yamepanda bei kwenye soko la dunia kama siyo siku ya pili bei juu, juu zaidi!
 
1) Bei ya mafuta imekuwa ikiporomoka kwa kasi katika soko la dunia .. USA imefikia.mpaka wastani wa $800+ per litre toka $1600+ per litre ... je bei hii nayo imeshuka kwa kasi hiyo hiyo katika soko la tanzania?

2) Je, prof. Tibaijuka katoswa ili mwakani CCM wakisema ni zamu ya wanawake mama Migiro ndio pekee aonekane anafaa?
 
1) Bei ya mafuta imekuwa ikiporomoka kwa kasi katika soko la dunia .. USA imefikia.mpaka wastani wa $800+ per litre toka $1600+ per litre ... je bei hii nayo imeshuka kwa kasi hiyo hiyo katika soko la tanzania?

2) Je, prof. Tibaijuka katoswa ili mwakani CCM wakisema ni zamu ya wanawake mama Migiro ndio pekee aonekane anafaa?

Duh.... liter moja ya mafuta USA ni USD 800 mbona ni ghali sana ukiconvert kwa pesa ya madafu. Hebu icheck vizuri mdau.
 
Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa. Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40% haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta ikiwemo wenye daladala na kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua. Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli, bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.
EWURA,inasemekana, wamesema kuwa bei za hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu waagizaji huagiza kwa ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo la bei. Hata hivyo bei zimeanza kushuka toka mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa wananchi. Ingekuwa bei ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na sababu za kununua ' bulky' huwa hazitolewi.
Ni kweli kwamba Tanzania hununua mafuta yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo. Lakini hao wasafishaji hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo ni dhahiri lazima bei za pampu zipungue. Vile vile ni kweli kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi hawawezi kuona unafuu wa bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za kigeni na kuuzwa kwa Sarafu yetu. Hata hivyo kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta ni 40% wakati shilingi imeshuka kwa chini ya 10%. Katika hali ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.
Ni dhahiri mamlaka za nchi na hasa EWURA wanapaswa kueleza kwa umma ni Kwanini bei za mafuta hazishuki kulingana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia. Wananchi wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo basi bei hizo zishuke na wananchi wafaidike na punguzo hilo.
 
Back
Top Bottom