Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,675
- 40,929
Kitendo cha Waziri wa Fedha kukiri kwamba akiba ya Taifa ya Fedha za kigeni ilichotwa na fedha kutumika kwa ujenzi wa Madarasa ni kiashiria cha dhahiri kukosekana fedha katika njia za kawaida (makusanyo ya mapato).
Foreign Reserve hutumika tu endapo kuna mkwamo wa kiuchumi na serikali huzitumia fedha hizo katika manunuzi ya bidhaa na gharama nyinginezo pindi inapobidi kufanyika hivyo.
Hivyo matumizi yake ni kwa dharura tu na SI VINGINEVYO.
Kuchota akiba inamaana kwamba hatuna fedha na tumeshindwa kukusanya mapato ipasavyo.
Kama tumeshaanza kuigusa akiba yetu haraka namna hii nini mustakabali wa Taifa hili kwa kuzingatia kwamba bado tunaendelea kukopa na bado kuna miradi mingi ya kimkakati ya kutekeleza.
Ni kwa namna gani tunaweza rejesha fedha tulizochukua katika akiba?
Je kuchota akiba ya Taifa was the only available solution??
Mimi naona kama vile kuna jambo ambalo tunafichwa kuhusiana na hali yetu ya kifedha ila sio siri tena maana hata huko mtaani kuna uhaba wa fedha za kigeni ukijaribu kununua unaambiwa hazipo , ila ukichange wanapokea.
Kwakua kuna mkwamo na Baraza la Mawaziri limeshindwa kumshauri Rais ili kuhakikisha ukali wa maisha unapungua.
Nashauri Baraza hili livunjwe.
Rais asiangalie majina aangalie matokeo ya hao wanaopewa majukumu.
Hii nchi ni yetu sote, kuendelea kubebena wakati tunaingia shimoni sio jambo sahihi.
Hapa ili tupone kuna watu inabidi waachie nafasi zao, wapishe wengine.