Mkuu huu mjadala ulishaongelewa sana humu pamoja na kwenye mkutano mkuu wa wamiliki wa vyombo vya usafirishaji Dsm.
Majibu yaliishawekwa wazi, kwamba askari wa kada yoyote Dsm atapanda bure akiwa amevaa kikazi, isipokuwa akiwa kwenye nguo za nyumbani atatozwa, mbona utaratibu huo upo tangu enzi za Mwinyi?
Hoja hii imekuwa ikifukuta kama volcano. Inaripuka na kusinyaa na maisha yanaendelea.
Hoja hii hata ingelifikishwa kwa Magufuli, utapata jibu 'simple' sana na utashindwa kuamini masikio yako.
Wenzetu hao wana sacrifice sana maisa yao kwa ajili yetu sisi raia.
Wana magari yao kweli, lakini kwa mazingira ya Dar ni vigumu kuwakidhi.
Acha tu wapande bure, maana hakuna namna.