Kwanini ameshtakiwa Max badala ya kushtakiwa kampuni?

Kwanini ameshtakiwa Max badala ya kushtakiwa kampuni?

[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#bringbackbenalive[/HASHTAG]
[HASHTAG]#justiceforlema[/HASHTAG]
 
Ukiangalia coments nyingi humu ndani zinaonyesha ni vipi mnaumia juu ya hari ya nchi ilivo kwasasa,

Kama kweli mmechoshwa andamaneni labda mambo yatabadirika bila hivo nothing will change,,,
 
Na viongozi wa cabinet wako humu wanashindana kutoa ufafanuzi,.
 
At times, the law requires that a veil of incorporation to be lifted so as to prosecute individual persons rather than a company. For media cases, instead of a journalist its an editor who is prosecuted.
Kodofan nadhani hii ni sheria ya zamani kwa hii mpya ya 2016 wana deal na Journalist husika nadhani,I stand to be corrected
 
Ukiangalia coments nyingi humu ndani zinaonyesha ni vipi mnaumia juu ya hari ya nchi ilivo kwasasa,

Kama kweli mmechoshwa andamaneni labda mambo yatabadirika bila hivo nothing will change,,,
Yaani wewe huumii na hii hali? Halafu unawaambia akina nani waandamane? Wewe unafurahia yanayotokea?
 
Wanajua kuishitaki kampuni kwakuwa ipo kisheria hawawezi kuishinda so wana dill na vitisho kwa mtu mmoja mmoja.
 
Inasikitisha sana, sidhani kuwa kweli haya mambo ya kukamata kamata.... ndo' msingi wa shughuli za kiserikali kama taifa ili liendelee mbele, na kuwa nchi ya viwanda.... rather than hali tete ya chakula, maji, mikopo ya wanafunzi vyuo vikuu, pembejeo za wakulima, madai ya wafanyakazi etc.
 
At times, the law requires that a veil of incorporation to be lifted so as to prosecute individual persons rather than a company. For media cases, instead of a journalist its an editor who is prosecuted.

ongea kiswahili mzee hatukuelewi
 
Ukiangalia coments nyingi humu ndani zinaonyesha ni vipi mnaumia juu ya hari ya nchi ilivo kwasasa,

Kama kweli mmechoshwa andamaneni labda mambo yatabadirika bila hivo nothing will change,,,

Nchi yetu uwoga tuliopandikizwa hakuna anayeweza kuandamana, wakiona kirungu cha polisi na vimaji vyenye pilipili hoho wanatoka mbio utaona miguu inagusa mgongo!
 
Habari wanajamvi!

Binafsi ni msomaji mzuri ila ni mchangiaji finyu wa mada za humu majukwaani, lakini hichi kimachoendelea kuhusu Max, co-founder wa huu mtandao maridhawa na unaohitajika sana nasi, kwa kweli imeniumiza sana, sina budi kushiriki mtazamo wangu na kuomba kueleweshwa zaidi.

Mimi sio mwanasheria, ila wanasheria na wajuvi wa mambo hayo mtanisaidia kwenye hili. Minavyofahamu kwa elimu yangu ndogo niliyonayo ni kwamba kampuni (mfano jamii media imayomiliki mtandao huu jf) kama entity huwa ni kama mtu yani kampuni yenyewe ni artificial being ambayo huzaliwa kisheria inapewa jina kisheria inaishi na kifanya shughuli zake kisheria na inaweza kufa kisheria, hivyo basi ikikosea kisheria pia kampuni hushitakiwa kisheria ndio maana kwenye makampuni kuna legal officers

Sasa swali langu kwa nini hii issue inaonekana kuwa ya personal sana mpaka anashitakiwa Max badala ya Jamii Media company?

Sina details sana, lakini mtakubaliana na mimi kwamba Microsoft ikikosea na ikashitakiwa huwezi ona Bill gates ndio anakamtwa na kiwekwa lumande, au mfano ile dispute ya Apple na Samsung, sikuona mtu anawekwa rumamde pale, ila wanasheria tu ndio wanabishana vizimbani.

Kwa nini Max amekamtwa na kushatikiwa, hata charges za kuizia sijui polisi kifanya upelelezi kwa kanini kapewa yeye badala hizo charges ziende kwa kampuni? Yes he is one of founders does that mean jf is his personal blog? And not owned by a Jamii Media company?

Nisaidieni wadau kielewa hili...

Na kweli, serikali iwe na utu na icheze karata zake smart... Kinachoendelea sio fair kwa max, sio fair kwa watuamiaji wa mitandao, sio fair kwa watanzania, na sio fair kwa taifa zima.
[HASHTAG]#freemax[/HASHTAG]
Hiyo inaitwa the corporate veil ambapo kwenye kesi za madai (civil), kampuni inasimama kama kampuni. Lakini kwenye kesi za jinai, (criminal), mmiliki /mtendaji mkuu ndie anashitakiwa. Kampuni haiwezi kufungwa jela. Ila pía kumshitaki mmiliki kwa niaba ya kampuni kunahitajika mahakama ndio itoe kibali cha ku unveil ile corporate veil. Wanasheria wakicheza vizuri hakuna kesi yoyote hapo ni kusumbuana na kuoneana tuu.

Paskali
 
Mbona kama unaonekana kama sheria unaijua. Lakini sio ishu ngoja waje watueleze wajuzi wa sheria
 
Back
Top Bottom