Why was Albert Einstein a genius?
Jibu ni moja tu. Alikuwa mbunifu.
Einstein hakuwa anajua hesabu kama Sir Isaac Newton au wanasayansi wengine. Ndio, alikuwa anajua hesabu kiasi chake lakini angekuwa anategemea tu ujuzi wake wa hesabu kuna uwezekano mkubwa sana tusingekaa kulisikia hili jina la Einstein.
Einstein is synonymous with genius.
Kuna mnao uliza je Einstein ana impact gani kuliko Newton? Ana nini kipya?
Niseme tu kwa ufupi kwamba Dunia yetu hii ya sasa na namna tunavyoishi na namna tutakavyoishi hata miaka 1000 ijayo ni kwasababu ya mawazo na fikra zake. Hakubuni chochote moja kwa moja lakini waliobuni walimtumia sana Einstein. Bila yeye tusingekuwa na internet connection, smartphones, satellites, computers, etc.
Na bado hatujamaliza kumtumia. Quantum mechanics, space travel, colonization of the galaxy, discovery of other dimensions, etc.
Kwa ufupi Einstein ni moja kati ya msingi wa binadamu hasa huko tunapoenda.
Newton ni moja kati ya watu waliosaidia sana tukafika hapa, Einstein ni moja kati ya watu watakao tusaidia kwenda mbele.
Hivyo basi kwanini Einstein alikuwa genius? Aliweza kuufikirisha ubongo na kuwaza namna gani mwanga, sayari na spacetime zinavyo behave ili kuufanya ulimwengu uwe kama ulivyo. Alikuja na mawazo ambayo watu hawakuamini na ya kushangaza kabisa. Walihisi ni kama uchawi, na bado tuna hisi ni uchawi kwasababu kwa jinsi binadamu tulivyo hatuwezi kuelewa kiurahisi haya mambo. But each and every time he has always been proven right.
And this is why Einstein was a genius.