Kwanini ajira hakuna?

Kwanini ajira hakuna?

Ajira ni zoezi endelevu,kwa sababu kuna watumishi wanastahafu kwa mujibu wa sheria kuna wanaofukuzwa,wapo wanaofariki kuna wanaohamua kuacha kazi wenyewe nk.
Kama hakuna ajira kwa visingizio vyoyote vile ni janga kwa taifa,kwa sababu wale wanaoondoka kwenye ajira hawapati watumishi wapya wakuelekeza kazi zinavyofanyika.
Lakini pia hospitalit zinakosa madaktari shule zinakosa walimu wataalamu wa kilimo mifugo nk hawajiriwi,matokeo yake wagonjwa na wanafunzi wanakosa huduma na kila kukicha pengo la ajira linazidi kuongezeka.
Tuliaminishwa kuwa baada ya uhakiki wa watumishi hewa ajira zitaanza lakini kumbe ilikuwa ni uongo.
 
Huku ni ukakamavu tuu siku hzi no job........Asante sana jiwe hatutokusahau kwa hillView attachment 1163317
FB_IMG_1563667486399.jpeg
 
na kwanza kuna haja gani ya mtu kusoma sheria kwa miaka 18 halafu leo hii aende akajiajiri shambani ambako hakuna uhusiano wowote na taaluma yake ya sheria?
Kama wewe nawe ni msomi na una mawazo ya kizembe kama haya basi taifa limepata hasara. Aliyekuambia MTU akisoma basi hapaswi kulima ni nani? Kwa akili yako hii utasugua masufuria kwa shemeji yako mpk uzeeke.
 
Kubwa jinga wewe.. nimeuliza kuna uhusiano gani wowote wa lazima kati ya hicho kilimo unachokipigia debe na taaluma ya sheria kiasi cha kunitaka mimi niende shambani mara tu nimalizapo masomo?

Na kwanini serikali itumie rasilimali nyingi kunipa elimu halafu baadae inanitelekeza kwa kuniacha niende kutumia elimu yangu mahali isikohitajika hata kidogo?

Kwa unavyojibu watu humu wewe ndio unaonekana wazi unaishi kwa dada yako na umeridhika, hata hapo umevimbiwa ugali wa shemeji.. punguani wahed wewe
 
niende kutumia elimu yangu mahali isikohitajika hata kidogo?
Hivi wewe ulisoma ama umehudhuria darasami tu? Sheria haihitajiki kwenye kilimo? Historia, sayansi ya siasa, ustawi was jamii havihitajiki kwenye kilimo?

Elimu yoyote ile lengo lake ni kumjengea uwezo mwanadamu kuzikabili changamoto zinazomzunguka ktk mazingira take. Sasa kama wewe umesoma halafu unalilia ajira basi hujaelimika.
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.

Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila amaemaliza chuo anapata ajira.....kujiajiri ni utashi wa mtu....ndo maana unaona nchi zilizoendelea zinakua na statistics za employment!
 
mwambie atatatua migogoro ya mashamba as a lawyer..lol

Kwa nini usome law walati unaona kama unataka kujiajiri kuna sehemu tatu,biashara,kilimo na teknolojia...

nakubaliana na yeye though,elimu yetu haimuandai mtu kuexplore his environment for opportunities..
 
Ebo, flyover, barabara, shule, mavituo ya afya ukusanyaji bora wa mapato, wezi na majipu kutumbuliwa, uchumi kukuwa, viwanda kede kede halafu unalalamika hakuna ajira? Wewe sasa naona unataka kuhujumu maendeleo tunayoyapata.
My take: Innovate Innovate Innovate. Serikali sio muajiri hata kama ana waajiriwa.

Yale ya juu ni yale ambayo tunaamini kuwa yanaleta ajira. Ni vibarua.
 
Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila amaemaliza chuo anapata ajira.....kujiajiri ni utashi wa mtu....ndo maana unaona nchi zilizoendelea zinakua na statistics za employment!

Ni dhambi au dhihaki kumdanganya mwenzio. Sio wajibu wa Serikali. Serikali ina tengeneza sera kuwezesha watu kujiajiri na kuajiriwa kama na mie sijadanganya hapa basi, tuendelee...tunabanana na kupambana humu humu... statistics nini bana, kazi hamna basi ndio hivyo, hamna.
Hizo nchi zilioendelea, Serikali zimetengeneza kama insurance kwa wale amabao wanakosa ajira, na asilimia kubwa ni kwa vibarua tu

Tanzania yetu lazima hili liende kwa utashi, ni kweli na nakubaliana na yeyote anayeamini hivyo.
Hatuwezi kuwa na sera kama za hizo nchi kwani wao wana maendeleo tofauti katika jamii zao, wanatamaduni ambazo kwangu aidha ni duni kwetu, au ziko kinyume na za Kiafrika au hapa Tanzania
Historia ya dunia, inajirudia ama iko pale pale.
Akili ni mali
 
Tatizo la Ajira nchini Tanzania ni Mtambuka sana Mkuu ambapo Wazazi wana lawama zao, Shule na Taasisi za Elimu zina lawama zao, Serikali kupitia Wizara husika na Waziri husika wana lawama zao na Wanafunzi wenyewe nao wana lawama zao vile vile na tena huenda Wanafunzi ndiyo wakabeba lawama nyingi katika hawa Wahusika wote hapa.

Wazazi wengi wanawalazimisha Watoto Wao Kuchukua Kozi wasizoziweza hatimaye wanakwamisha Ndoto zao Kitaaluma.

Shule na Taasisi za Elimu nchini haziwaandai Wanafunzi kuja Kujiajiri wenyewe na Kutengeneza Mitaala ambavyo itakuwa inaakisi Soko la Ajira kwa sasa duniani na badala yake Elimu ya Tanzania bado imekuwa ni ile ile aliyotuachia Mkoloni.

Serikali na Wizara husika hazijatambua kuwa dawa pekee ya Kumaliza hili tatizo ni Kwanza kubadili Sera zake hasa katika Mashirika na Makampuni huku zikiwataka Taasisi za Kbenki nchini kuwa wanatoa Mikopo ya Riba nafuu kwa Vikundi mbalimbali vya Wahitimu ili wakimaliza tu Masomo yao wawaze Kujiajiri na siyo Kuzunguka hovyo Mitaani na Bahasha za Kaki pekee. Kipengele cha Uzoefu kiondolewe kwani Mtu Uzoefu haupatii akiwa Jobless bali akiwa Kazini kutoka kwa Wakongwe aliowakuta na ambao wanatarajia Kustaafu.

Wanafunzi wengi wa sasa wa Tanzania hawajui wanataka nini, hawajitambui kabisa na wengi Wao wanasoma kwa Mkumbo na siyo Kusoma ili waje kuwa Tegemeo. Kama Mwanafunzi wa Kidato cha Nne au Sita unamuuliza anataka kuja nani baadae anakujibu hajui au anakutaka Wewe uliyemuuliza hilo Swali umtathmini alivyo kisha umfanyie Kazi ya Marehemu Sheikh Yahya umtabirie asomee nini hapo hakuna tatizo? Wanafunzi wengi ni Wavivu na hawapendi Kujiimarisha Kimaarifa ili waje kuwa Wanataaluma wazuri kwa baadae.

Yangu ni haya tu Mkuu.
Pamoja na yotee uliyoyasema athari ya hayo haikuwa hivi kipindi cha Mkapa na Kikwete huyu alienda mbali zaidi kwa kutoa wafanyakazi hewa na wa vyeti feki na bado anawatupa wasomi wengi mtaani.
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Hivi unajua kuwa kilimo kinahitaji mtaji mkubwa sana.
Sio wote wenye mashamba ya kurithi kama wewe.
Inabidi wanunue,
Ili kilimo kiwe cha kibiashara ni lazima uwekeze vya kutosha.
Mitaji iko wapi?

Tatizo ni kukosa vipao mbele vya kitaifa kwa watanzania .
Kuwekeza kwenye kuwainua watoto wa maskini kwa kuwakopesha mikopo hailipi kwa watawala wanaosaka pesa za kujinufaisha kisasa.
Kuchukua bil. 700 ukanunua Magari ya kifahari ya serikali inalipa zaidi mana kuna 10% inayotolewa na kampuni unapowaunganishia dili kubwa kama hilo.
Tumesahau kuwa watawala ni binadam wasioridhika ,tukaamua kuwaachia kila kitu waamue wao matokeo yake ndio hayo watakimbilia mamiradi makubwa yenye kutoa tenda na usimamizi kwa ndugu na marafiki zao kwa mishahara mikubwa .

Kama Vijana wanaokaa JKT kwa mwaka mmoja wanaweza wakazalisha chakula kingi sana inakuaje hakuna ajira ya maana kwenye kilimo?
Kwa nini wasiwe wanaanzisha mashamba mapya kila mwaka na kuwaachia vijana hao wayaendeshe wenyewe kama mtaji wao huku wakitakiwa kurudisha mtaji wao na kodi kwa serikali ili wengine wapate?

Bila shaka hatuna vipao mbele vinavyowagusa watu wa chini zaidi ya vipao mbele vya kisiasa kwa malengo ya kisiasa na kupiga picha mbele ya kamera.
 
Mpaka Leo vijana wengi wako mitaani na degree zao ,hakuna ajira waalimu hawapandishwi madaraja,

Vijana wa kitanzania leo hii wanaenda jkt kufundishwa ukakamavu..s kwel watu wanaenda kutafuta ajira bt wanakalishwa miaka halafu leo hii wanarudishwa mitaan je wafanye nini huku au mnataka watukabe

Wahitimu wa chuo leo hii hawana thaman..wimbi kuubwa la waalimu wa michepuo ya sanaa hawapew ajira na hata zkitangazwa sijui wanapewa akina nani

Ndugu zangu am not happy cuz ama victim of this chain..
Je tulishawahi kuwekeza kwenye hilo eneo? Au mawazo yetu yote yako kwenye siasa?
 
Wasomi wa Miaka hii Aibu Tupu...
Mtu unakaa na akili zako Huoni Aibu unalalamika Ajira Hakuna hahahaaa

Sasa Kama ww na usomi wako unalalamika Ajira Hakuna Je yule Aliyeishia La Saba atafanyaje...

Na usomi wako unashindwa Hata kulima bustani ya mchicha mtaji ni 20,000/-
Na usomi w@ko unashindwa Kulima Hata nyanya Kwa greenhouse Mtaji wa Laki Moja?
Ila umekaa nyumbani tu kwa baba unalalamika tu hakuna ajira

Sema kwamba ww unasubiri ajira za serikali na wala hushughuliki na Ajira binafsi na Kijiajiri

Pole Sana...

Hakuna serikali ya Namna hiyo Duniani ikawa na uwezo wa Kuajiri wananchi wake wote wanaotaka ajira
Akili yako haiko sawa, sorry
 
Hivi wewe ulisoma ama umehudhuria darasami tu? Sheria haihitajiki kwenye kilimo? Historia, sayansi ya siasa, ustawi was jamii havihitajiki kwenye kilimo?

Elimu yoyote ile lengo lake ni kumjengea uwezo mwanadamu kuzikabili changamoto zinazomzunguka ktk mazingira take. Sasa kama wewe umesoma halafu unalilia ajira basi hujaelimika.

Kwamba mtu asome sheria au utawala wa uma halafu akimaliza hapo aelekee moja kwa moja kulima viazi? hatumie taaluma ya utawala wa uma kukabiliana na changamoto za kilimo cha viazi?

Punguani kabisa wewe. tena usini quote tena
 
Nitaendelea kuku-quote **** wewe. Maana yaelekea na wewe unajiita msomi wakati hujaelimika. Yaani unaona ajabu MTU kumaliza chuo na kwenda kujiajiri kwenye kilimo?!!! Utaendelea kula kwa shemeji yako mpk uzeeke
 
Aiseeeee
Kama wewe nawe ni msomi na una mawazo ya kizembe kama haya basi taifa limepata hasara. Aliyekuambia MTU akisoma basi hapaswi kulima ni nani? Kwa akili yako hii utasugua masufuria kwa shemeji yako mpk uzeeke.
 
Wasomi wa Miaka hii Aibu Tupu...
Mtu unakaa na akili zako Huoni Aibu unalalamika Ajira Hakuna hahahaaa

Sasa Kama ww na usomi wako unalalamika Ajira Hakuna Je yule Aliyeishia La Saba atafanyaje...

Na usomi wako unashindwa Hata kulima bustani ya mchicha mtaji ni 20,000/-
Na usomi w@ko unashindwa Kulima Hata nyanya Kwa greenhouse Mtaji wa Laki Moja?
Ila umekaa nyumbani tu kwa baba unalalamika tu hakuna ajira

Sema kwamba ww unasubiri ajira za serikali na wala hushughuliki na Ajira binafsi na Kijiajiri

Pole Sana...

Hakuna serikali ya Namna hiyo Duniani ikawa na uwezo wa Kuajiri wananchi wake wote wanaotaka ajira
Mkuu ebu ongea kwa ustaarabu..kilimo sio rahisi kama unavyosema..changamoto ni nyingi sana.
 
Back
Top Bottom