Kwanini ajira hakuna?

Kwanini ajira hakuna?

Agriculture is a proven engine for poverty reduction. GDP growth generated by agriculture is more effective in reducing poverty than growth in any other sector. In sub-Saharan Africa, growth in agriculture .reduces poverty up to 11 times faster than growth in other sectors...Kilimo Kwanza ingetutoa..mnakuja na Tanzania ya viwanda..Vijana adui yenu CCM hawataki Vijana matajiri..
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Basi kama ni hivyo, vyuo vyote visitoe degree vianzishe mashamba ili f6 leavers waingie mashambani directly...

Nyambaaaaf
 
Hii dhana ya kuitegemea serikali kama mtengeneza ajira ndio inatufikisha hapa tulipo. Duniani kote sekta binafsi ndio chanzo kikuu cha ajira, kinachotokea tunatengeneza wasomi wasiokuwa na ujuzi wa kuweza kujiajiri na pia hatuna mazingira wezeshi kwa biashara ndogo ndogo kwa ajili ya sheria na sera za ovyo. Tungeanzia hapo.
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Mtu apewi ajira kama dezo..anaomba ajira ili atumie ujuzi alio nao katika kutatua changamoto,alafu unajua hujui kitu isee..yawezekana hufahamu mfumo wa uchumi na uzalishaji.Kama wewe una biashara bila shaka wafanyakazi wako ni masikini unawaonea.
 
Wasomi wa Miaka hii Aibu Tupu...
Mtu unakaa na akili zako Huoni Aibu unalalamika Ajira Hakuna hahahaaa

Sasa Kama ww na usomi wako unalalamika Ajira Hakuna Je yule Aliyeishia La Saba atafanyaje...

Na usomi wako unashindwa Hata kulima bustani ya mchicha mtaji ni 20,000/-
Na usomi w@ko unashindwa Kulima Hata nyanya Kwa greenhouse Mtaji wa Laki Moja?
Ila umekaa nyumbani tu kwa baba unalalamika tu hakuna ajira

Sema kwamba ww unasubiri ajira za serikali na wala hushughuliki na Ajira binafsi na Kijiajiri

Pole Sana...

Hakuna serikali ya Namna hiyo Duniani ikawa na uwezo wa Kuajiri wananchi wake wote wanaotaka ajira
 
Hii dhana ya kuitegemea serikali kama mtengeneza ajira ndio inatufikisha hapa tulipo. Duniani kote sekta binafsi ndio chanzo kikuu cha ajira, kinachotokea tunatengeneza wasomi wasiokuwa na ujuzi wa kuweza kujiajiri na pia hatuna mazingira wezeshi kwa biashara ndogo ndogo kwa ajili ya sheria na sera za ovyo. Tungeanzia hapo.
Tatizo ni mifumo ya Siasa yetu na mipango yetu kuanzia ngazi za familia hadi kitaifa.Hii tunayoita kujiajiri imetengeneza wauza bidhaa wa wengi wadogo wadogo wasio na maana na wanateseka.Yani fikiria mtu anazunguka kwa miguu jiji zima la Dar anauza nguo au mihogo na matunda alafu kesho wanaingia watu kama mia mbili hivi wanafanya kazi hiyo hiyo kwa msingi wa kujiajiri je kuna sululisho hapo au kuongeza shida? kama una akili kali utabaini kuwa ndio maana usiku kuna biashara haramu nyingi zinazotumika kama njia ya kujazia kipato.Tukibadili dira zetu na tukapata watu wenye UWEZO WA KUONA KWA UPANA hizi hali za kustaajabisha zitaisha. Nchi lazima sekta zote ziimarishwe, mifumo ya kukariri jinsi ya kuendesha mambo iondolewe,kufanya mabadiliko kwa kuangalia jirani anafanyaje sio mbinu sahihi kila wakati nadiriki kusema ni uoga wa kufanya uamuzi wetu sisi. Hali itazidi kuwa mbaya muda ai mrefu tasisi za kimataifa zitalazimika kuja kusaidia Kaya.
Serikali ni Baba na Sekta binafsi ndio mama kama hakuna uhusiano hapo maisha hakuna.Inajulikana kuwa ni wajibu wa serikali kusimamia mambo yote ya ajira (kuajiriwa au kujiajiri) haiwezekani watu wa kujiajiri wawe wengi kuliko watu wa kuajiriwa ikitokea hivyo lazima black markets na syndicates za ajabu ajabu zitatokea na serkali itashindwa ku control mambo na matokeo yake nguvu itatumika kubwa...
 
Mbaya zaidi wapo wajinga wanasema huyu jamaa kafanya mambo makubwa sana ndani ya muda mfupi!
Ni wale tu waliowekewa keki ya taifa mezani kwao mkuu, so hawana budi kufanya hvyo ili waendelee kuupata utamu wa keki
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Mkuu wewe umejiajiri...una hata bustani ya mboga,uzuri wa dunia inazunguka,leo utajiona mjanja na kukashfu watoto wa wenzio wanaohangaika...hujui kesho ni nani,huenda akawa mdogo wako,mtoto wako or hata mtoto wa dada yako...karma is watching you...naye atakutana na kashfa kama hizi unazowapa watoto wa wenzio
 
Wasomi wa Miaka hii Aibu Tupu...
Mtu unakaa na akili zako Huoni Aibu unalalamika Ajira Hakuna hahahaaa
Sasa Kama ww na usomi wako unalalamika Ajira Hakuna Je yule Aliyeishia La Saba atafanyaje...
Na usomi wako unashindwa Hata kulima bustani ya mchicha mtaji ni 20,000/-
Na usomi w@ko unashindwa Kulima Hata nyanya Kwa greenhouse Mtaji wa Laki Moja?
Ila umekaa nyumbani tu kwa baba unalalamika tu hakuna ajira
Sema kwamba ww unasubiri ajira za serikali na wala hushughuliki na Ajira binafsi na Kijiajiri
Pole Sana...
Hakuna serikali ya Namna hiyo Duniani ikawa na uwezo wa Kuajiri wananchi wake wote wanaotaka ajira
Kweli kuna tofauti kubwa sana katika vichwa vyetu.Hivi wewe kijana fikiria Mhitimu wa Mawasiliano, Uhandisi,Ugavi au Uhasibu ameandaliwa kwa miaka mitatu au mitano thamani yake kwa maana ya utendaji kazi ni shilingi ngapi ? pengine huo mchicha ndio alilima na Baba na Mama yake wakauza wakiamini asome aje asaidie taifa katika sekta nyingine na mapato yatayopatikana huko pengine atawanunulia japo Trekta wazazi wake wapunguze tabu za jembe la mkono. Hivi mfano mtu analima mchicha na ni mhandisi katika muda wa ziada kuna shida jibu ni hapana,je mtu ni mtaalamu wa uhandisi na kuna uhitaji wake ila analima mchicha kwa sasa hiyo ni sawa? Yakupasa urudi darasani kujifunza kufikiria..
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Wewe ndio hauna akili kwa fikra zako watu waende mashambani wakalime, umewapa huo mtaji? Hayo mashamba? Muwe mnafikilisha akili hata kidogo, weka mazingira ya hao watu kujiajiri then you can talk. Pia ni jukumu la serikali kuweka mazingira ya private sector to thrives ili watu wapate ajira
 
Aiseeee Hivi mnajua kwamba swala la kujiajiri hata wazazi wa graduates waliolipa ada hawataki kulisikia.
Kujiajiri sio suala baya, tatizo ni mtaji, hamna anaweza kujiajiri no matter how smart he is bila capital, hata kama unaplan nzuri ya kujiajiri unajiajiri vipi?
 
Back
Top Bottom