Kwanini ajira hakuna?

Kwanini ajira hakuna?

Agriculture is a proven engine for poverty reduction. GDP growth generated by agriculture is more effective in reducing poverty than growth in any other sector. In sub-Saharan Africa, growth in agriculture .reduces poverty up to 11 times faster than growth in other sectors...Kilimo Kwanza ingetutoa..mnakuja na Tanzania ya viwanda..Vijana adui yenu CCM hawataki Vijana matajiri..
Ulianza vizuri, lakini ukaharibu mwisho na siasa za upinzani! Kilimo kwanza na Tanzania ya viwanda zote sera za CCM. Au ulikuwa hujui?
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
We ndo mbuziiiiiiiiiiii!?
 
Mpaka Leo vijana wengi wako mitaani na degree zao ,hakuna ajira waalimu hawapandishwi madaraja,

Vijana wa kitanzania leo hii wanaenda jkt kufundishwa ukakamavu..s kwel watu wanaenda kutafuta ajira bt wanakalishwa miaka halafu leo hii wanarudishwa mitaan je wafanye nini huku au mnataka watukabe


Wahitimu wa chuo leo hii hawana thaman..wimbi kuubwa la waalimu wa michepuo ya sanaa hawapew ajira na hata zkitangazwa sijui wanapewa akina nani




Ndugu zangu am not happy cuz ama victim of this chain..

Ngoja ni waite Vuvuzela wa sereklai hii wakujibu Mzee Mwanakijiji Tunaomba jibu.
 
Daaah wazee punguzeni hasira aseeh... tuendeleeni tu kutandika mtori nyama tutazikuta tu chini... ila hali ni mbaya sana yaani..
watu wana mahasira
 
On the other side of the coin, tuwe wakweli mtaani purchasing power imepungua! Tujikite katika kilimo it's ok, mazao nayo bei si ya kuridhisha kivile, mambo si marahisi kama tunavyo type hapa kwenye keyboard!
Sasa kama awamu hii ilivyogota na kushindwa kutengeneza ajira, wasomi waendelee kukaa tu mpaka awamu nyingine? Tanzania ardhi yenye rutuba tunayo tele kwann wasijiajiri
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Unafahamu ajira ambazo lazima izitoe
Ngoja nkuambie serikal lazma iajir
Waalimu cuz inamiliki while
Madaktar cuz wanamilk hospital
Wanajeshi/mapolice,maaskar wote kwa sababu wanamilki vkos vya ulinz na usalama...



Unajua wew unasema ivo cuz mmekaririshwa sumu ambayo hao waliowapa wameajiriwa na serikal
We kalia kuamn ivo huyo mwanao atakuja kula majan kama hali ikiendelea hapo baadae....


Inabd tuweke misngi mizur ili tuwe na maendeleo chanya.

Sasa mnasema tujiajir Hatujasomea hizo INTERPRINEURSHIP bana wapo wenye fani zao
 
Tatizo vijana wengi wanaomaliza hawawazi nje box, kazi wanataka za ofisini kisa mtu ana degree... Chengine JKT hai ajiri wanasisitiza kila siku wale jamaa wa JWTZ kwenye Media....... Cjui tunafeli wapi kutafuta uelewa wa mambo
Sasa iweje wawachukue vijana na kuwapelekesha huko kwenye kambi zao kama hawaajir hao vikos vingine vinatoa wapi watu cuz kila askar yeyote lazma apitie jkt au unataka kunambia jeshi LA kujenga taifa jkt limekufwaa....achen ujinga swala la ajira kwann lisiulizwe au lisjadiliwe kwenye awamu hiii? Halafu mkiulizwa mnakimbilia kujiajir
Hiv ndo solutions kweli eg..ualimu inamaana walimu wamejaa huko kwenye mashule inamaana watu hawastaaf,hawaachi kazi au hawafi ili replacement isiwepo
 
Tatizo la Ajira nchini Tanzania ni Mtambuka sana Mkuu ambapo Wazazi wana lawama zao, Shule na Taasisi za Elimu zina lawama zao, Serikali kupitia Wizara husika na Waziri husika wana lawama zao na Wanafunzi wenyewe nao wana lawama zao vile vile na tena huenda Wanafunzi ndiyo wakabeba lawama nyingi katika hawa Wahusika wote hapa.

Wazazi wengi wanawalazimisha Watoto Wao Kuchukua Kozi wasizoziweza hatimaye wanakwamisha Ndoto zao Kitaaluma.

Shule na Taasisi za Elimu nchini haziwaandai Wanafunzi kuja Kujiajiri wenyewe na Kutengeneza Mitaala ambavyo itakuwa inaakisi Soko la Ajira kwa sasa duniani na badala yake Elimu ya Tanzania bado imekuwa ni ile ile aliyotuachia Mkoloni.

Serikali na Wizara husika hazijatambua kuwa dawa pekee ya Kumaliza hili tatizo ni Kwanza kubadili Sera zake hasa katika Mashirika na Makampuni huku zikiwataka Taasisi za Kbenki nchini kuwa wanatoa Mikopo ya Riba nafuu kwa Vikundi mbalimbali vya Wahitimu ili wakimaliza tu Masomo yao wawaze Kujiajiri na siyo Kuzunguka hovyo Mitaani na Bahasha za Kaki pekee. Kipengele cha Uzoefu kiondolewe kwani Mtu Uzoefu haupatii akiwa Jobless bali akiwa Kazini kutoka kwa Wakongwe aliowakuta na ambao wanatarajia Kustaafu.

Wanafunzi wengi wa sasa wa Tanzania hawajui wanataka nini, hawajitambui kabisa na wengi Wao wanasoma kwa Mkumbo na siyo Kusoma ili waje kuwa Tegemeo. Kama Mwanafunzi wa Kidato cha Nne au Sita unamuuliza anataka kuja nani baadae anakujibu hajui au anakutaka Wewe uliyemuuliza hilo Swali umtathmini alivyo kisha umfanyie Kazi ya Marehemu Sheikh Yahya umtabirie asomee nini hapo hakuna tatizo? Wanafunzi wengi ni Wavivu na hawapendi Kujiimarisha Kimaarifa ili waje kuwa Wanataaluma wazuri kwa baadae.

Yangu ni haya tu Mkuu.
Nimekusoma mkuu
Tukianza kujadili swala LA elimu etu hatuta maliza Leo cuz kunamapungufu meengi ambayo lazma yaondolewe ili kuendana na hali ya hiv sasa....
Pia mfumo wa ajira inabdi urekebishwe bcoz Haupo fair kwa muhitimu.
 
Nadhani wewe ndo kipofu na mjinga. Ulitaka akujengeebnyumba? Alete posa kwenu? Akuajiri ? Ndo ujue?. Jinga kabisaa
Mbaya zaidi wapo wajinga wanasema huyu jamaa kafanya mambo makubwa sana ndani ya muda mfupi!
 
Sasa hapo ndo umejibu swal langu bt miaka ote pesa za kuajir vijan zalikuwa znatoka wap!???kama sio CHOYO na udikteta wa kizaman wa akina Hitler na wenzake
Hakuna hela za kulipa mishahara, Waajiri wengi wanataka kupunguza gharama za uendeshaji. POLE SANA
 
N ukosefu wa kujitambua tu kwetu sisi RAIA bcoz hamna hata sector iliyo hoji au kutengeneza hoja zenye muktadha wa kuhoji ajira zko WAP
N haki kwel mwalimu akalime huko mbinde akat wanafunz hawana wa kuwafundsha elimu inaenda wap?
Kuna mbwa wachache wanao kula na kusaza kwa kutumia kodi zetu. Hawa wanaona ukosefu waajira kama ni tatizo la kujitakia.Wataanza kukuambia habari za ukalime ili kujiaajiri na wanaongea hivyo wakati wao hawana hata bustani.Wanasahau hata nchi zilizoendelea kama Marekani,France,Britain nk zinatoa mafunzo ya kujiajiri kwa vijana wao wanapokua masomoni lakini hiyo haitoshi pia wale vijana wanapomaliza masomo husidiwa ajira au fedha za mitaji ili kujiajiri; kumbukeni tatizo la ajira lilivyo kiua wakati Barrack Obama anaingia madarakani mliona jinsi alivyo toa ajira nyingi badala ya kutoa kejeli kwamba wakalime.sio jambo la maana sana nchi kusomesha watubwake wengi kisha iwaambie wakalime, hivyo tunajitengenezea bomu litakalolipuka siku za baadae
 
Ajira hazipo sio kwa sababu ya mtawala wa sasa au yul aliepita. Ajira zilipotea mara baada ya kuacha kufikiria kwa malengo ya muda mrefu kwa kuwa na mfumo jumuishi wa ajira.

Walimu, polisi, sekta ya afya, sekta nyngi za huduma zinatengemea mishahara itokanayo na makusanyo ya kodi na vyanzo vingine visivyo vya kikodi (wao huko serikalini wanaita maduhuli ya serikali)

Viwanda ndiyo mfumo pekee ambao una-absorb watu wengi kupata ajira maana viwanda vinalenga kuzalisha kwa faida. Kiwanda kikiwepo popota kinatoa ajira moja kwa moja. Then kuna kodi za mauzo ya bidhaa serikali inapata, kuna kodi za mishahara serikali inapata. Kuna kodi za kiwanda kununua malighafi, serikali inapata, kuna malipo ya viwanda kununua huduma
Umeme
Maji
Bima
Kutumia huduma za kibeki
Huduma za kisheria na kadhalika.

Kama uko ofisini au shambani au popote, angali asilimia kubwa ya vitu, nguo, baadhi ya vyakula, magari, fanicha za ofisini na mengine mengi… importation inasababisha fedha yetu kwenda ughaibuni. Maana tuna import mpaka wembe, toilet peper, toothpick (It was a grave mistake kuua viwanda)

Tukiwa na viwanda vingi, private sekta, maana yake serikali itahitajika pia kuajiri watu wengi (service sekta kushirikiana na private sekta)… no short cut.

Tanzania tunategemea kilimo… ingia maduka ya kilimo mbegu, madawa ya Wanyama, madawa ya kilimo, pump za kupuliza dawa, mbolea kule zinakotengenezwa ndiko ajira zilipo.
Tungetengeneza ndani, ajira zingebaki humu.

So, tusitafute mchawi. Tuoneni namna gani ya kukaa mezani na JPM na askari wake wa mwamvuli. Tufungue miradi ya uwekezaji inayo-cut down imports. Then tuanze ku export walau vitambaa, chakula cha Wanyama, unga ukiwa packed, mafuta ya kula ya alizeti na ufuta ni hot cake ulaya na mataifa yalioendelea… eventually vijana watapata ajira.

Sijui kama wengi wanafikiria kwa picha hii kwenye public sector kama facilitating agency ya kukua kwa private sekta.
Private sekta ikitengeneza faida 25% to 30% ya net profit ni kodi kwa serikali. It goes without saying serikali ni shareholder wa private sekta.

Ajira zitapatikana if we decide inclusively to solve our own problems and the problem of other countries. Nje hapo, hakuna ajira. No short cut.

Tutafika siku moja. Mungu ibariki Tanzania
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.

Lengo kuu la serikali kuwasomesha/kuwapa elimu wanainchi wake ni kuhakikisha kwamba kupitia wanainchi hao walioelimika tunapata taifa imara wakitumia taaluma zao ipasavyo katika nyanja mbali mbali.

Na katika kutimiza hilo serikali ndio inayotoa muongozo kwa kuunda sera mbali mbali ambazo zinatekelezwa kwa mtindo wa mgawanyo wa kimajukumu. Na wakufanya majukumu hayo ni hao hao wanainchi, hivyo basi kumbe serikali inatengeneza wasomi hili ije iwaajiri hapo baadae.

Sasa labda nikuulize wewe, unaposema kwamba ajira za kupewa hakuna na hizo ajenda/sera/majukumu zinatekelezwaje na wanazitekeleza wakina nani?

Huko mashambani unapokusema ndio watu wanaenda tu hivi hivi hata kama hawana A wala B kama starting point ya kujiajiri? na kwanza kuna haja gani ya mtu kusoma sheria kwa miaka 18 halafu leo hii aende akajiajiri shambani ambako hakuna uhusiano wowote na taaluma yake ya sheria?

Nina binadamu zangu wawili mmoja ana shahada ya political science na mwingine ya Public administration, hawa wote hawana ajira. Sasa je, na wao wakajiajiri huko mashambani unakosema wakitumia hizo taaluma zao?

Kwanza sehemu zingine za huko duniani unafahamu kwamba wana sera nzuri za kiuchumi kuliko sisi na zinafanya kazi ipasavyo lakini bado serikali inalaumiwa kwa wanainchi kukosa kazi na inakubali lawama? yaani mpaka wameamua kuja na program mbadala wa kutatua tatizo la ajira, unafahamu kitu kinachoitwa working claims?

Serikali haiweze kukuepuka hili suala la unemployment linalokuwa kwa kasi, wao ndio wahusika namba moja wa kubeba lawama.

Imeshindwa kuandaa mazingira/sera nzuri za kukabiliana na tatizo hili. Halafu kuna wapuuzi kama wewe mnakuja na kauli nyepesi za kutetea hovyo ineptness ya serikali yenu eboo!!

Binafsi nafikiri wewe ndio uachage ujinga kabisa! shwaini
 
Kuna mbwa wachache wanao kula na kusaza kwa kutumia kodi zetu. Hawa wanaona ukosefu waajira kama ni tatizo la kujitakia.Wataanza kukuambia habari za ukalime ili kujiaajiri na wanaongea hivyo wakati wao hawana hata bustani.Wanasahau hata nchi zilizoendelea kama Marekani,France,Britain nk zinatoa mafunzo ya kujiajiri kwa vijana wao wanapokua masomoni lakini hiyo haitoshi pia wale vijana wanapomaliza masomo husidiwa ajira au fedha za mitaji ili kujiajiri; kumbukeni tatizo la ajira lilivyo kiua wakati Barrack Obama anaingia madarakani mliona jinsi alivyo toa ajira nyingi badala ya kutoa kejeli kwamba wakalime.sio jambo la maana sana nchi kusomesha watubwake wengi kisha iwaambie wakalime, hivyo tunajitengenezea bomu litakalolipuka siku za baadae

Kuna mpuuzi mmoja hapo kwenye comment za mwanzo kaniudhi sana!
 
Mpaka Leo vijana wengi wako mitaani na degree zao ,hakuna ajira waalimu hawapandishwi madaraja,

Vijana wa kitanzania leo hii wanaenda jkt kufundishwa ukakamavu..s kwel watu wanaenda kutafuta ajira bt wanakalishwa miaka halafu leo hii wanarudishwa mitaan je wafanye nini huku au mnataka watukabe


Wahitimu wa chuo leo hii hawana thaman..wimbi kuubwa la waalimu wa michepuo ya sanaa hawapew ajira na hata zkitangazwa sijui wanapewa akina nani




Ndugu zangu am not happy cuz ama victim of this chain..
soma kuajiriwa kupo tu
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Hilo unatutukana sisi wakulima, ondoa kauri yako. Tunawalipa mishahara mtunge sera, je mliweka lini mtaala wa kilimo kwa walimu? Kilimo ni fani, usikisharau. Ulitakiwa kuweka vitivo vingi vya kilimo, leo usingesikia kelele za ukosefu wa ajira. Uliyakoroga, yanywe. Ajiri vijana kulingana na elimu zao.Malumbano nao mitaani hayana tija. A wasaidiwe kusomea fani mbadala.
 
Back
Top Bottom