Kwanini ajira hakuna?

Kwanini ajira hakuna?

Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Hizi akili hizi!
Nchi kama Japan,Korea,USA,na UK wana uchumi mkubwa mala 1000,ya wakwetu,lakini wanazungumzia ajira za wasomi wao wakitoka vyuoni! Sasa TZ ambayo bado hata kujitoshereza kwa bajeti yake haiwezi,unashangaa vijana kutaka wapewe ajira!
Kama hao wakubwa na elimu yao nzuri,wanayotoa bado wasomi wao wanatafuta ajira za umma,sembuse sie! Acha kuwa mchawi!
Unafikiri kusomea shahada ya kwanza ni sawa na kuendesha boda bora au kutumia simu janja!
Wewe kama ulisoma hesabu za aljebra darasa LA saba,ukafikiri ndio mwisho wa hesabu,kuna kitu kinaitwa Engineering mathematics!
 
Kwani ukiwa na degree lazima upewe ajira? Acheni ujinga ninyi wasomi, ajira za kupewa hakuna duniani kote. Nendeni mashambani mkajiajiri kwa kulima.
Mbaya zaidi waonaosema haya maneno na wenyewe hua wameajiriwa , hawajawahi kuwaza au kujiajiri hata siku moja
 
Wasomi wa Miaka hii Aibu Tupu...
Mtu unakaa na akili zako Huoni Aibu unalalamika Ajira Hakuna hahahaaa

Sasa Kama ww na usomi wako unalalamika Ajira Hakuna Je yule Aliyeishia La Saba atafanyaje...

Na usomi wako unashindwa Hata kulima bustani ya mchicha mtaji ni 20,000/-
Na usomi w@ko unashindwa Kulima Hata nyanya Kwa greenhouse Mtaji wa Laki Moja?
Ila umekaa nyumbani tu kwa baba unalalamika tu hakuna ajira

Sema kwamba ww unasubiri ajira za serikali na wala hushughuliki na Ajira binafsi na Kijiajiri

Pole Sana...

Hakuna serikali ya Namna hiyo Duniani ikawa na uwezo wa Kuajiri wananchi wake wote wanaotaka ajira
Fafanua hiyo green house ya mtaji wa laki moja!! Kweli masikini akipata mata.ko ulia mbwata
 
Unafikiri kusomea shahada ya kwanza ni sawa na kuendesha boda bora au kutumia simu janja!
Wewe kama ulisoma hesabu za aljebra darasa LA saba,ukafikiri ndio mwisho wa hesabu,kuna kitu kinaitwa Engineering mathematics!
Pumbavu! Sasa kama wewe ulisoma zaidi ya aljebra umeshindwa vipi kujitegemea? Mbona sisi wa aljebra tunaishi maisha yeti hatulii kama wewe?

Halafu we mjinga hebu tega sikio nikwamboe kitu. Huko kwenye mataifa uliyoyataja hakuna ardhi kubwa yenye rutuba kama iliyopo Tanzania.

Kwahiyo kwa msomi aliyeelimika hapa Tanzania anapomaliza chuo tayari anakuwa na mitaji 3 ya kujiqjiri:- nguvu zake, elimu yake, na ardhi tele yenye rutuba inayopatikaa bure ktk mikoa ya Tanga, Katavi, na Tabora.

Ukiendelea na mawazo haya utadeki choo na kufua nguo za shemeji yako mpk uzeeke
 
Ajira hazipo sio kwa sababu ya mtawala wa sasa au yul aliepita. Ajira zilipotea mara baada ya kuacha kufikiria kwa malengo ya muda mrefu kwa kuwa na mfumo jumuishi wa ajira.

Walimu, polisi, sekta ya afya, sekta nyngi za huduma zinatengemea mishahara itokanayo na makusanyo ya kodi na vyanzo vingine visivyo vya kikodi (wao huko serikalini wanaita maduhuli ya serikali)

Viwanda ndiyo mfumo pekee ambao una-absorb watu wengi kupata ajira maana viwanda vinalenga kuzalisha kwa faida. Kiwanda kikiwepo popota kinatoa ajira moja kwa moja. Then kuna kodi za mauzo ya bidhaa serikali inapata, kuna kodi za mishahara serikali inapata. Kuna kodi za kiwanda kununua malighafi, serikali inapata, kuna malipo ya viwanda kununua huduma
Umeme
Maji
Bima
Kutumia huduma za kibeki
Huduma za kisheria na kadhalika.

Kama uko ofisini au shambani au popote, angali asilimia kubwa ya vitu, nguo, baadhi ya vyakula, magari, fanicha za ofisini na mengine mengi… importation inasababisha fedha yetu kwenda ughaibuni. Maana tuna import mpaka wembe, toilet peper, toothpick (It was a grave mistake kuua viwanda)

Tukiwa na viwanda vingi, private sekta, maana yake serikali itahitajika pia kuajiri watu wengi (service sekta kushirikiana na private sekta)… no short cut.

Tanzania tunategemea kilimo… ingia maduka ya kilimo mbegu, madawa ya Wanyama, madawa ya kilimo, pump za kupuliza dawa, mbolea kule zinakotengenezwa ndiko ajira zilipo.
Tungetengeneza ndani, ajira zingebaki humu.

So, tusitafute mchawi. Tuoneni namna gani ya kukaa mezani na JPM na askari wake wa mwamvuli. Tufungue miradi ya uwekezaji inayo-cut down imports. Then tuanze ku export walau vitambaa, chakula cha Wanyama, unga ukiwa packed, mafuta ya kula ya alizeti na ufuta ni hot cake ulaya na mataifa yalioendelea… eventually vijana watapata ajira.

Sijui kama wengi wanafikiria kwa picha hii kwenye public sector kama facilitating agency ya kukua kwa private sekta.
Private sekta ikitengeneza faida 25% to 30% ya net profit ni kodi kwa serikali. It goes without saying serikali ni shareholder wa private sekta.

Ajira zitapatikana if we decide inclusively to solve our own problems and the problem of other countries. Nje hapo, hakuna ajira. No short cut.

Tutafika siku moja. Mungu ibariki Tanzania
Akili nyingi🕴️
 
Ajira nyingi zingetokana na wingi wa wajasili mali wadogo wadogo.
Tungetegemea benki zetu kwa kushirikiana na serikali iache kupuuzia entrepreneur hao.

Kwa mfano katika mega projects za Raisi Magufuli kama angekuna kichwa na wabobezi wa uchumi akatenga Trillion 6 kwa miradi ya wajasili kwa wastani wa sh milioni 1 kila mradi, ni wastani wa miradi milioni 6 siyo haba.

Hao wajasili mali wakiweza kurudisha mkopo huo na riba ndogo baada ya miaka mitatu tunaweza kutengeneza miradi mingine midogo midogo milioni 6.hivyo kwa kipindi kidogo cha miaka 6 tutakuwa na miradi midogo midogo milioni 12.

Watu ndio uchumi, ukiwezesha watu,hao watu ndio wanatengeneza uchumi.
Hata hiyo mega projects za Raisi Magufuli itakuwa rahisi sana kuijenga kutokana na wingi wa walipa kodi.
 
Mpaka Leo vijana wengi wako mitaani na degree zao ,hakuna ajira waalimu hawapandishwi madaraja,

Vijana wa kitanzania leo hii wanaenda jkt kufundishwa ukakamavu..s kwel watu wanaenda kutafuta ajira bt wanakalishwa miaka halafu leo hii wanarudishwa mitaan je wafanye nini huku au mnataka watukabe

Wahitimu wa chuo leo hii hawana thaman..wimbi kuubwa la waalimu wa michepuo ya sanaa hawapew ajira na hata zkitangazwa sijui wanapewa akina nani

Ndugu zangu am not happy cuz ama victim of this chain..

Herla zote zinaelkezwa kwneey SGR, Nyerere DAM, Ndege.
 
Mpaka Leo vijana wengi wako mitaani na degree zao ,hakuna ajira waalimu hawapandishwi madaraja,

Vijana wa kitanzania leo hii wanaenda jkt kufundishwa ukakamavu..s kwel watu wanaenda kutafuta ajira bt wanakalishwa miaka halafu leo hii wanarudishwa mitaan je wafanye nini huku au mnataka watukabe

Wahitimu wa chuo leo hii hawana thaman..wimbi kuubwa la waalimu wa michepuo ya sanaa hawapew ajira na hata zkitangazwa sijui wanapewa akina nani

Ndugu zangu am not happy cuz ama victim of this chain..
Ajira zote zilizopo huzioni?
 
Ajira nyingi zingetokana na wingi wa wajasili mali wadogo wadogo.
Tungetegemea benki zetu kwa kushirikiana na serikali iache kupuuzia entrepreneur hao.

Kwa mfano katika mega projects za Raisi Magufuli kama angekuna kichwa na wabobezi wa uchumi akatenga Trillion 6 kwa miradi ya wajasili kwa wastani wa sh milioni 1 kila mradi, ni wastani wa miradi milioni 6 siyo haba.

Hao wajasili mali wakiweza kurudisha mkopo huo na riba ndogo baada ya miaka mitatu tunaweza kutengeneza miradi mingine midogo midogo milioni 6.hivyo kwa kipindi kidogo cha miaka 6 tutakuwa na miradi midogo midogo milioni 12.

Watu ndio uchumi, ukiwezesha watu,hao watu ndio wanatengeneza uchumi.
Hata hiyo mega projects za Raisi Magufuli itakuwa rahisi sana kuijenga kutokana na wingi wa walipa kodi.
Toka Sumaye akiwa PM mikopo midogo midogo imekuwa ikitolewa kwa vijana na akina mama, na baadae walemavu nao wameongezwa ukiangalia impact kwa ni ndogo sana.

Mfumo wa ajira ambao haupo kwenye organized sector ambayo watu wanazalisha, wanatengeneza faida, wanalipana mishahara, wanachangia mifuko ya pensheni kwa mishahara yao na kukua kwenye profession hadi kufikia apex ya fani/kada aliyopo. Ni muujiza mkubwa kwa mmachinga, bodododa kuweza kukua hadi kufikia apex ya maisha bora na anapostaafu at 60 years akapata pensheni.

Waajiriwa kwenye organized sector ndiyo wame-breed NSSF,NHIF, PPF, PSPF, LAPF na GEPF (ambazo sasa zimezaa PSSSF).
Wamachinga na bodaboda ni wengi sana kuliko wachangiaji wa iliyokuwa PPF; ila kwa kuwa ni unorganized society sio rahisi tukajenge uchumi endelevu kupitia watu kama hawa.

Moja ya namna ya kutengeneza ajira, jibu alitoa JPM wakati wa mkutano wa SADC 2019.

Kuna sehemu ya ajira tunazipeleka Ulaya kwa kuuza raw materials; wakati tungetengeneza consumable goods, tungetengeza ajira za kutosha
 
Mkuu wewe mwenyewe unakili hiyo misaada haijaleta impact kwa sababu haikufanyiwa upembuzi yakinifu.
Lakini mkuu kama nguvu kazi tugeitumia kwa mfano ukulima wa tractor na pembejeo kama ulimaji wa miwa na utengenezaji wa sukari ya viwanda vidogo ingeleta impact na zaidi ya hapo tusingekuwa na tatizo la sukari.
Au kama wangepewa mikopo ya kununua ngombe wa maziwa,wakafuga tukapata maziwa ya kutosha.Sio siri ni watanzania wachache wanakunywa maziwa au hata chai ya maziwa ukilinganisha na Kenya.
Kwa kilimo tuna fursa nyingi hadi samaki wa kufugwa kama prawns n.k
Hiyo miradi haikupewa kipaumbele, laiti ingepewa kipaumbele vijana wasio na kipato waliokuwa vijiji wangekaa huko huko wala usingekuwa na lundo la machinga mjini.
Nina imani ingeleta impact.
Kwa sasa machinga ni mtaji wa kisiasa kwa wanasiasa tu wanaowatumia kwa maslahi yao tu.
Hizo habari za kwamba tunapeleka Ulaya raw material ndio tatizo is too theoretical kama tunajua hilo mbona hatujachukuwa hatua za msingi?
Mfano hai ni Tanganyika Packers ikizalisha nyama ya makopo kupeleka nchi za nje leo imegeuka kanisa la Mwaiposa!!
Mifano ni mingi.
 
Wasomi wengi wanategemea kazi za shati nyeupe, swali ni je mfumo uliopo unazalisha hizo kazi kwa kasi ya kuendana na kuzalisha wahitimu wa vyuo ama tumekalia kuimba “tuko pazuri, tutembee kifua mbele????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mbwa wachache wanao kula na kusaza kwa kutumia kodi zetu. Hawa wanaona ukosefu waajira kama ni tatizo la kujitakia.Wataanza kukuambia habari za ukalime ili kujiaajiri na wanaongea hivyo wakati wao hawana hata bustani.Wanasahau hata nchi zilizoendelea kama Marekani,France,Britain nk zinatoa mafunzo ya kujiajiri kwa vijana wao wanapokua masomoni lakini hiyo haitoshi pia wale vijana wanapomaliza masomo husidiwa ajira au fedha za mitaji ili kujiajiri; kumbukeni tatizo la ajira lilivyo kiua wakati Barrack Obama anaingia madarakani mliona jinsi alivyo toa ajira nyingi badala ya kutoa kejeli kwamba wakalime.sio jambo la maana sana nchi kusomesha watubwake wengi kisha iwaambie wakalime, hivyo tunajitengenezea bomu litakalolipuka siku za baadae

Wao si wakalime tuone au wanasema vijana mjiajiri wakati pesa zao wameweka overseas kwenye fixed desposit.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka Leo vijana wengi wako mitaani na degree zao ,hakuna ajira waalimu hawapandishwi madaraja,

Vijana wa kitanzania leo hii wanaenda jkt kufundishwa ukakamavu..s kwel watu wanaenda kutafuta ajira bt wanakalishwa miaka halafu leo hii wanarudishwa mitaan je wafanye nini huku au mnataka watukabe

Wahitimu wa chuo leo hii hawana thaman..wimbi kuubwa la waalimu wa michepuo ya sanaa hawapew ajira na hata zkitangazwa sijui wanapewa akina nani

Ndugu zangu am not happy cuz ama victim of this chain..
Mbona kazi zipo tu kibao? Degree yako inatakiwa ikusaidie kuona fursa zilizopo.
 
Back
Top Bottom