Kwanini ajali nyingi hutokea usiku?

Ze Heby

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
5,252
5,319
Wanajamvi salaam.

Kwa utafiti wangu usio rasmi kwenye vyanzo mbali mbali vya habari ikiwemo JamiiForums, nimebaini kwamba ajali nyingi hasa zile mbaya hutokea mida ya usiku. Barabara maarufu kwa ajali kama maeneo ya Mikese imekua ikishuhudia ajali mbaya zinavypelekea vifo vya watu wengi na ulemavu.

Ifahamike kwamba, madereva wengi wanadokeza kwamba usiku hali ya barabara hua ni utulivu sana na hakuna magari mengi, hivyo ingetarajiwa kwamba ajali zingekua chache, lakini ni kinyume chake.

Naleta kwenu tujadili nini kinaweza kua chanzo cha ajali nyingi kua usiku wakati hali iko tulivu na favourable kwa dereva makini


Pumzika kwa amani daktari.
 
Sababu kuu ni moja tu, Kusinzia. Pombe na mambo mengine ni asilimia chache sana, na ndio maana utaona hata sehemu gari zinapoanguka ni sehemu ya kawaida sana.

Ukipanda daladala usiku, ukiona konda anapiga piga mlango unnecessarily, ujue anamshtua dereva.

Ukisikia makonda anataja taja neno " zeshen" hii maana yake dereva analala.


Na sababu nyingine wakichoka wanawapa manyoka ambao hawana experience.
 
Sababu kuu ni moja tu, Kusinzia. Pombe na mambo mengine ni asilimia chache sana, na ndio maana utaona hata sehemu gari zinapoanguka ni sehemu ya kawaida sana....
"Ukipanda daladala usiku, ukiona konda anapiga piga mlango unnecessarily, ujue anamshtua dereva.

Ukisikia makonda anataja taja neno " zeshen" hii maana yake dereva analala"

Juzi hapa Dodoma🤝🤝🙌🙌🙌🙌
 
Ila usiku kuona mbali inakuwa shida hata kama taa zako ziko vizuri, bado usiku visibility ni tatizo.....halafu hapohapo serikali inaruhusu magari ya abiria kusafiri masaa 24, tutarajie majanga zaidi....
 
Wanajamvi salaam.

Kwa utafiti wangu usio rasmi kwenye vyanzo mbali mbali vya habari ikiwemo JamiiForums, nimebaini kwamba ajali nyingi hasa zile mbaya hutokea mida ya usiku. Barabara maarufu kwa ajali kama maeneo ya Mikese imekua ikishuhudia ajali mbaya zinavypelekea vifo vya watu wengi na ulemavu....
Kwa eneo moja tu unaweza kutoa huo mtazamo lakini kwa takwimu rasmi za jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ajali nyingi hutokea mchana kutokana na Mwingiliano mkubwa wa watu.

Mwingiliano mkubwa wa magari.

Shughuli nyingi kufanyika asubuhi mchana na jioni na maranyingi ikiwa ni asubuhi na jioni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchovu unaopelekea usingizi. Mchana kutwa mtu anazunguka na shughuli zake ili asafiri usiku.
 
Asilimia kubwa ni kuchoka na usingizi + speed kubwa kwa magari mengi nyakati za usiku, na angalia Sana Ajali nyingi hutokea Kuanzia saa 9 Usiku na kuendelea
 
Back
Top Bottom