Kwanini Afrika ni bara masikini na lisiloendelea?

Andrew Tate

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
3,824
5,811
KWANINI AFRICA NI BARA MASIKINI?

Heshima yenu wakubwa na wadogo.

Bara la Afrika ni bara la pili kwa ukubwa baada ya Asia, ni bara lenye kila aina ya utajiri na rasilimali za kutosha.

La kushangaza ni bara masikini kuliko yote na la mwisho katika kila kitu, yaani ni masikini kiasi cha kustaajabisha.

Je, tatizo ni nini? ni kitu gani kinachosababisha bara hili kuwa masikini kiasi hiki?

Haya ni mambo matatu yanayoweza kuwa chanzo cha yote.

1: JE, NI ELIMU?
AFRICA imekuwa iikitumia elimu ile ya mkoloni. elimu ambayo ipo ili kuandaa watu waje kufanya kazi ya mtoa elimu huyo yani mkoloni. na sio elimu ambayo itakujenga kifikra au kiakili. Sio elimu itakayokujenga uwe mbunifu na kutumia ubunifu huo kutatua changamoto zako na za jamii yako. elimu itakayokufanya ujitambue ili ujitegemee utegemee akili yako binafsi. HAPANA bali ni inayokuandaa kuwa mtumwa uliye advance.

Hadi leo elimu hii inafanya kazi ya kukalilisha watu mambo ambayo hayana impact kwenye maisha yao zaidi ya kwenda kuomba kazi ambayo ataifanya maiha yake yote mpaka kufa kwake.

Hivyo nadhani elimu ni tatizo kubwa linalotufanya tuendelee kubaki hapa tulipo. Hivyo suluhisho ni kubadilisha mfumo mzima wa elimu yetu hii tunayoitumia.

2: JE, NI SIASA?
Africa bado tunafanya siasa ambayo haina tofauti na ukoloni. Viongozi wetu wote wanafanya mambo amabayo yana asili ya ukoloni ndani yake. UFISADI, RUSHWA, MASLAHI BINAFSI na WIZI bado vipo ndani ya siasa ya Africa.

Mwanasiasa anaiaba pesa anakwenda kuweka nje AFRICA. Uchumi wetu karibu asilimia 60% upo nje.

Siasa nalo ni tatizo pia. na tatizo hili linatokana na ELIMU ambayo nimeelezea hapo juu. Viongozi na wananchi ni zao la elimu ya mkoloni ambayo haimjengi mtu kujitambua{self awareness} Haimjengi mtu kutumia akili yake ipasavyo kama nilivyosema juu.

Hivyo siasa ni tatizo linalotoka na elimu yetu. solution ni kubadirisha mfumo wetu wa elimu. Alafu tutakuwa tumepiga ndege wawili kwa jiwe moja.

3: JE, NI DINI?
AFRICA tumekuwa tunatumia dini zilizoletwa na Mkoloni.{DINI ZOTE} dini ambazo zimeletwa ili kujenga hofu {fear} kumbuka ukitaka kumuendesha na kumteka mtu basi anza kumteka akili kwa kumjengea hofu.

Hivyo dini ni ya mkoloni ni jambo ambalo linachangia kwa kiasi chake kulibakiza BARA letu pendwa kuendelea kubaki nyuma na kubaki kuwa masikini miaka yote. dini imejenga mitazamo kwa watu ambayo ni migumu kung'oka. Solution ni ngumu kwa hapa sababu hii kitu ipo kwenye damu na imani amabayo ni ngumu kuibadirisha.

MFANO mdogo ni pale ambapo Mwafrika anakutwa na tatizo na kushindwa kuitatua sababu ana imani litatatuliwa na hicho anachoamini. Hii inapelekea kubweteka na kusubiria hivyo kubaki na tatizo hilo milele.

Hayo ni mambo matatu makuu yanayosababisha Afrika kuendelea kubaki nyuma kila siku. wewe Mwafrikaunadhani ni nini kinacho
sababisha afrika kubaki nyuma mpaka leo hii kwani miaka karibu 60 imepita tangu Mkoloni aondokea Tanzania na nchi baadhi za
Afrika.

Maoni yako nini?
 
Vyote ulivyovitaja apo juu na mabeberu ndo wanaofanya yote aya kupandikiza vibaraka wao kwajili ya maslahi yao mfano wazelendo kama Lumumba,Sankara na Gadaffi wote waliuliwa kwa njama zamabeberu..
 
Ukweli elimu ya mkoloni daily inatufanya kuwa watumwa kifikra kwa kuamini kua wao ndo chanzo cha elim akati hata sisi kupitia mawazo yetu tunaweza unda mfumo wa elim ulio rafiki na utakaoendana na mazingira yetu

kwenye siasa jambo kubwa ni kubadili mfumo huu wa mkoloni yaani tukawa na demokrasia inayoendana na matakwa yetu pia hata haki za binadam na nk...
 
Shida kubwa ya sis Africans ni uwezo hafifu wakufikiria
kwanza itatakiwa tukubali kua tunahiyo shida natuangalie nikwakiasi gani inatuathiri. hali duni za ustawi wajamii kma watoto kukosa malezi ya mzazi au wazazi, lishe duni, huduma Mbovu za afya na mahitaji muhimu ya Jamii inapelekea kudumaza uwezo waakili zetu nauwezo wetu wakutatua matatizo kua mdogo sana. Kulibadili hili bara haitakua Kazi rahis
 
Mimi naona ni kukopy kwetu kila walichofanya wao na sisi tunataka tupite mulemule,
badala ya sisi kugundua vya kwetu ambavyo havifanani na wao .
Hapa namaanisha kila kitu kuanzia nyumba magari ndege simu yani kila kitu ,ilibidi wakija huku washangae tumewezaje wezaje .
Mfano usafiri sisi ilibdi tufike mahali kwa haraka bila kutumia gari,kupaa bila ndege na magorofa ya kipee sio hayo waloanzisha wao.
Hapo tungekuwa matajir kuliko wao na tusingekuwa na shobo kama sasa.
Leo mtu anakwambia tauanataka kuwa kama ulaya wakati miaka inavyoenda na hiyo ulaya inabadilika sasa sijui lini tutakuwa kama ulaya hili ndio kosa kubwa tulokosea na Mungu atatuhukumu kwa upumbavu watu wakuiga kila kitu.
Maana yeye alitutenganisha alikuwa na maana yake angetaka tufanane kila kitu angtuumba wote weupe na bila haya mabara na mipaka.
 
Vyote ulivyovitaja apo juu na mabeberu ndo wanaofanya yote aya kupandikiza vibaraka wao kwajili ya maslahi yao mfano wazelendo kama Lumumba,Sankara na Gadaffi wote waliuliwa kwa njama zamabeberu..
Unadhani suruhisho ni nini mkuu?
 
KWANINI AFRICA NI BARA MASIKINI?

Heshima yenu wakubwa na wadogo.

Bara la Afrika ni bara la pili kwa ukubwa baada ya Asia, ni bara lenye kila aina ya utajiri na rasilimali za kutosha.

La kushangaza ni bara masikini kuliko yote na la mwisho katika kila kitu, yaani ni masikini kiasi cha kustaajabisha.

Je, tatizo ni nini? ni kitu gani kinachosababisha bara hili kuwa masikini kiasi hiki?

Haya ni mambo matatu yanayoweza kuwa chanzo cha yote.

1: JE, NI ELIMU?
AFRICA imekuwa iikitumia elimu ile ya mkoloni. elimu ambayo ipo ili kuandaa watu waje kufanya kazi ya mtoa elimu huyo yani mkoloni. na sio elimu ambayo itakujenga kifikra au kiakili. Sio elimu itakayokujenga uwe mbunifu na kutumia ubunifu huo kutatua changamoto zako na za jamii yako. elimu itakayokufanya ujitambue ili ujitegemee utegemee akili yako binafsi. HAPANA bali ni inayokuandaa kuwa mtumwa uliye advance.

Hadi leo elimu hii inafanya kazi ya kukalilisha watu mambo ambayo hayana impact kwenye maisha yao zaidi ya kwenda kuomba kazi ambayo ataifanya maiha yake yote mpaka kufa kwake.

Hivyo nadhani elimu ni tatizo kubwa linalotufanya tuendelee kubaki hapa tulipo. Hivyo suluhisho ni kubadilisha mfumo mzima wa elimu yetu hii tunayoitumia.

2: JE, NI SIASA?
Africa bado tunafanya siasa ambayo haina tofauti na ukoloni. Viongozi wetu wote wanafanya mambo amabayo yana asili ya ukoloni ndani yake. UFISADI, RUSHWA, MASLAHI BINAFSI na WIZI bado vipo ndani ya siasa ya Africa.

Mwanasiasa anaiaba pesa anakwenda kuweka nje AFRICA. Uchumi wetu karibu asilimia 60% upo nje.

Siasa nalo ni tatizo pia. na tatizo hili linatokana na ELIMU ambayo nimeelezea hapo juu. Viongozi na wananchi ni zao la elimu ya mkoloni ambayo haimjengi mtu kujitambua{self awareness} Haimjengi mtu kutumia akili yake ipasavyo kama nilivyosema juu.

Hivyo siasa ni tatizo linalotoka na elimu yetu. solution ni kubadirisha mfumo wetu wa elimu. Alafu tutakuwa tumepiga ndege wawili kwa jiwe moja.

3: JE, NI DINI?
AFRICA tumekuwa tunatumia dini zilizoletwa na Mkoloni.{DINI ZOTE} dini ambazo zimeletwa ili kujenga hofu {fear} kumbuka ukitaka kumuendesha na kumteka mtu basi anza kumteka akili kwa kumjengea hofu.

Hivyo dini ni ya mkoloni ni jambo ambalo linachangia kwa kiasi chake kulibakiza BARA letu pendwa kuendelea kubaki nyuma na kubaki kuwa masikini miaka yote. dini imejenga mitazamo kwa watu ambayo ni migumu kung'oka. Solution ni ngumu kwa hapa sababu hii kitu ipo kwenye damu na imani amabayo ni ngumu kuibadirisha.

MFANO mdogo ni pale ambapo Mwafrika anakutwa na tatizo na kushindwa kuitatua sababu ana imani litatatuliwa na hicho anachoamini. Hii inapelekea kubweteka na kusubiria hivyo kubaki na tatizo hilo milele.

Hayo ni mambo matatu makuu yanayosababisha Afrika kuendelea kubaki nyuma kila siku. wewe Mwafrikaunadhani ni nini kinacho
sababisha afrika kubaki nyuma mpaka leo hii kwani miaka karibu 60 imepita tangu Mkoloni aondokea Tanzania na nchi baadhi za
Afrika.

Maoni yako nini?

Mimi ni mdogo wenu TEENAGER.
Pia jaribu kupitia nyuzi hizi zinaweza kukusaidia sana kaka mkubwa.

A BITTER TRUTH: Kwanini watu weusi walishindwa kwenda Ulaya/Amerika (Ughaibuni) kuwachukua wazungu (Whites) kisha kuwaleta Afrika kuwafanya watumwa?

FOR GREAT THINKERS: Is Africa still a dark continent or a crucial partner in sustaining a better world?
 
Back
Top Bottom