Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,146
- 13,216
HUWA NATAFAKARI SANA
Ninapoona mama haridhiki mtoto akila chakula kidogo hadi anafikia kumchapa ati ale ashibe hadi aone tumbo limejaa
Mtu mzima anakula lakini asiposhiba yaani chakula kidogo haridhiki ...ukitaka kuuona huu ubishi hasa uende wanapouzia chips utasiki 'za kushiba'
Hivi hii asili yake ni nini hasa?
ina tija yoyote kwenye mwili ama akili ya mwanadamu ama ni mazoea tu y kurithi?
Je unapendelea kula sana hadi tumbo liwe gundu kama kindiki?
Fahamu kuwa kula sana hadi kuvimbiwa siyo sifa, bali ni hatari kwa afya yako. Unaweza kusababisha matatizo ya kiafya ambayo yasiyoweza kurekebishika.
Ni vizuri kula chakula kiasi kwa wakati mmoja ili kutunza afya bora na kupunguza kiungulia. Kula chakula kingi kupita uwezo kwa wakati mmoja hufanya tumbo kutanuka zaidi ya uwezo na kusababisha chakula kurudi kwenye njia ya koromeo.