safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,164
- 15,848
Suala la kula kupindukia hata kama mtu hakipendi chakula hiko kivile ni suala limezoeleka hapa duniani pengine wewe msomaji ni katika wao.
Kula chakula kingi sana ni ulafi na kushindwa kujizuia na kuidhibiti nafsi yako ipasavyo.
Kwa kawaida mwili wa binadamu tumbo lake ili ajihisi ameshiba basi akae kama dakika 5 mpaka kumi baada ya kula chakula,
hii maana yake ukijihisi umeshiba huku unaendelea kula basi jua kilichokushibisha ni chakula ulichokula dakika tano nyuma,hiki unachokula sasa hivi kinaenda kukuongezea mauzito na manyama zembe tu.
SIO SALAMA KABISA KUJIHISI UMESHIBA WAKATI UNAENDELEA KULA, NI HATARI KWA AFYA.
Wakati unatia chakula nafsi ya ulafi hujisemea "hapa nakula sana mchana jioni sili ama nakula kidogo tu"
Sio kweli hii ni shetani wa ulafi mkimbie,tia chakula kidogo tu utakachohisi umeshiba bbaada ya kula na sio wakati wa kula.
Unapokula sana ukashiba haswa hii hutanua misuli ya tumbo na kufanya tumbo liwe linatanuka jambo ambalo litafanya uwe na tumbo kubwa ambalo halitopungua kiurahisi kwa sababu kilichotanuka ni misuli.
Salama kwa tumbo lako ni ule chakula alafu usihisi umeshiba kwa kiasi cha tumbo kutanuka.
Ukila ukashibaaa sana kwanza haufeel comfortabble hata kidogo, unahemea juu juu tu.
Ukila ukashiba ndindindi unajinyima fursa ya kununua japo njugu ama tikiti ukitembea kwa sababu hakuna pa kuweka.
Tumbo ni kama kapu safarini, usitie ukalijaza na safari hujaanza, tia machungwa kidogo, then acha nafasi ya vitu vingine kukaa, unaweza kuona vitu vizuri hina pa kuweka, na tumbo hivyo hivyo.
Usione kama tumbo lako ni kwa ajili ya ugali tu, basi ukala mpaka ukinywa maji yanarudi juu. Ugali kidogo acha, tunda kidogo, karanga kidogo maji kidogo n.k
Anza leo kutia chakula ambacho ukimaliza unatamani kula tena, usitie tena hiyo ni nafsi tu pambana nayo, tia chakula cha wastani ukimaliza utajihisi uko comfortable zaidi.
Kula kawaida kuhifadhi mwili wako.
Unafahamu kuwa tumbo linafanyia kazi chakula chako, je uko tayari kutia chakula kingi zaidi ya uwezo wa tumbo kufanya kazi?
Je, unafahamu kuwa unapokula chakula cha wastani kidogo unarahisisha mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula na kupata choo kwa umaridadi kabisa?
Kuna watu hula mpaka ahujitapisha kwa sababu mwanzo alijihisi furaha na utamu wakati anakula lakini alipomaliza kula akakaa dakika tano kumi akajihisi kushiba zaidi na kujiona hayupo sawa, solution anajitapisha.
Kuepuka haya yote unaweza kujipangilia kula matonge kumi tu ya chakula chako yale ya wastani.ndio matonge kumi tu jitahidi kama WEWE SIO MTU WA KAZI NGUMU NA ZA NGUVU.