Kwani Rais Magufuli alitoa ratiba ya kuwapeleka mafisadi mahakamani?

ccm ni kama popo, si ndege wala mnyama, walimshangilia sana kikwete alivyosema pesa si za umma, wakafurahi sana kafulila kuitwa tumbili, wakampigia debe muhongo ni mzalendo arudishwe kazini, leo ndio hao hao wanao msifia magu kuwafikisha mahakamani waliokwapua pesa za umma ambazo rais mstaafu alibariki zichotwe, aisee! inashangaza mno hawa jamaa kila rais kwao ni JEMBE, anatenda vyema..
 
Tusishangilie sana. Hawa jamaa wameshtakiwa, hawajakutwa na hatia au kufungwa bado. Binafsi nadhani hii kesi imeisha kabla haijaanza maana serikali haitaki marais wastaafu wahusishwe na hili sakata wakati ktk akili ya kawaida, walihusika kwa namna moja au nyingine.

Kesi hii itaisha pale itakapotakiwa na mahakama, marais wastaafu waitwe mahakamani kama mashahidi-kwa kupenda au kwa kutopenda (hostile witness). Tutafanya nini kama Rugemalila akisema hela aliruhusiwa azitoe na rais na tunakumbuka rais alisema hela sio za serikali? Mtazuia vip rais asiitwe kama shahidi.

Kwa sisi wanyonge, Sethi na Ruge kushtakiwa na kulala selo inatosha-it is a strong enough political statement. Basi! Mengine ya kukutwa na hatia ni majaliwa (sio PM).
 
ccm ni kama popo, si ndege wala mnyama, walimshangilia sana kikwete alivyosema pesa si za umma, wakafurahi sana kafulila kuitwa tumbili, wakampigia debe muhongo ni mzalendo arudishwe kazini, leo ndio hao hao wanao msifia magu kuwafikisha mahakamani waliokwapua pesa za umma ambazo rais mstaafu alibariki zichotwe, aisee! inashangaza mno hawa jamaa kila rais kwao ni JEMBE, anatenda vyema..
Lakini ni Kikwete huyohuyo wiki iliyopita kambi yetu rasmi ya upinzani tumemuimbia mapambio mjengoni kwamba "tuna imani na Kikwete...........". Kwa maana hii hata sisi tunamuona JEMBE kama wao, na kwahiyo hata sisi ni POPO kabisa.
Mkuu achana na siasa za nchi hii, fanya yako.
 
Tatizo hana bundle, wala hajafungua hiyo clip kusikia kilichomo. Kwahiyo wala hajui kinachoendelea. Naomba umsamehe bure.
NSHAMSAMEHE MKUU, HAJUI ALISEMALO KAMEZESHWA MANENO KAMA KASUKU ,HANA HATA LA KUJIBU
 
Uko sahihi, lakini huo ni mtazamo mmoja tu, kuna mtazamo mwingine. pamoja na kwamba hatujui ratiba yake, lakini tunaweza kuongea machache kuhusu hatua hizo anazochukua. kuna mwelekeo fulani unaonekana. kwa mfano hataki marais waliopita hata watajwe tu. tunajua wanazo kinga kisheria, kwamba hawawezi kushitakiwa. lakini hawana kinga ya kisheria ya kutojadiliwa. hivyo kwa kukataza vyombo vya habari hata wasiwaandike, hapo Rais mwenyewe anavunja katiba inayompa uhuru mtu/chombo kutoa mawazo yake.

Jambo la msingi ni kwamba inatakiwa uhuru wa kutoa maoni ulindwe kwa gharama zote, ili hata Rais anapokosea, akosolewe, na wakosoaji walindwe kisheria.
 
Lowassa anawaumiza vichwa sana, mbona alikwishasema kuwa yeye alikuwa anatekeleza amri kutoka juu, juu yake kulikuwa na makamu wa raisi na raisi
Viongozi wote wa ccm ni wapiga dili. Mbona siku hizi sisikii wakimuita Mtukufu? Hata ile kauli ya hapa kazi siisikii tena
 
Hivi nani angekuwa anaishi kwenye zile nyumba angekataa kuuziwa?!!! Wewe unaepinga nyumba zile kuuzwa kwa wafanyakazi wa serikali, ungekuwa mmoja wao ungekataa na kuhama kupisha mwingine anunue?
 
Nazungumzia ratiba ya kuwapeleka mafisadi kwenye mahakama ya mafisadi na kuwafungulia mashitaka. Inawezekana labda aliwahi kuitoa au kuitaja hiyo ratiba lakini mimi ama sikuiona au sikuisikia.

Hivyo, ndo maana nauliza hapa. Kama kuna anayejua nitamshukuru akitufahamisha sie tusiojua. Aliwahi kuahidi kuwa fulani na fulani atawapeleka kwenye hiyo mahakama na atawapeleka lini?

Kikubwa kilichonifanya niulize ni kile kilichotokea jana kwa wale watu wawili [Harbinder Sing na James Rugemalira] kukamatwa na kupelekwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yao.

Inavyoelekea watu walio wengi hawakuwa wakitegemea kuwa hao jamaa wangekamatwa hiyo jana. Na ndo maana kitendo cha wao kukamatwa kimepokelewa kwa mshangao, furaha, na wasiwasi.

Sasa, kuna wale ambao wanahoji kuwa kama Lowassa ni fisadi kwa nini hapandishwi kizimbani. Ndo nami swali linalonijia ni hilo kwenye kichwa cha mada.

Sijui labda watu walitaka kumwona yeye akiwa wa kwanza kupandishwa kizimbani kujibu hizo tuhuma dhidi yake au sijui wanataka kuona kila siku kuna mtu mpya anapandishwa kizimbani!

Muhula wa huyu Ngosha ni bado sana kuisha. Bado ana zaidi ya miaka miwili ndipo amalize muhula wake wa kwanza.

Tayari keshaonyesha kuwa ni mtu ambaye hatabiriki kirahisi wakati mwingine. Hivyo msije shangaa siku moja mnaamka na kumwona [Lowassa] akiwa 'perp walked' nje ya mahakama ya Kisutu.

Hapo naweza hata kutabiri kuwa wengi wenu mnaohoji kwa nini kama yeye ni fisadi hapandishwi kizimbani, mtabadili magoli na si ajabu mkasema kuwa anaonewa kwa sababu za kisiasa.

Vita dhidi ya ufisadi ni vita ndefu na ni endelevu. Mnapokuwa vitani kamanda hawezi ku-telegraph mipango na matendo yake kwani kufanya hivyo kunaweza kumnufaisha adui na akajipanga vizuri ili akushinde.

Siku ya siku ikifika msije kusema sikuwaambia....na msije kulia na kuhamisha magoli hapa!
Tumezoea kubadilishwa gear angani, ndio maana tunakuwa na pessimism.Hata hivyo isiwe tabu,so far so good.Tutaendelea kusubiri,ila tusije tukabadilishiwa gear angani tena.
 
HIYO TRACK YENU YA NYUMBA ZA SERIKALI HAIICHUJI TU KWENU , NADHANI MAPAKA SASA UNGEKUA USHAITOA KAMA UNGEKUA UMEMSIKILIZA MWENYEKITI WENU WA CHAMA KANDA YA PWANI ALISHALIELEZA HILO VIZURI TU, AU MWENZETU KIZIWI

Mkapa nae hivi ilikuwaje akampa huyu jamaa u-PM kwa awamu zote mbili?
 
...

Vita dhidi ya ufisadi ni vita ndefu na ni endelevu. ...

Siku ya siku ikifika msije kusema sikuwaambia....na msije kulia na kuhamisha magoli hapa!

Ishara ya mvua ni mawingu. Popote mlipo mafisadi kengele ya tahadhari imelia, kama mna uwezo ombeni ardhi ipasuke iwafiche.

Kwa sasa MAFISADI waishi tu kama mashetani wakisubiri siku na saa ya kufikishwa kwa Kaisari.
 
Back
Top Bottom